Wabunge wapya walioteuliwa kuwa Mawaziri wataanza na kiapo kipi, cha Ubunge au cha Uwaziri?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,754
139,558
Miaka ya nyuma iliwezekana waziri kuanza na majukumu yake kabla hajala kiapo cha ubunge na hii ilikuwa ni kwa sababu wabunge waliapishwa wakati wa vikao vya bunge.

Je, kwa sasa hawa wabunge wapya akina Dkt. Dorothy na mwenzake itabidi waanze kwa Ndugai ndio waelekee Chamwino?

Nawatakia Dominica yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
 
Inawezekana walishaapishwa

Ndugai akisema jioni ile ile baada ya mechi ya Simba na Wa Nigeria alimpigia simu Doroth Gwajima na yule Mwenzie wakakutana ndani ya fence ya Bunge akampa kiapo cha fasta fasta utabisha?
 
Dr Doroth Gwajima,je baada ya miaka 5 akawa ajapata ubunge na pia age ya kustaafu kisheria haijafika anarudi ktk nafasi yake y utumishi wa umma,au ukiteuliwa ubunge utumishi wa umma unakuwa terminated? naomba maarifa kidogo.
 
Hata wakati wa JK aliwahi kuteua mawaziri kwa kuwapa ubunge wa kuteuliwa, wakala kiapo cha uwaziri na baada ya Bunge kuanza wakala kiapo cha ubunge,

Kumbuka Prof. Mhongo aliteliwa kuwa Mbunge na Waziri wa Nishati na Madini;
Saada Mkuya - Mbunge na N/Fedha

Janeth Mbene - Mbunge na N/Fedha.

Bila shaka katiba na sheria hazija stipulate lazima mbunge ateuliwe na kula kiapo cha ubunge kabla ya kuwa waziri.

Katika hili tukumbuke, kabla ya 1995 haikuwa lazika Waziri Mkuu kuwa Mbunge wa Jimbo.
Warioba na Malecela kwa nyakati zao Rais Mwinyi alikuwa anawapa ubunge na Uwaziri Mkuu papo kwa hapo.

Pengine ipelekwe sheria ya kulazimisha mtu kuwa mbunge kwanza, kula kiapo cha ubunge kabla ya kuteuliwa kwenu cabinet.

Aidha, kwa kuwa hawajala kiapo na kuanza kutimiza majukumu yao, kesho wanaweza kutokea mbele ya Mhe. Spika wakala kiapo cha ubunge kabla ya siku ya kuapishwa rasmi mbele ya Mhe. Rais wa JMT.

Nimechangia kwenye administrative point of view; wanasheria wanaweza kutupa sheria imeweka maelekezo gani?
 
Kwa kuwa huyu kateuliwa na Rais, ajira yake inakuwa suspended sio terminated, baada ya ubunge wake kukoma ataandika Barua kwa katibu Mkuu utumishi kuomba kurejea kazini, kurejea kwake hapo kutategemea majibu ya barua hiyo!
Dr Doroth Gwajima,je baada ya miaka 5 akawa ajapata ubunge na pia age ya kustaafu kisheria haijafika anarudi ktk nafasi yake y utumishi wa umma,au ukiteuliwa ubunge utumishi wa umma unakuwa terminated? naomba maarifa kidogo.
 
Kwa kuwa huyu kateuliwa na Rais, ajira yake inakuwa suspended sio terminated, baada ya ubunge wake kukoma ataandika Barua kwa katibu Mkuu utumishi kuomba kurejea kazini, kurejea kwake hapo kutategemea majibu ya barua hiyo!
oky asante kwa ufafanuzi.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom