Wabunge wasio zidi 50 wangetosha

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,185
18,513
Nimekua nikifuatilia bunge la JMT.. kiukweli wanao jadili na kuchangia hoja za maendeleo, miswada etc ni wabunge walewale kila siku nao hawazidi 50.. najiuliza hawa wengine kazi yao nini? Kupokea posho tuu?
Nadhani moja ya sehemu serikali inapoteza fedha zisizo tumika ni kwa wabunge.. wanalipwa kwa kulala na kutoroka vikao na kuzomea ikitokea.
Nauhakika kabisa wabunge wasio zidi 50 wangeweza kuisimamia serikali vizuri kabisa..
 
Nashauri ungetengeneza orodha ya hao wabunge 50 (jina na chama) ili wananchi waone na kuafiki hiyo orodha. Ninaamini orodha hii haijumuishi Waziri Mkuu, Mawaziri, Naibu Mawaziri, Spika, Naibu Spika na Mwenyekiti wa Bunge.
 
Tuseme uko sahihi. Je hawa wangeweza kuwakilisha majimbo yote Tanzania....? Au kwako kuwakilisha ni kusimama na kuongea bungeni tu?
 
Wabunge wetu wengi wako pale kujitafuti mkate wa kila siku ndio maana awatiki kuonyeshwa live hili wapate muda wa kuchapa usingizi vizuri wanajua muda wa kuedit watatolewa na hivyo wanaichi awatona upuuzi wao
 
Tulipotembelea bunge mwaka 2013 tuliuliza swali kujua kuwa huenda wengine hawachangii kitu zaidi ya kuuchapa usingizi.
Tuliambiwa wanatoa michango kwa maandishi so usione tu hao 50 ukafikiri wengine wako kimnya hapana.
 
Tuseme uko sahihi. Je hawa wangeweza kuwakilisha majimbo yote Tanzania....? Au kwako kuwakilisha ni kusimama na kuongea bungeni tu?
Kwani kwasasa wanaleta faida gani majimboni kwao ikiwa hawawasemei kero zao bungeni?au ww kwako kusimamia ni kuwepo na kuchukua posho bungeni?
 
100% ya wabunge wa Ccm hawapo bungeni kwa ajili ya kuwakilisha wananchi wa majimboni mwao. Wapo kwa ajili ya kuitetea serikali, haijawahi hata siku moja kwa umoja na uwingi wao wakapinga hoja za serikali zisizo na mashiko kwa wananchi wao ni kugonga muhuri tu wa kuidhinisha.
Mfano mdogo ni juzi tu wakati wa kikao cha nne, waziri wa fedha Dr. Mpango alipo wasilisha mpango wa maendeleo wa serikali wa mwaka mmoja. Pamoja na kasoro kubwa kabisa na ya kutisha ambayo mwishowe uliivua nguo serikali waliong'amua madudu hayo ni wapinzani. Lakini wabunge wa Ccm walikuwa kimya na walikuwa tayari kutetea kama serikali ingelazimisha hoja iende kama ilivyo.
Kifupi, WABUNGE WA CCM WANATIA AIBU SANA!
 
Nimekua nikifuatilia bunge la JMT.. kiukweli wanao jadili na kuchangia hoja za maendeleo, miswada etc ni wabunge walewale kila siku nao hawazidi 50.. najiuliza hawa wengine kazi yao nini? Kupokea posho tuu?
Nadhani moja ya sehemu serikali inapoteza fedha zisizo tumika ni kwa wabunge.. wanalipwa kwa kulala na kutoroka vikao na kuzomea ikitokea.
Nauhakika kabisa wabunge wasio zidi 50 wangeweza kuisimamia serikali vizuri kabisa..
Hamsini 3/4 wakiwa ni wa upinzani
 
Kwani kwasasa wanaleta faida gani majimboni kwao ikiwa hawawasemei kero zao bungeni?au ww kwako kusimamia ni kuwepo na kuchukua posho bungeni?

Hata ukiambiwa hutosadiki....nafikiri umeongea tu kufurahisha baraza.
 
Nimekua nikifuatilia bunge la JMT.. kiukweli wanao jadili na kuchangia hoja za maendeleo, miswada etc ni wabunge walewale kila siku nao hawazidi 50.. najiuliza hawa wengine kazi yao nini? Kupokea posho tuu?
Nadhani moja ya sehemu serikali inapoteza fedha zisizo tumika ni kwa wabunge.. wanalipwa kwa kulala na kutoroka vikao na kuzomea ikitokea.
Nauhakika kabisa wabunge wasio zidi 50 wangeweza kuisimamia serikali vizuri kabisa..
Lumumba salama??
 
Tuseme uko sahihi. Je hawa wangeweza kuwakilisha majimbo yote Tanzania....? Au kwako kuwakilisha ni kusimama na kuongea bungeni tu?
nafikiri wangeweza kabisa.. Kigoma zzk kabwe au serukamba angetosha.. singida Tundu lissu..etc..
 
Kuna kuchangia kwa kuongea moja kwa moja na kuchangia kwa maandishi. Mwisho wa siku wote wanatoa michango yao. Kumbuka kuwa kila mbunge hutoa mchango kwa muda usiozidi dakika 15, na wabunge wanakuwa na mambo mengi wanayotaka kuyawasilisha kwa baraza la mawaziri. Binafsi sizipendi zile hoja zinazojengwa kwa nia ya kukashifu elimu za watu, kwa sababu elimu huweza kutafutwa hata wakati mtu ameshakuwa mzee. Halafu wanaowachagua wabunge ni watu ambao wanaishi nao, wanazijua busara zao, wanaujua moyo wa ushirikiano wanaoupata kutoka kwa wabunge wao. Sioni kama ni ustaarabu kumdharau mtu eti kwa sababu ameishia darasa la saba. Anaweza kuwa na elimu ndogo ya darasani lakini akawa na vipaji vingi ambavyo wewe unayejivunia elimu ya chuoni, hukupewa na Mungu.

Huyo huyo aliyeishia darasa la nne anapeleka maji jimboni, anasaidia katika upatikanaji wa mikopo, yuko karibu na watu, hapendi majungu, haendekezi chuki kwa watu. Wewe msomi ambaye una shahada zetu hizi za kibongo ambazo baadhi yake ni magumashi, unaweza ukawa humfikii kwa karama huyo mbunge unayemuona ni kilaza.
 
Back
Top Bottom