Wabunge wazoa Sh 90mil kila mmoja kujinunulia Magari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wazoa Sh 90mil kila mmoja kujinunulia Magari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gurudumu, Feb 15, 2011.

 1. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #1
  Feb 15, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Wabunge wazoa Sh90mil kila mmoja

  Tuesday, 15 February 2011
  Mwandishi Wetu, Dodoma


  JUMLA ya Sh3.24 bilioni zimelipwa kwa wabunge ili kuwawezesha kununua magari binafsi kwa ajili ya shughuli za kibunge, imeelezwa.

  Kwa mujibu wa habari hizo kila mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amelipwa Sh90 kwa ajili ya kujinunulia gari.


  Aidha, wabunge hao wapatao 360 wamekatiwa bima ya afya inayotarajiwa kuanza kutumika kabla ya mwezi Juni mwaka huu.


  Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika uzinduzi wa Tawi la Chadema, Mipango Kata ya Miyuji mkoani Dodoma wabunge wa Chadema, walisema kuwa wanashangazwa na hatua ya Rais Kikwete kuweka pikipiki za matairi matatu (Bajaji) kama moja ya vipaumbele vyake ili zitumike kubeba wajawazito wakati wabunge wanalipwa mamilioni.


  Katika hotuba yake ya kulizindua bunge Kikwete alieleza mpango wa serikali yake kununua pikipiki hizo 400 zitakazosambazwa maeneo mbalimbali hasa vijijini kwa ajili ya kuwabebea wajawazito kama njia ya kupunguza matatizo ya usafiri kwenye maeneo hayo.


  "Ndugu zangu hali ni mbaya, siku moja tutafanya maandamano bungeni, sio kutoka nje ya ukumbi. Inashangaza, tumepewa Sh90 milioni za magari kwa wabunge wote, huku bungeni tunajadili bajaji kuwa 'ambulance'(gari ya kubebea wagonjwa),'" alisema mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema.


  Alisema mbali na hilo katika hali inayoonyesha kuwa hospitali za serikali ni mbaya, katika semina iliyofanyika Dar es Salaam hivi karibuni, wabunge waliomba kuwekewa bima za afya, kutibiwa nje ya nchi na katika hospitali binafsi hapa nchini.


  Aliongeza kuwa: Ndoto ya kuiondoa CCM ni 'serious' (thabiti), lakini mkifanya noma ya kupata haki, hiyo imebarikiwa. Kama (CCM) wanafikiri wanaweza kuendesha nchi watakavyo, sasa hawawezi, ninyi vijana msipojitoa kwa sasa nchi itakufa."


  Alikwenda mbali zaidi akisema anaomba wake za viongozi wapate ujauzito na kupakiwa katika bajaji hizo wakati wa uchungu kwenda kujifungua ili waone adha ya usafiri huo itakavyokuwa.


  Akiongea katika mkutano huo naye mbunge Tundu Lissu aliwataka wananchi kutoogopa mabadiliko na kwamba historia haiheshimu watu wanaoogopa.


  ""Historia haiheshimu wanaoogopa, tusije kusahau bei ya mabadiliko, bei yake ni kupigwa, kufungwa hata bei kubwa zaidi ya kifo," alisema Lissu.
  My take: Nakubaliana na uchungu walionao hawa makamanda, nasubiri kuona watafanyaje kuhusu hizo Sh 90mil

   

  Attached Files:

 2. jcb

  jcb JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2011
  Joined: Jul 6, 2010
  Messages: 281
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wabunge wamelipwa milioni 90 kwaajili yakununulia magari............... Mh. Lema mbunge wa Arusha "CHADEMA" anasema ameshangazwa na jambo hili kwani wanajadili Ambulance za Bajaji wakati wao wanapewa 90M kwaajili ya magari pia Bima ya afya kwaajili ya wabunge wanataka wapatiwe katika Hospitali Binafsi na siyo za serikali kutokana na uduni wa huduma katika Hospitali za Serikali....

  Source: MWANANCHI Leo Tar: 15/02/2011
   
 3. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #3
  Feb 15, 2011
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo hizo zenye huduma duni ndo sisi wananchi tutibiwe huko? Kwali aliyeshiba hamjui mwenye njaa!!
   
 4. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #4
  Feb 15, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Hilo la Afya wamechemsha.

  Hospitali za serikali ndiyo Hospitali zitokanazo na Mipango yao Bungeni.
  Kwa nini wanakimbia matokeo ya mipango yao?

  Ubovu wa hospitali za serikali unatokana na Ubovu wa mikakati yao ya Afya Bungeni.

  Sasa watakimbia mambo mamngapi yaliyo matokeo ya Mipango yao Bungeni??


  Hivi karibuni wataomba Wanunuliwe Helcopter kwa sababu Barabara ni mbaya.

   
 5. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #5
  Feb 15, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kwani hata wanaosoma shule za sekondari za kata ni akina nani ndugu? Tuna nchi mbili ndani ya nchi moja!
   
 6. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #6
  Feb 15, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mh. Lema mbunge wa Arusha akatatae hizo milioni 90 ili iwe mfano kwa wabunge wengine na wananchi kwa ujumla!!
   
 7. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #7
  Feb 15, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mtawajua kwa matunda yao!
   
 8. m

  mob JF-Expert Member

  #8
  Feb 15, 2011
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  1. inaonyesha hata fedha kwa ajili ya kutatua tatizo la umeme hapa nchini zipo ila wanazibania tu.ukifanya hesabu ya harakaharaka unaweza ukajua kuliko serikali kununua bajaji 400 wangechukua zile fedha za magari ya wabunge wakanunua ambulance kwa kila jimbo.
  2. pili ni magari gani wanaenda kununua kwa hizo fedha?
  kwa hesabu za nyepesi inatosha kabisha kwa mbunge kununuliwa nissan hard top ambayo haizidi milioni 45 that means tax exception.na fedha zinazobaki zikaelekezwa katika sehemu nyingine ambazo zingeleta tija kwa jamii

  ni vizuri tukahoji ina maana wabunge waliokuwepo kwenye bunge lililopita nao wanapata tena hizo fedha za magari au inakuwaje? je ambao ni wakuu wa mikoa na wabunge pia nao wanapata tena
   
 9. m

  magee Senior Member

  #9
  Feb 15, 2011
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  shame on them,nawalaani wooote waliopokea,hata kama wachadema nao wamepokea tena wao ndo nawalaani zaidi!!!!Lema,mbowe,sweetheart wangu mdee na mylove wangu mnyika nawaalani pia kama mmekubali hizo hela za wanyanganyi hao inhali mwajua nchi yetu na hali za watanzania zilivo ngumu!!Naomba muwe mfano......

  Hela hizo mzipeleke kwenye huduma za jamii,zito kigoma watt wanakalia mawe darasani tena hata madasa wanasomea ya makuti!!UBAO NDIO HAWANA KABISA......we lema arusha vijana ajira hawana kabisa tumia hela hiyo kufanya miradi utakayotengeneza japo ajira 200...

  MMH JAMANI AFYA ETI HOSPITALI BINAFSI KWAHIYO NDOMAANA HAWAZIJALI HOSPITALI ZETU HATA!!!NDO MAANA WAMAMA WAJAWAZITO NA WATOTO WANAKUFA OVYO... NDO MAANA MWANANYAMALA IPO ILIVYO.....SABABU WAO WANATIBIWA TMJ, AGHAKAN....

  MMMH.....INAUMA!!!!!!!!!!!!
   
 10. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #10
  Feb 15, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Unataka afanye kama Pinda alivyokataa shangingi wengine wakaendelea kujinafasi nalo? Na hizo akizikataa ndio zitapelekwa Mwananyamala au Muhimbili?
   
 11. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #11
  Feb 15, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mipango na matokeo mabovu Bungeni ndiyo inawafanya na wao wakimbie hosiptali za Serikali kutokana na mipango yao mibovu ndio maana wanataka wakatibiwe katika hosiptali za binafsi, hii yote inatokana na ubovu wa mikakati katika Sekta ya Afya, kama ndio wamenza kudai hivyo kesho watadai wabadilishiwe magari kwa kuwa hayo waliyonayo sio hadhi yao.

  Wanajadili maslahi yao binafsi badala ya kujadili maslahi ya wananchi waliowatuma bungeni
   
 12. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #12
  Feb 15, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Pinda naye alikuwa anajikosha tu mbona wakati gari linaagizwa hakusema chochote gari lifike ndio ulikatae??? Wakati watu wameishaingia gharama za kuliagiza halafu anasema eti Serikali inataka kubana matumizi
   
 13. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #13
  Feb 15, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kweli, Lema zichukue ukaboreshe huduma za hospitali Arusha!
   
 14. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #14
  Feb 15, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hii inaonyesha kabisa kwamba wabunge wetu wanafanya kazi ya kuhakikisha kwamba wanakuwa kwenye 1st class citizens wakati wapiga kura wao wakiendelea kuogelea kwenye dimbwi la ufukara!
   
 15. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #15
  Feb 15, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Unauliza maswali mazuri na hilo la mwisho ni zuri zaidi. iweje wabunge wa zamani na wapya wote wapewe pesa za magari? Labda watu wa ofisi ya bunge watupe ufafanuzi. Na vipaumbele vyetu ni huduma kwa wananchi au ni welfare ya wanasiasa?
   
 16. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #16
  Feb 15, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ndiyo maana wanakuwa wakali sana kwa mtu yeyote anayehamasisha wananchi kudai haki yao na kuhoji maamuzi mabovu ya serikali, kama haya ya kununulia wabunge magari ya kifahari na kupeleka bakuli kwa wafadhili kuomba wachangie huduma na miradi ya jamii. Kwamba anahatarisha amani na utulivu!!!!
   
 17. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #17
  Feb 15, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Mrs Mallaba:Are you coming to vote? The polling station will be closing in an hour.
  Mr Mallaba :It's raining!
  Mrs Mallaba:So what?
  Mr Mallaba: I can't be bothered. It doesn't matter who I vote for, we always end up worse off. They're all as bad as each other.
  Mrs Mallaba:Well don't complain to me if you don't like the policies of whoever wins.
  Mr Mallaba:I don't think anyone will win. They're predicting a hung parliament.
  Mrs Mallaba:Well if no one bothers to vote, I guess they'll be right. I'll be back in ten.
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Feb 15, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  halafu watu wanakataa lunch ya milioni moja.. right.
   
 19. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #19
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  24 bln!!!..wakati wa kampeni walitembea kwa miguu? hebu nenda mwananyamala wodi ya wazazi uone kufuru hii,one bed wamama 4 na vichanga..
  ubunge sio ajira..kama kweli wapo kihalali kila mbunge achangiwe na wapiga kura wake wa jimboni waliomchagua..sasa mbunge wa ilala anapewa gari yenye thamani sawa na mbunge wa Nkasi kusikokuwa na lami hata ya maonyesho!
   
 20. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #20
  Feb 15, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Yaani nimeipenda sana logic yako.
  Ndiyo maana tangu wiki iliyopita ninafanyia kazi tija na ufanisi wa bunge na wabunge.
  Hizi ndizo sababu zilizowapelekea watunisi na wamisri kutumia nguvu ya umma.
  Kwa sababu una uchaguzi ambao matokeo ya uchaguzi ni kinyume cha matakwa ya wananchi na una bunge ambalo ni rubber stamp, wanafanya uvuvuzela zaidi kuliko kushikisha serikali adabu.
   
Loading...