Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,199
- 1,969
Nakumbuka Rais Obama aliapishwa mara mbili kwa sababu alikosea kiapo chake kwa sababu ya kuweka neno "faithfully" mahali ambapo si pake! Kiapo chake kilikuwa kama ifuatavyo:
ROBERTS: I, Barack Hussein Obama...
OBAMA: I, Barack...
ROBERTS: ... do solemnly swear...
OBAMA: I, Barack Hussein Obama, do solemnly swear...
ROBERTS: ... that I will execute the office of president to the United States faithfully...
OBAMA: ... that I will execute...
ROBERTS: ... faithfully the office of president of the United States...
OBAMA: ... the office of president of the United States faithfully...
Chief Justice administers oath of office again to President Barack Obama at the White House
Kwa upande wa Wabunge wetu walioapa leo, naona wengi wamekosea viapo vyao, aidha kwa kuongeza maneno au kuyaruka au kuyabadilisha, lakini Mheshimiwa Spika, Anne Semamba Makinda amekubali viapo vyao bila matatizo yoyote.
Kiapo chenyewe kina maneno yafuatayo:
"Mimi......................................................, naapa kwamba, nitakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuitumikia kwa moyo wangu wote na kwamba, nitaihifadhi, nitailinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa Sheria iliyowekwa. Ewe Mwenyezi Mungu, nisaidie."
Wafuatao ni Wabunge waliokosea kuapa:
1. Peter Joseph Serukamba: hakutaja neno "wa Tanzania" ie alisema nitailinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano (bila kutaja wa Tanzania)...
2. Haroub Mohamed Shamis: alisema Ewe Mwenyezi Mungu naomba unisaidie. Hilo neno "naomba" halipo kwenye kiapo.
3. Said Musa Zuberi: alisema "na nitaitumikia" badala ya "na kuitumikia," pia alisema Ewe Mwenyezi Mungu, "unisaidie" badala ya "nisaidie."
4. Ayoub Jacob Hashim: alianza na maneno "Bismillah Rahman Rahim" ambayo hayapo kwenye kiapo na alimalizia kwa maneno "inshallah" ambayo hayapo pia kwenye viapo.
5. Asa Osman Hamad: alisema kwa mujibu wa Sheria "iliyoweka" badala ya "iliyowekwa."
6. Hamad Zahara Ally: alisema Ewe Mwenyezi Mungu "naomba" nisaidie. Hilo neno "naomba" halipo kwenye kiapo.
7. Shawalla Azan: alisema "nitahifadhi" badala ya "nitaihifadhi," pia alisema "nitalinda" badala ya "nitailinda."
8. Silima Musa Hamis: alitaja neno "sharia" badala ya "Sheria" ambalo lipo kwenye kiapo. Pia aliongeza neno "amin" ambalo halipo kwenye kiapo.
8. Salim Hassan Turkey: huyu alisema kwa mujibu wa Sheria, hakutaja neno "iliyowekwa."
Hayo ndio makosa niliyoyaona kwa leo, sikufuatilia viapo vya Waheshimiwa Wabunge jana, labda makosa hayo yalikuwepo pia.
Mimi naamini, nikiwa Mwanasheria, Waheshimiwa Wabunge waliokosea viapo vyao wanatakiwa warudie kuapa kwa mujibu wa Kanuni ya 24, Fasili ya 1 ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Mwaka 2007, kama alivyorudia kuapa Rais Obama kwa Sheria za Marekani.
Tujadili.