Wabunge wapya walioteuliwa kuwa Mawaziri wataanza na kiapo kipi, cha Ubunge au cha Uwaziri?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
42,020
2,000
Miaka ya nyuma iliwezekana waziri kuanza na majukumu yake kabla hajala kiapo cha ubunge na hii ilikuwa ni kwa sababu wabunge waliapishwa wakati wa vikao vya bunge.

Je, kwa sasa hawa wabunge wapya akina Dkt. Dorothy na mwenzake itabidi waanze kwa Ndugai ndio waelekee Chamwino?

Nawatakia Dominica yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
 

Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
23,747
2,000
Inawezekana walishaapishwa

Ndugai akisema jioni ile ile baada ya mechi ya Simba na Wa Nigeria alimpigia simu Doroth Gwajima na yule Mwenzie wakakutana ndani ya fence ya Bunge akampa kiapo cha fasta fasta utabisha?
 

Mhemba

Member
Aug 20, 2019
29
45
Dr Doroth Gwajima,je baada ya miaka 5 akawa ajapata ubunge na pia age ya kustaafu kisheria haijafika anarudi ktk nafasi yake y utumishi wa umma,au ukiteuliwa ubunge utumishi wa umma unakuwa terminated? naomba maarifa kidogo.
 

Wyatt Mathewson

JF-Expert Member
Dec 22, 2017
10,992
2,000
Yaani thinking ya Mawe ni very strange aisee

Huwezi kua na thinking process ya hovyo namna hii, hafati common sense, flow ya thinking iliyo sahihi inayofata flowchart ya software build up

Thinking ni art, yaani huyu bwana anatakiwa awe na thinking process kama poetry in motion mpaka wananchi washangae

Cha ajabu huyu jamaa ni full zigzag kama mwehu yaani...what a loss!
 

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
1,054
2,000
Hata wakati wa JK aliwahi kuteua mawaziri kwa kuwapa ubunge wa kuteuliwa, wakala kiapo cha uwaziri na baada ya Bunge kuanza wakala kiapo cha ubunge,

Kumbuka Prof. Mhongo aliteliwa kuwa Mbunge na Waziri wa Nishati na Madini;
Saada Mkuya - Mbunge na N/Fedha

Janeth Mbene - Mbunge na N/Fedha.

Bila shaka katiba na sheria hazija stipulate lazima mbunge ateuliwe na kula kiapo cha ubunge kabla ya kuwa waziri.

Katika hili tukumbuke, kabla ya 1995 haikuwa lazika Waziri Mkuu kuwa Mbunge wa Jimbo.
Warioba na Malecela kwa nyakati zao Rais Mwinyi alikuwa anawapa ubunge na Uwaziri Mkuu papo kwa hapo.

Pengine ipelekwe sheria ya kulazimisha mtu kuwa mbunge kwanza, kula kiapo cha ubunge kabla ya kuteuliwa kwenu cabinet.

Aidha, kwa kuwa hawajala kiapo na kuanza kutimiza majukumu yao, kesho wanaweza kutokea mbele ya Mhe. Spika wakala kiapo cha ubunge kabla ya siku ya kuapishwa rasmi mbele ya Mhe. Rais wa JMT.

Nimechangia kwenye administrative point of view; wanasheria wanaweza kutupa sheria imeweka maelekezo gani?
 

Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
23,747
2,000
Kwa kuwa huyu kateuliwa na Rais, ajira yake inakuwa suspended sio terminated, baada ya ubunge wake kukoma ataandika Barua kwa katibu Mkuu utumishi kuomba kurejea kazini, kurejea kwake hapo kutategemea majibu ya barua hiyo!
Dr Doroth Gwajima,je baada ya miaka 5 akawa ajapata ubunge na pia age ya kustaafu kisheria haijafika anarudi ktk nafasi yake y utumishi wa umma,au ukiteuliwa ubunge utumishi wa umma unakuwa terminated? naomba maarifa kidogo.
 

Mhemba

Member
Aug 20, 2019
29
45
Kwa kuwa huyu kateuliwa na Rais, ajira yake inakuwa suspended sio terminated, baada ya ubunge wake kukoma ataandika Barua kwa katibu Mkuu utumishi kuomba kurejea kazini, kurejea kwake hapo kutategemea majibu ya barua hiyo!
oky asante kwa ufafanuzi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom