PAS
JF-Expert Member
- May 3, 2010
- 454
- 8
wabunge wa kuchakachuliwa utawaona tu hata kiapo wanakosea...dahhh kazi kweli kweli
umejuaeje??? yani hawaamini wamefikaje mjengoni
wabunge wa kuchakachuliwa utawaona tu hata kiapo wanakosea...dahhh kazi kweli kweli
Jamani Hivi Wa bunge wengi ni Ngumbalu???
Nakumbuka Rais Obama aliapishwa mara mbili kwa sababu alikosea kiapo chake kwa sababu ya kuweka neno "faithfully" mahali ambapo si pake! Kiapo chake kilikuwa kama ifuatavyo:
ROBERTS: I, Barack Hussein Obama...
OBAMA: I, Barack...
ROBERTS: ... do solemnly swear...
OBAMA: I, Barack Hussein Obama, do solemnly swear...
ROBERTS: ... that I will execute the office of president to the United States faithfully...
OBAMA: ... that I will execute...
ROBERTS: ... faithfully the office of president of the United States...
OBAMA: ... the office of president of the United States faithfully...
Chief Justice administers oath of office again to President Barack Obama at the White House
Kwa upande wa Wabunge wetu walioapa leo, naona wengi wamekosea viapo vyao, aidha kwa kuongeza maneno au kuyaruka au kuyabadilisha, lakini Mheshimiwa Spika, Anne Semamba Makinda amekubali viapo vyao bila matatizo yoyote.
Kiapo chenyewe kina maneno yafuatayo:
"Mimi......................................................, naapa kwamba, nitakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuitumikia kwa moyo wangu wote na kwamba, nitaihifadhi, nitailinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa Sheria iliyowekwa. Ewe Mwenyezi Mungu, nisaidie."
Wafuatao ni Wabunge waliokosea kuapa:
1. Peter Joseph Serukamba: hakutaja neno "wa Tanzania" ie alisema nitailinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano (bila kutaja wa Tanzania)...
2. Haroub Mohamed Shamis: alisema Ewe Mwenyezi Mungu naomba unisaidie. Hilo neno "naomba" halipo kwenye kiapo.
3. Said Musa Zuberi: alisema "na nitaitumikia" badala ya "na kuitumikia," pia alisema Ewe Mwenyezi Mungu, "unisaidie" badala ya "nisaidie."
4. Ayoub Jacob Hashim: alianza na maneno "Bismillah Rahman Rahim" ambayo hayapo kwenye kiapo na alimalizia kwa maneno "inshallah" ambayo hayapo pia kwenye viapo.
5. Asa Osman Hamad: alisema kwa mujibu wa Sheria "iliyoweka" badala ya "iliyowekwa."
6. Hamad Zahara Ally: alisema Ewe Mwenyezi Mungu "naomba" nisaidie. Hilo neno "naomba" halipo kwenye kiapo.
7. Shawalla Azan: alisema "nitahifadhi" badala ya "nitaihifadhi," pia alisema "nitalinda" badala ya "nitailinda."
8. Silima Musa Hamis: alitaja neno "sharia" badala ya "Sheria" ambalo lipo kwenye kiapo. Pia aliongeza neno "amin" ambalo halipo kwenye kiapo.
8. Salim Hassan Turkey: huyu alisema kwa mujibu wa Sheria, hakutaja neno "iliyowekwa."
Hayo ndio makosa niliyoyaona kwa leo, sikufuatilia viapo vya Waheshimiwa Wabunge jana, labda makosa hayo yalikuwepo pia.
Mimi naamini, nikiwa Mwanasheria, Waheshimiwa Wabunge waliokosea viapo vyao wanatakiwa warudie kuapa kwa mujibu wa Kanuni ya 24, Fasili ya 1 ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Mwaka 2007, kama alivyorudia kuapa Rais Obama kwa Sheria za Marekani.
Tujadili.
Inabidi warudie hivyo viapo. Kwa kuwa pale walikuwa wanaapa kwa watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sisi ndio waajiri. Spika ni msimamizi kwa niaba ya wananchi. Kwa hiyo kama hawakuapa inavyotakiwa, ni vyema wakarudia kwa kuwa kuapa si hiyari yao ni lazima
Buchanan, kama sijakosea katika kile kiapo cha Rais Obama sio Obama aliyekosea bali Roberts ndiye aliyekosea hivyo kumfanya arudie kumuapisha tena. Ndio maana alipokuwa anakula kile kiapo utaona Obama anasita kumfuatila alivyosema Roberts kwani aligundua kuwa Roberts alikuwa amekosea!! I stand to be corrected.
Inabidi warudie hivyo viapo. Kwa kuwa pale walikuwa wanaapa kwa watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sisi ndio waajiri. Spika ni msimamizi kwa niaba ya wananchi. Kwa hiyo kama hawakuapa inavyotakiwa, ni vyema wakarudia kwa kuwa kuapa si hiyari yao ni lazima
Hivi ni kwa sababu gani hivi viapo vina hii sentesi: "Ewe Mwenyezi Mungu Nisaidie". Hiki kipengele ndio kinasababisha watu kushika vitabu vya dini kama biblia au kurani wakati wa kuapa. Katiba ya nchi imetoa uhuru wa kuabudu au kutoabudu (Uwe muislamu, mkristo, mhindi, myahudi, au mpagani una haki na uhuru wa kuchagua kufuata imani au kutofuata imani yoyote ile). Jaribu kufikiria. Wahindi wanaabudu MIUNGU wengi (Gods and Goddesses). Kiapo kinalazmisha anayefuata dini ya 'Hindu' kuomba msaada kutoka kwa MUNGU mmoja! Hicho kipengele kwenye kiapo kinachomlazimisha anayeapa kuomba (kusali) nadhani ni 'unconstitutional'.
Nakumbuka Rais Obama aliapishwa mara mbili kwa sababu alikosea kiapo chake kwa sababu ya kuweka neno "faithfully" mahali ambapo si pake! Kiapo chake kilikuwa kama ifuatavyo:
ROBERTS: I, Barack Hussein Obama...
OBAMA: I, Barack...
ROBERTS: ... do solemnly swear...
OBAMA: I, Barack Hussein Obama, do solemnly swear...
ROBERTS: ... that I will execute the office of president to the United States faithfully...
OBAMA: ... that I will execute...
ROBERTS: ... faithfully the office of president of the United States...
OBAMA: ... the office of president of the United States faithfully...
Chief Justice administers oath of office again to President Barack Obama at the White House
Kwa upande wa Wabunge wetu walioapa leo, naona wengi wamekosea viapo vyao, aidha kwa kuongeza maneno au kuyaruka au kuyabadilisha, lakini Mheshimiwa Spika, Anne Semamba Makinda amekubali viapo vyao bila matatizo yoyote.
Kiapo chenyewe kina maneno yafuatayo:
"Mimi......................................................, naapa kwamba, nitakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuitumikia kwa moyo wangu wote na kwamba, nitaihifadhi, nitailinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa Sheria iliyowekwa. Ewe Mwenyezi Mungu, nisaidie."
Wafuatao ni Wabunge waliokosea kuapa:
1. Peter Joseph Serukamba: hakutaja neno "wa Tanzania" ie alisema nitailinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano (bila kutaja wa Tanzania)...
2. Haroub Mohamed Shamis: alisema Ewe Mwenyezi Mungu naomba unisaidie. Hilo neno "naomba" halipo kwenye kiapo.
3. Said Musa Zuberi: alisema "na nitaitumikia" badala ya "na kuitumikia," pia alisema Ewe Mwenyezi Mungu, "unisaidie" badala ya "nisaidie."
4. Ayoub Jacob Hashim: alianza na maneno "Bismillah Rahman Rahim" ambayo hayapo kwenye kiapo na alimalizia kwa maneno "inshallah" ambayo hayapo pia kwenye viapo.
5. Asa Osman Hamad: alisema kwa mujibu wa Sheria "iliyoweka" badala ya "iliyowekwa."
6. Hamad Zahara Ally: alisema Ewe Mwenyezi Mungu "naomba" nisaidie. Hilo neno "naomba" halipo kwenye kiapo.
7. Shawalla Azan: alisema "nitahifadhi" badala ya "nitaihifadhi," pia alisema "nitalinda" badala ya "nitailinda."
8. Silima Musa Hamis: alitaja neno "sharia" badala ya "Sheria" ambalo lipo kwenye kiapo. Pia aliongeza neno "amin" ambalo halipo kwenye kiapo.
8. Salim Hassan Turkey: huyu alisema kwa mujibu wa Sheria, hakutaja neno "iliyowekwa."
Hayo ndio makosa niliyoyaona kwa leo, sikufuatilia viapo vya Waheshimiwa Wabunge jana, labda makosa hayo yalikuwepo pia.
Mimi naamini, nikiwa Mwanasheria, Waheshimiwa Wabunge waliokosea viapo vyao wanatakiwa warudie kuapa kwa mujibu wa Kanuni ya 24, Fasili ya 1 ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Mwaka 2007, kama alivyorudia kuapa Rais Obama kwa Sheria za Marekani.
Tujadili.
1. Stephen Ngonyani (maji marefu) strd 7
2. Livingstone Lusinde - Strd 7
3. Lameck Airo - strd 7
4. Deo Sanga (jah poeple) - strd 7
Hapa kazi ipo kweli kweli! Hivi kama wabunge wote wangekuwa strd 7 baraza la mawaziri itakuwaje? maana kwa katiba ya sasa mawaziri watatoka ndani ya bunge.
Nani waziri wa elimu?
Nani waziri wa mambo ya nje?
Nani waziri wa sheria na katiba?
Ndiyo maana ndiyo mzee nyingi.
Nilikuwa najibu neno NGUMBARU