Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,360
- 29,831
Tulipokea taarifa jana kuwa Mahakama Kuu, chini ya Jaji John Mgeta, kuwa ameyatupilia mbali maombi ya wabunge 19, wakiongozwa na Halima Mdee, waliofungua shauri lao Katika Mahakama hiyo kupinga kuvuliwa uanachama wao na kilichokuwa chama chao cha Chadema.
Ikumbukwe kuwa wabunge hao mwezi November 2020, walivuliwa uanachama wao na Kamati Kuu ya Chadema.
Hata hivyo uamuzi huo wa Chadema "ulidhihakiwa" sana na aliyekuwa Spika wa wakati huo, Job Ndugai na akadai kuwa yeye ndiye mwenye mamlaka ya mwisho wa wabunge gani waendelee kuwepo Bungeni, kwa hiyo akawahakikishia wabunge hao wasitishike na mtu yoyote, kwa kuwa yeye atawalinda.
Kama tujuavyo ni kuwa Spika Ndugai alijiuzuru nafasi hiyo ya u-Spika na aliyerithi nafasi yake, Tulia Ackson, tarehe 16/5/2022 naye alitoa msimamo wake, baada ya kupata barua toka Chadema, kuwa Baraza Kuu (ambalo wabunge hao walikata rufaa zao) chama hicho kimeafiki uamuzi uliofanywa na Kamati Kuu, ya kuwavua uanachama wao, kuwa yeye kama Spika mwenye Shahada ya PhD ya sheria ni lazima afuate sheria na kwa kuwa wabunge hao wamelipeleka suala lao mahakamani, kwa hiyo itabidi asubiri uamuzi huo wa Mahakama, na kama Mahakama nayo italitupilia mbali shauri hilo, itabidi alazimike kuutii mhimili huo wa Mahakama.
Jana Mahakama Kuu imeyatupilia mbali maombi hayo ya akina Halima Mdee na wenzake 18, pia Mahakama hiyo pia imelitupilia mbali ombi lao la kutaka waendelee na ubunge wao.
Kama tujuavyo pia kwa mujibu wa wa Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mbunge yeyote ni LAZIMA awe mwanachama wa chama cha siasa.
Leo tarehe 23/6/2022 wameonekana wabunge hao waliovuliwa uanachama wao na Chadema, baadhi yao wakiuliza maswali ndani ya Bunge.
Nimuulize maswali mepesi tu Spika wetu, Tulia Ackson, je yeye ameamua kwa makusudi kuendelea kuwakumbatia wabunge hao, wakati akijua kuwa hata Mahakama, aliyotuambia kuwa ikifikia uamuzi, hata yeye itabidi aitii Mahakama hiyo?
Je, kwa kuendelea kuwakumbatia wabunge hao, wakati mchakato wote wa kuwavua ubunge umeshafika tamati, je hiyo ni ishara ya wazi kabisa kuwa mhimili wake wa Bunge umeupuuza mhimili mwenzake wa Mahakama na kuuona kuwa si lolote wala chochote?