Hata wakati wa JK aliwahi kuteua mawaziri kwa kuwapa ubunge wa kuteuliwa, wakala kiapo cha uwaziri na baada ya Bunge kuanza wakala kiapo cha ubunge,
Kumbuka Prof. Mhongo aliteliwa kuwa Mbunge na Waziri wa Nishati na Madini;
Saada Mkuya - Mbunge na N/Fedha
Janeth Mbene - Mbunge na N/Fedha.
Bila shaka katiba na sheria hazija stipulate lazima mbunge ateuliwe na kula kiapo cha ubunge kabla ya kuwa waziri.
Katika hili tukumbuke, kabla ya 1995 haikuwa lazika Waziri Mkuu kuwa Mbunge wa Jimbo.
Warioba na Malecela kwa nyakati zao Rais Mwinyi alikuwa anawapa ubunge na Uwaziri Mkuu papo kwa hapo.
Pengine ipelekwe sheria ya kulazimisha mtu kuwa mbunge kwanza, kula kiapo cha ubunge kabla ya kuteuliwa kwenu cabinet.
Aidha, kwa kuwa hawajala kiapo na kuanza kutimiza majukumu yao, kesho wanaweza kutokea mbele ya Mhe. Spika wakala kiapo cha ubunge kabla ya siku ya kuapishwa rasmi mbele ya Mhe. Rais wa JMT.
Nimechangia kwenye administrative point of view; wanasheria wanaweza kutupa sheria imeweka maelekezo gani?