Wabunge walazimishwe kutembelea majimbo yao..

Rebeca 83

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2016
Posts
15,618
Reaction score
33,475
hello JF,

kushinikiza wabunge wafanye kilichowapeleka bungeni,

Naomba Magufuli aweke kila mbunge atembelee KWA LAZIMA vikao at least 12,

kwa mwaka,

kwenye majimbo yao

kushirikiana na wenyeviti wa halmashauri ,

Wabunge na wenyeviti wa halmashauri washirikiane na wananchi wa majimbo yao ku identify na kubuni plans za jinsi ya kutatua changamoto za majimbo yao...na ku exploit fursa ambazo ziko karibu yao

Na sio kutembelea majimbo yao pande wanapojiskia...

the current system inawafanya wabunge kuwa lazy

Na hivi tumezuiwa bunge kuliona,kuna wabunge wanakua too comfortable huko ndani..LOL

kama sijaeleweka mods nisaidie,,lol
 
Juzi juzi nimemsikia mbunge wa Tarime vijijini nafikiri, anaishi GOBA Dar es salaam. Hii ndio sampobya wabunge karibu wote.
Ni Mbunge wa Tarime Viti Maalum kupitia CHADEMA lkn kubwa zaidi nililokuwa silijui kumbe ni Mzazi Mwenzake na Sal Mwalimu so kiuhalisia hizo nafasi za Special Seat wajanja wamejaza Michepuko yao na ndugu zao kuendeleza BMW system (mfumo wa Baba, Mama na Watoto) respect to Mwalimu wangu Dr. LWAITAMA alikuwa akiitumia saaaana hiii slogan ya BMW.
 
waje kufanya nini wakati hakuna cha kufanya miradi ya maendeleo inatokea ikulu na sio kwa wananchi kama ilivyo zamani au mnataka kudai zile milioni hamsini zenu??
 
ni kweli hakuna cha kufanya?? naamini hii system ya kutoka chini kwenda juu ni nzuri saidi
 
Kutembelea hakuna TIJA kama yale unayoyachukua kutoka kwa wananchi wako HAYATIMILIZWI na kuhemiwa na Watekelezaji.

Kutembelea ni kupea matumaini MFU tu, kwamba tunaye mwakilishi ingawa kiuhalisia HALETI lolote tunalolitaka tulilomwagiza akatusemee!

Leo nafasi hizo zimewekwa mikononi mwa Mhimili uliojichimbia zaidi yani kwa Wakuu wa Wilaya, Mikoana Mawaziri!
 
hii itakua nzuri sana, pia wakitembelea huko wawe na majibu ya kwanini huduma muhimu za kijamii hazipo na wakati wao wapo!

nilipata kwenda kijiji kimoja huko kusini, aisee kwanza barabara tu ukiacha ile main road ya rami huko ndani ni udongo na vumbi tu..

hospitali ipo moja tu tena ya mission, nikaulizia kuhusu viongozi wa kule nikaambiwa huyo mbunge wao ni mzawa wa kule kabisa na amekulia kule lkn tangu achaguliwe kumpata ni shida japo amejenga nyumba kule ya kuwazuga wananchi,

safari moja nakumbuka nilichelewa kutoka kule...saa mbili usiku ndio nikaanza kutoka alafu plus na mvua, kuja kuipata barabara kubwa ni saa saba usiku...

hakufai kupeleka gari kipindi cha mvua kule....ukienda jua linawaka mvua ikakukuta kule hautaweza kurudi, pikipiki wengine tunaziogopa.

wabunge waache kutanua tu mjini warudi makwao huko.
 
mkuu hao wananchi wanaoona kila baada kikao na kikao hawatimiliziwi watafanya kweli kwenye sanduku la kura,vikao Zaidi ya kumi na mbili ni chujio tosha kumuengua mbunge legelege...ndipo hoja yangu ilipolalia….sijasema wafanye mambo kivyao,ofcourse watashirikiana na viongozi wengine katika majimbo yao...ila waongeze contact time
 
Ni Mbunge wa Tarime Viti Maalum kupitia CHADEMA lkn kubwa zaidi nililokuwa silijui kumbe ni Mzazi Mwenzake na Sal Mwalimu so kiuhalisia hizo nafasi za Special Seat wajanja wamejaza Michepuko yao na ndugu zao kuendeleza BMW system (mfumo wa Baba, Mama na Watoto) respect to Mwalimu wangu Dr. LWAITAMA alikuwa akiitumia saaaana hiii slogan ya BMW.
Sio wa Viti maalumu.

Ni Mbunge wa Tarime Mjini Mh. Mwal. Ester Matiko!

Ni nani mwenye uchumi mzuru, Msomi aliyefanya kazi Dar asiye na Makazi Dar Es Salaam?

Watanganyika lazima tujue tofauti ya kimajukumu ya Mbunge na Watendaji wa serikali!

Mbungr kazi zake ni seasonal hazimbani kwamba kika muda awepo katika eneo Bubge lake, hiyo ni kazi ya Watendaji wa serikali.

Kuanzia Watendaji wa vijiji/mitaa, watendaji Kata, Maafisa Tarafa, Wakurugenzi, Wakuu wa Idara katika Wilaya au halmashauri husika na viongizi wa serikali ngazi ya Mkoa na Taifa!

Hawa wenyeviti wa vijiji, Kata, Madiwani na Wabunge ni wasemaji tu wa raisa katika maeneo yao, ambayo shughuli zao za kila siku hazimpasi kuwepo kika siku au kisa saa katika eneo lake!

Tukomeshe hii tabia ya kusema Mbunge kajenga A b c d maana hana fungu wala hausiki moja kwa moja katika hilo.

Hiyo ni kazi ha SERIKALI
 
sisi wananchi ndiyo wakuwalazimisha. Magufili akifanya hivyo ni kuingilia bunge. Wabunge hawawezi kufanya kitu ambacho wananchi hawajaridhia. Ukiona viongozi wanafanya mambo ya ajabu ujue wanachi wameruhusu.
 
Ni Mbunge wa Tarime Viti Maalum kupitia CHADEMA lkn kubwa zaidi nililokuwa silijui kumbe ni Mzazi Mwenzake na Sal Mwalimu so kiuhalisia hizo nafasi za Special Seat wajanja wamejaza Michepuko yao na ndugu zao kuendeleza BMW system (mfumo wa Baba, Mama na Watoto) respect to Mwalimu wangu Dr. LWAITAMA alikuwa akiitumia saaaana hiii slogan ya BMW.
Esther amepigania jimbo tena lile gumu na kulishinda. Msimpakazie na mara nyingi yuko jimboni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hii itakua nzuri sana, pia wakitembelea huko wawe na majibu ya kwanini huduma muhimu za kijamii hazipo na wakati wao wapo!

nilipata kwenda kijiji kimoja huko kusini, aisee kwanza barabara tu ukiacha ile main road ya rami huko ndani ni udongo na vumbi tu..

hospitali ipo moja tu tena ya mission, nikaulizia kuhusu viongozi wa kule nikaambiwa huyo mbunge wao ni mzawa wa kule kabisa na amekulia kule lkn tangu achaguliwe kumpata ni shida japo amejenga nyumba kule ya kuwazuga wananchi,

safari moja nakumbuka nilichelewa kutoka kule...saa mbili usiku ndio nikaanza kutoka alafu plus na mvua, kuja kuipata barabara kubwa ni saa saba usiku...

hakufai kupeleka gari kipindi cha mvua kule....ukienda jua linawaka mvua ikakukuta kule hautaweza kurudi, pikipiki wengine tunaziogopa.

wabunge waache kutanua tu mjini warudi makwao huko.

Asante kwa mchango wako,afu I love you mkaka mpole 😱😱😱😱😎😎😎😎
 
mkuu hao wananchi wanaoona kila baada kikao na kikao hawatimiliziwi watafanya kweli kwenye sanduku la kura,vikao Zaidi ya kumi na mbili ni chujio tosha kumuengua mbunge legelege...ndipo hoja yangu ilipolalia….sijasema wafanye mambo kivyao,ofcourse watashirikiana na viongozi wengine katika majimbo yao...ila waongeze contact time
Mkuu unamaana unataka kuniaminisha kwamba Wah. Wabunge wote waliopo Bungeni wameishi au waliishi na kufanya vikao katika maeneo yao Bunge ndio maana wakashinda ubunge?

Ushindi wa Mbunge wala hauendani na Mbunge kaishi au katembelea eneo Bunge lake mara ngapi.

Naweza kulithibitisha hili kwa mifano lukuki. Rostam Azizi hakuea anaishi Igunga ila watu walimlilia alipojiuzuru!

Nape hakuwa anaishi Mtama au kutembelea kule ndio maana akashinda ubunge!
Je Hawa Ghasia alikuwa anishi na kufanya vikao Mtwara Vijijini mpaka wakampa ubunge?

Siasa zetu hazina uhalisia huo. Watu wanachaguliwa kwa sababu ya umaarufu wao, fedha zao, na kukubalika kwa vyama vyao!....na wala si kwa sababu mbunge flani tunakaa nae hapa!
 
Back
Top Bottom