Wabunge wazoa Sh 90mil kila mmoja kujinunulia Magari

Hakuna kurudisha kila mmoja achukue tu maana hii ni nchi ya wajinga. Tutakoma! Najua hata kingekuwa chama gani lazima haya yangekuwapo tu wala watu wasitake kujikosha hapa.
sio kwamba hata kingekuwa chama gani?JK mwenyewe kashindwa kuweka mfumo mzuri utakaoondoa hili,suluhisho sio kwa wabunge wa CDM kutozichukua hizo 90 bali ni kupigania nchi iwe na mfumo utakaoleta usawa.
Nchi inahitaji mifumo mizuri yenye kuleta usawa kwani Vigogo wa serikali wanachota hela nyingi mno yaan WAZIRI mmoja kumtunza ni sawa na kuwatunza mamia ya wanaichi huku kijijini kwetu
 
hiyo ni bora zaidi ya kuzikataa, maana hazitarudi hazina.zitaishia tu mikononi mwa wanyang'anyi

Ahaa, wazichukue lakini wakazitumie kutoa huduma kwa wananchi majimboni mwao. Lakini ujue huo ni mkopo ambao hukatwa kwenye mshahara wa wabunge, je wananchi watamsadia mbunge kulipa deni hilo?
 
Aaaa Mallaba bana, there must be an impact. Pinda alikataa shangingi ilikuwa ni milestone ingawa wengi walibeza nadhani kuna impact katika uamuzi wa serikali kupanga kununua mashangingi in the future.

Sina uhakika sana kwamba hizo pesa hazitarudi hazina, zingatia Zitto ni waziri wa fedha kivuli bwana atafuatilia.

Lakini jiulize pia impact itakayowapata Chadema kama wakikubali hayo mashangingi. Yaani waswahili wanasema heri nusu shari kuliko shari kamili au siyo mkuu.
Hapo nimekupata mkuu,
lakini basi isiwe kwa CDM pekee ,kuna CUF,NCCR,TLP kwani sio vyama vya upinzani?
 
sio kwamba hata kingekuwa chama gani?JK mwenyewe kashindwa kuweka mfumo mzuri utakaoondoa hili,suluhisho sio kwa wabunge wa CDM kutozichukua hizo 90 bali ni kupigania nchi iwe na mfumo utakaoleta usawa.
Nchi inahitaji mifumo mizuri yenye kuleta usawa kwani Vigogo wa serikali wanachota hela nyingi mno yaan WAZIRI mmoja kumtunza ni sawa na kuwatunza mamia ya wanaichi huku kijijini kwetu

Sasa Marytina dada yangu, si unajua Chadema ni serikali kivuli? Jana Mbowe alitangaza baraza la mawaziri dogo kwa sababu ni sera yao. Iweje leo wachukue hizo pesa kwa sababu wengine wote wanachukua?

Kama ni mifumo, si wao wanatakiwa watuoneshe kwa vitendo badala ya kuendelea kufaidi ndani ya mfumo mbovu huku wanatudanganya kwamba eti ni mbovu?
 
Ahaa, wazichukue lakini wakazitumie kutoa huduma kwa wananchi majimboni mwao. Lakini ujue huo ni mkopo ambao hukatwa kwenye mshahara wa wabunge, je wananchi watamsadia mbunge kulipa deni hilo?
N anapolitumia hilo gari kwani ni nani anayemsaidia kulipa hilo deni?
mbona mchezo ni ule ule tu mkuu?
hapa badala ya kununua VX ya 90M na kuanza kulipa deni, ananunua gari la 40-50M, zinazobaki anaziingiza kwenye miradi jimboni kwake..then anaendelea kulipa deni kama kawa
what is the different?
 
Hapo umesema ukweli,
wabunge karibu wote ni uozo tu.
Ila CDM wakifanya basi itakuwa ni fundisho kwa wengine wote.
sio CDM wazikatae bali washinikize mabadiliko ya kisera yatakayoleta usawa.Nchi hii inaporwa mamiliono ya fedha na watanzania wenzetu inaitajika sera na sheria madhubuti na sio kuzikataa hizo 90,90 kisha wanawaachia shamba nguruwe CCM yalile lote.
 
naanza mkakati wa kuhama tanzania,niahamie nchi jirani kwa lengo la kuitenga tanzania.
sasa naanza kuelewa why nchi kama sudan inagawanywa kuwa south sudan and northen sudan.
 
Sasa Marytina dada yangu, si unajua Chadema ni serikali kivuli? Jana Mbowe alitangaza baraza la mawaziri dogo kwa sababu ni sera yao. Iweje leo wachukue hizo pesa kwa sababu wengine wote wanachukua?

Kama ni mifumo, si wao wanatakiwa watuoneshe kwa vitendo badala ya kuendelea kufaidi ndani ya mfumo mbovu huku wanatudanganya kwamba eti ni mbovu?
nasisitiza nchi hii haina matatizo ya pesa ni tajiri sana ila tatizo ni mgawanyo usiosawa ambao ni zao la sera na sheria zetu.
Sera na sheria madhubuti zitasaidia kuzuia upotevu wa mamilioni ya pesa.
My take:Hata tupewe bajeti ya nchii zote za ulaya na marekani kwa miaka kumi HAKUTAKUWEPO MABADILIKO if watendaji wafuja hela hawatathibitiwa.
 
sio CDM wazikatae bali washinikize mabadiliko ya kisera yatakayoleta usawa.Nchi hii inaporwa mamiliono ya fedha na watanzania wenzetu inaitajika sera na sheria madhubuti na sio kuzikataa hizo 90,90 kisha wanawaachia shamba nguruwe CCM yalile lote.

nakubaliana na wewe kabisa, mabadiliko ya sera ndio kitu muhimu tena sera zenye kuleta usawa. CDM wajipange kwa hilo
 
ngoja tu siku moja watu wakate tamaa waende Jangwani Square.. !!!

Angalau sio Tanzania. Kilo ya sukari sasa hivi ni sh 2000. Watu hawanywi chai majumbani. Hali ni shwari kabisa. Nauli za mabasi na daladala zinapanda wiki ijayo. Hakuna litakalotokea. Wanafunzi waliandamana wiki chache zilizopita. Wamepewa coupon za chakula. Wamenyamaza. Tanzania yetu ni Nchi ya AMANI na UTULIVU bwana. Hatujawahi kuwa na serikali kwa ajili ya WATANZANIA WOTE baada ya Mwalimu kuondoka madarakani.
 
SHILINGI MILIONI 90 KUNUNULIA GARI AL-MAARUFU SHANGINGI!!!!!!!!!!!!!!

HAIKUBALIKI HATA KIDOGO!
Huu ni wizi ambao Watanzania tunatakiwa tuukatae kwa Maandamano ya PEOPLES POWER.Haiwezekani Wabunge wale cake ya Taifa peke yao wakti mamilioni ya Watanzania wako kwenye lindi kubwa la umaskini!

Naichukia sana serikali ya CCM na wanasiasa wote kwa ujumla wao. Ni hivi majuzi tu kama sikosei mwaka jana Pinda alisema yeye hakubaliani na Serikali kununua MASHANGINGI YA MILIONI 90 KWA GARI MOJA. Lakini huyu huyu leo kama Waziri Mkuu amebariki Wabunge wote 360 AKIWEMO YEYE MWENYEWE KUPEWA 90 MILIONI TSHS!!!!!

Gazeti la the CITIZEN la jana likliandika kuhusu SERIKALI KUWA NA HALI MBAYA KIFEDHA NA TAYARI IMEANZA KUTEMBEZA BAKULI KWENYE TAASISI ZA KIMATAIFA ZIKIWEMO WB,IMF NA SCANDINAVIAN COUNTRIES KUOMBA MSAADA WA PESA MAANA AKIBA ILIYOKO KWA SASA INATOSHA KUAGIZA BIDHAAA KWA MIEZI 6 TU! HAPO HAPO WANATAKA KUWALIPA DOWANS BILIONI 94!!!!!!!!!!

KUNA MASWALI YA KUULIZA:NI NINI VIPAUMBELE VYA SERIKALI YA CCM? JE, NI KUWANUNULIA WABUNGE MASHANGINGI YA TSHS.32.4 BILIONI NA KULIPA DOWANS TSHS.94 BILIONI?



USHAURI NA MAONI: KWA WABUNGE WA CHADEMA WAKATAE HIZI PESA ZA SERIKALI NA BADALA YAKE WAPENDEKEZE HAYA YAFUATAYO:
  1. HIZO PESA ZIPUNGUZWE KWA 50% YAANI 45 MILIONI ZIPELEKWE KUIMARISHA SHULE ZA KATA ZISIZOKUWA NA WAALIMU NA KWENYE ZAHANATI VIJIJINI AMBAZO AGHALABU HAZINA MADAWA NA VITANDA.
  2. WABUNGE WATAFUTIE MAGARI YENYE 4WD YENYE THAMANI ISIYOZIDI 45 MILIONI TSHS.
  3. KAMA SERIKALI ITALAZIMISHA HIYO PESA KUWAPA BASI WABUNGE WA CHADEMA WACHUKUE PESA HIYO NA NUSU YAKE WAKAIMARISHE SHULE NA ZAHANATI KWENYE MAJIMBO YAO.
Kama CHADEMA watakubaliani na hizi pesa basi tutakuwa tumejua kuwa WAMETUSALITI na kuwa walichokuwa wanakihubiri wakti wa Kampeni mwaka jana 2010 ni uongo mtupu.

About 2 weeks ago nilihudhuria mkutano wa shule ya Kata ambako waalimu walikutana na wazazi/walezi wa watoto wa shule. Kuna kitu kilishangaza sana wakti mhasibuwa Shule alipotoa taarifa ya fedha. Alisema kwamba waliomba pesa ya UKARABATI WA MAJENGO YA SHULE KWA MWAKA WA FEDHA ULIOPITA 2010/11 NA WAKAPEWA SH.80,000/=!!!!!!!!!!!!!!

Mimi niliwaambia palepale kuwa SERIKALI YA CCM NDIYO INAYOUA ELIMU TANZANIA. WHAT IS 80,000/=TSHS KWA GHARAMA ZA SASA UKIZUNGUMZIA UKARABATI WA JENGO? HII NI NDOO MOJA YA RANGI TU!! HUU NI UHUNI!

Sasa linganisha Tshs.80,000/=ya kukarabati SHULE NZIMA yenye watoto zaidi ya 600 lakini hapa kuna MBUNGE ANAPEWA Tshs.90 milioni kununulia gari? CCM mnatupeleka wapi???? CCM you're NOT SERIOUS. LAZIMA TUTUMIE PEOPLES POWER KUWAONDOA TUMECHOOOOOOOOOOOOKAAAAAAAAAA!
 
Ni vizuri tukakumbuka kwamba fedha hizi walizopewa sio ruzuku. Fedha hizi ni mikopo inayotolewa na mabenki kwa waheshimwa hawa kwa ajili ya ununuzi wa magazi kwa udhamini wa ofisi ua bunge. Kwa hiyo ni hiari kwa wabunge wa zamani na hata hawa wapya kuchukua au kutokuchukua fedha hizo kwani mwisho wa siku wanapaswa kurejesha fedha hizo kwa kipindi watakachokuwa madarakani.

  1. inaonyesha hata fedha kwa ajili ya kutatua tatizo la umeme hapa nchini zipo ila wanazibania tu.ukifanya hesabu ya harakaharaka unaweza ukajua kuliko serikali kununua bajaji 400 wangechukua zile fedha za magari ya wabunge wakanunua ambulance kwa kila jimbo.
  2. pili ni magari gani wanaenda kununua kwa hizo fedha?
kwa hesabu za nyepesi inatosha kabisha kwa mbunge kununuliwa nissan hard top ambayo haizidi milioni 45 that means tax exception.na fedha zinazobaki zikaelekezwa katika sehemu nyingine ambazo zingeleta tija kwa jamii

ni vizuri tukahoji ina maana wabunge waliokuwepo kwenye bunge lililopita nao wanapata tena hizo fedha za magari au inakuwaje? je ambao ni wakuu wa mikoa na wabunge pia nao wanapata tena
 
Mimi nadhani kukataa kupokea hizo hela sio suala la msingi. Wabunge wa CHADEMA pokeeni hizo hela na hzio bima za kutibiwa pokeeni kabisa. Ila tunataka mpeleke hoja binafsi za kupunguza matumizi ya serekali kwa kuondoa hizo hela za gari. Wabunge wakienda bungeni wapewe ticket hata za ndege.
 
UBUNGE RAHA NAMIMI NAJIPANGA 2015 LAZIMA NIWE MJENGONI,NAAMINI 2015 TUTAPEWA MILIONI 200 ZA KUNUNUA mapersonal vehicles
 
Wabunge wetu wapige hatua moja zaidi....

Inasikitisha kwamba katika nchi hii ambayo ina struggle kukamilisha bajeti yake ya 2010/2011, hadi leo wafanyakazi wengi hawajalipwa malimbikizo ya mishahara yao, tunaweza kumpa kila mbunge milioni 90 kwa ajili ya kununua gari la matairi manne kwa ajili ya kusafiria. Tunawapongeza wabunge wetu wa CHADEMA kwa kuliona hili. Sasa baada ya kuanika uozo huu hadharani, ningependa wabunge wetu wapige hatua moja mbele.

Mapendekezo yangu ni kwamba wachukue hizo fedha na wakubaliane kununua magari yasiyozidi milioni 40 au 50. Pesa inayobaki wakubaliane kutekeleza mradi mmoja wenye manufaa kwa wananchi nzima. Wanaweza, kwa mfano, kuamua kutumia hizo pesa kununua madawati katika shule zetu nyingi ambazo watoto wanakaa chini. The impact will be immerse and far reaching.

Wabunge wa CHADEMA wapo 48. Kama watakubaliana kutumia sh 45m kununua magari kila mmoja ataokoa shilingi milioni 45. Kwa ujumla wao watakuwa wameokoa sh 2,160,000,000 (zaidi ya sh. 2bn). Kwa pesa hii wataweza kununua madawati takribani 47,000 yenye uwezo wa kukalisha watoto takribani 188,000! What a service that will be to a country, and ,of course, the political gain will not be insignificant.
 
mm naona wabunge wa chadema wazichuke halafu wazikabidhi kwa chama. Chama kibuni mradi mkubwa ambao utasaidia wananchi na hapo itakuwa ni kumbukumbu kubwa kwa taifa.
 
Back
Top Bottom