Hebu fikiria Tanzania ya mawaziri 10 tu, wabunge wachache, wakitumia Land Rover | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hebu fikiria Tanzania ya mawaziri 10 tu, wabunge wachache, wakitumia Land Rover

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sulphadoxine, Jan 9, 2012.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  WAKATI nchi masikini zinaongoza duniani kwa kuwa na serikali kubwa zinazokomba kodi za wananchi wake ili kulipa mishahara mikubwa na marupurupu, serikali za nchi tajiri ni ndogo tu.

  Pamoja na kwamba Rais Jakaya Kikwete alichagua baraza lake na mjadala wa ukubwa wa serikali umeshafungwa, lakini nadhani tuna haki ya kuendelea kujadili suala hili.

  Umuhimu wa kujadili zaidi suala hili unatokana na ukweli kwamba tunatakiwa tupunguze matumizi ya serikali ili bajeti zetu zijazo zijielekeze zaidi kwenye maendeo na si matumizi. Kadhalika itatusaidi katika kuandika katiba mpya.

  Hapa Tanzania ingekuwa busara, mtazamo wangu, tuwe na serikali ndogo, Bunge dogo na watumishi serikalini wawe wachache, wazalendo na waadilifu. Kwa kifupi mimi nilikuwa ninapingana sana na dhana ya kuongeza idadi ya majimbo, kwani ni sawa na mtu kuongeza idadi ya watoto huku hali yako ikiwa duni sana kimaisha.

  Kadhalika dhana ya wabunge wa viti maalum wanaongeza ‘midomo’ ya kula fedha za umma ambazo zingeelekezwa kwenye shughuli nyingine za maendelo, hivyo ni suala ambalo tunatakiwa kulipigia kelele sasa na kuangalia kama lina tija ama la.

  Marekani, yenye uchumi mkubwa, na wananchi wake bila shaka wanapindukia milioni 400, inao mawaziri wachache tu, ni baraza dogo la mawaziri kushinda nchi yoyote hapa Afrika.

  Kwa nini Tanzania ijikaange kwa kuwa na mawaziri na manaibu mawaziri wengi, na wabunge zaidi ya 200?

  Utawala wa Rais Mstaafu, George Walker Bush ulikuwa na mawaziri 14 tu: Waziri wa Mambo ya Nje, wakati huo Colin L. Powell, akaja Dk. Condoleezza Rice, alikuwepo Waziri wa Hazina, Waziri wa Ulinzi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri wa Kilimo, Waziri wa Biashara, Waziri wa Kazi, Waziri wa Afya na Huduma za Binadamu.

  Wengine katika serikali ya Bush walikuwa Waziri wa Usafirishaji, Waziri wa Nishati, Waziri wa Elimu na Waziri wa Mambo ya Maveterani.

  Hawa wakuu wa idara (mawaziri) mishahara yao ilikuwa Dola 161,200 kwa mwaka; na aslani hawatumii rasilimali za umma kama magari, ndege za serikali n.k kuzurura mitaani hata siku za mapumziko na kufanyia sherehe za harusi zao kama huku.

  Bush mwenyewe, mshahara wake ulikuwa Dola 400,000 (zilitozwa kodi) na alawansi ya matumizi kama Dola 50,000 kwa mwaka (hazikutozwa kodi). Masurufu ya safari alilipwa Dola 100,000 kwa mwaka, na viburudisho alilipwa Dola 19,000 bila kutozwa kodi.

  Naam, ni kama alilipwa Dola 569,000 hivi kwa mwaka ambazo ni sawa na Dola 47,416.7 kwa mwezi ambazo ni kama shilingi 61,641,667 tu.
  Miaka ya karibuni, serikali ya Kenya ilipanga kumwongezea mshahara Rais Emilio Mwai Kibaki, ufike Dola za Marekani kama 500,000 hivi kwa mwaka. Ilikuwa kasheshe. Raia walikuja juu na kupinga, Rais wa nchi masikini kulipwa mshahara sawa sawa na Bush wa Marekani!

  Hebu tazama: Makamu wa Rais wa Marekani, Richard (Dicky) Cheney alilipwa mshahara wa mwaka mzima Dola za Marekani 186,300. Zilitozwa kodi na Dola 10,000 za matumizi ambazo hazikutozwa kodi.
  Atakayetaka ubishi atazame website: http: www.whitehouse.gov./vicepresident

  Na kama Rais au Makamu wa Rais angetumia gari au ndege ya serikali kufanyia safari zake binafsi au biashara zake kama hawa vigogo wa hapa Bongo, nakuhakikishia asingekosa kuvuliwa madarakani na mashitaka juu.

  Richard Milhous Nixon (1969-74) wakati wa ile kashfa ya Watergate, alikabiliwa na kesi ya uhaini, akajiuzulu mapema. Makamu wa Rais Spiro T. Agnew, alijiuzulu wakati wa kashfa ya kuhongwa na wafanyabiashara ili awasaidie kukwepa kulipa kodi ya mapato.
  Kumbuka hata jambo dogo kama Rais Bill Clinton kufanya mapenzi Ikulu na Monica Lewinsky, “The Monicagate” aliponea tundu la sindano kuvuliwa madaraka.

  Nataka kusema kwamba, nchi tajiri zina serikali ndogo zinazotumia pesa kidogo na uadilifu wa hali ya juu, wakati watumishi wa umma wakikiuka maadili ya uongozi wanawajibishwa ipasavyo.

  Pesa nyingi zinatekeleza miradi ya maendeleo na Huduma za jamii, siyo kununulia ndege ya Rais kama Gulf stream 550, na rada mbovu za gharama kubwa wakati raia hawana maji ya kunywa, wanakula 'nyasi'.

  Sisi hapa Bongo, pato la nchi linashuka, mfumuko wa bei unaongezeka, mazao yamekosa soko makusanyo ya kodi serikalini yameshuka, serikali bado ni kubwa na watumishi ni wengi tena wezi, wabadhirifu, wazembe, wakwapuzi wa mali ya umma, mafisadi na wala rushwa, wanaoshiriki hujuma kubwa za uchumi wa nchi.

  Kila siku wanadai kuongezewa mishahara na marupurupu.
  Hawa, hawajawa na habari kwamba uchumi wa dunia umeshuka na Tanzania haiko kisiwani isikumbwe na kuanguka huko kwa uchumi.
  Badala ya kufanya kazi kwa tija, wao wanaendeleza uzembe, wizi, kudai rushwa na hujuma anuwai. Yaani, uchumi tegemezi huu wetu ununue mashangingi ya fahari ya kutembelea wakurugenzi wa Halmashauri zilizojaa waporaji wa mali za umma, wakati vijiji havina maji ya bomba, kituo cha afya wala barabara.

  Hawa wanaodai kuongezewa mishahara na posho kila siku wanachukua magari ya umma kama SU, STJ, STK, SM, DFP na mengineyo yanachukuliwa kufanya kazi za harusi za vigogo, na yanaendelea kama ilivyo ada kutembea siku za mapumziko na baada ya kazi. Ipo habari ya ofisa mmoja wa jeshi kupata likizo, kisha akaenda kwao na dereva ambaye ni askari ambaye hayuko likizo pamoja na gari la jeshi. Hebu fikiria namna watu wanavyotumia madaraka vibaya. Huyo dereva alilipwa mwezi mzima kwa kazi gani ya umma?

  Hakuna anayejali. Tunaimba na kuomboleza hakuna anayesikiliza maombolezo ya raia ili kukomesha ufisadi huu.
  Matokeo yake ni kwamba, fedha nyingi za bajeti zinaishia kwenye matumizi ya serikali (kubwa kuliko ya Marekani) halafu hakuna kutekeleza miradi ya maendeleo na huduma za jamii, ila kulipa posho za semina, kulipa mishahara, kununua mashangingi, mafuta na vupili bila kusahau sehemu kubwa kuibiwa kiujanjaujanja.

  Katika halmashauri nyingi nchini, fedha karibu zote za bajeti zinalipa mishahara na posho za madiwani. Fedha chache zinatengengwa kutekeleza miradi ya maendeleo. Barabara vijijini hakuna, hakuna zahanati zenye dawa, wauguzi na matabibu.

  Wakurugenzi na wahandisi wanawapa rafiki na jamaa zao zabuni za ujenzi wa barabara, zahanati na madaraja ili wajenge kwa kiwango duni cha ubora, halafu mamilioni wakagawane.

  Tunapoambiwa kwamba Ahadi ya Maisha Bora itatekelezwa na Halmashauri zenye madiwani na wakurugenzi na watumishi majahili, tunaona serikali inasema vitu visivyotekelezeka.

  Umeme, maji, barabara, reli, ndege n.k kuimarishwa na hawa watumishi wezi na mafisadi? Shule zitajengwa na hawa wezi, zahanati na vituo vya afya vijijini vitajengwa na wala rushwa hawa? Mabarabara yatajengwa kwa kiwango gani na hawa mafisadi?

  Hawa, hawana tamko lolote maarubu (mission statement) akilini mwao. Hawa bado wanagoma na kushinikiza tuwalipe mishahara minono kwa kutumia kodi zetu, wakati pamba na kahawa yetu ilishakosa bei ya maana katika soko la dunia, siyo?

  Yaani, sisi tunapinda mgongo kulipa kodi kubwa, wakati mazao yetu yameshuka, ili wao watumie mabilioni kunywea chai ya asubuhi!
  Ukiwa na akili tunduizi (critical mind) utapendekeza hawa waondolewe serikalini kwa sababu ni genge la wezi waliokabidhiwa kujenga uchumi wa waliowengi katika kipindi kibaya hiki.

  Hawa wezi serikalini hawana dira, hawana rajua ama rujua, ni mbumbumbu wasioona hatari inayotukabili.

  Juni 10 mwaka jana, Rais Jakaya Kikwete alipohutubia wazee wa Dodoma alisema mtikisiko wa uchumi ulisababisha mazao yetu kushuka kwa thamani ya Dola za Marekani milioni 31.
  Makusanyo ya kodi serikalini yalishuka kwa asilimia 9.5, viwanda na miradi ya mamilioni ilishakwama. Pamba ilishapata hasara ya bilioni 18, mauzo ya maua Ughaibuni yalishakuwa hafifu. Rais alisema uwekezaji katika madini kama Tanzanite ulishuka, wafanyakazi takriban 50,000 wakapoteza ajira zao.

  Sasa, kama sisi hatuna ajira kutokana na mtikisiko wa uchumi ambao unasemekana haujatulia huko Ulaya mpaka sasa, tukamuliwe sana kwa kodi, ili kulipa mishahara, mikopo ya mashangingi, posho na upuuzi mwingine, wakati tukikabiliwa na kukosa tiba, maji salama, umeme, barabara na huduma muhimu kwa sababu ya wezi hawa.

  Kama makusanyo ya kodi yanapungua, maana yake ni kwamba serikali itazidi kutoza kodi katika maeneo mengi ili kupata pesa za kuwalipa hawa wazembe na wezi serikalini. Yaani, mazao yetu yanapokosa soko, sisi tunapopoteza ajira, wao walipwe vizuri wakati hawatupi huduma nzuri!
  Ni kwa sababu hii, tunasema tutakuwa tayari kutozwa kodi kwa huduma bora siyo kwa wizi na utapeli.

  Mbali na kusubiri katiba mpya, ninapenda kumshauri Rais Kikwete mwenye uwezo wa kuvnja Baraza la Mawaziri na kuliunda upya afikirie uwezekano wa kulipunguza na kubana zaidi matumizi ya serikali yasiyokuwa ya lazima.

  Watanzani tunataka serikali ndogo, makini na sikivu, serikali yenye mdomo mdogo, macho makubwa sana na masikio makubwa kama ungo.
   
 2. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Enhee, ndio kaka, Rais Nixon alipokabiliwa na kesi ya uhaini alikua anataka kufanya nini, ku commit suicide ?
   
 3. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #3
  Jan 9, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Umegusa engle zote kamanda.Hiyo budget ya mshahara wa makamu wa Rais kwa mwaka ni ndogo ukilinganisha na safari moja ya JK kwenda ulaya na kundi lake utafikiri bendi ya Kofi olomide.Wote tunakumbuka Waziri mkuu mstaafu F. Sumaye alivyofanya ziara siku chache ulaya na kutumia takribani 500mil Tshs.Hawa wanacheza na akili zetu ila ipo siku watajuta kwa uchafu wanaoufanua.Bila kujua ni kuwa wanawatengenezea familia zao maisha mabaya ya baadae, kwasababu ndio watakaokuja kujieleza na kutoa jasho pindi mambo yatakapowaka.
   
 4. Z

  Zlatanmasoud Member

  #4
  Jan 9, 2012
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 71
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nilwahi kupost siku chache zilizopita kuwa waziri mkuu wa Kenya ndie anaengoza kwa kulipwa fedha nyingi duniani kilinganisha na GDP yao. Anapokea zaidi ya dola laki nne za Marekani kwa mwaka wakati Rais wa China mshahara wake ni Dola elf kum na moja tu.

  Hivyo ni wazi utaona Africa viongozi lengo lao ni fedha tu na sio shida za wananchi.
   
 5. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #5
  Jan 9, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ipo siku tu tutawasimamisha kizimbani, wapi Hosni Mubarak na familia yake.? Na hawa akina one watakimbia nchi watake wasitake,
   
 6. Z

  Zlatanmasoud Member

  #6
  Jan 9, 2012
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 71
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yes, the day will come that they will not be protected by their title and I hope time for honouring themselves will soon come to an end.
   
 7. mpinga shetani

  mpinga shetani JF-Expert Member

  #7
  Jan 9, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 3,268
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Rekebisha title maana Landrover za siku hizi bei ni kuanzia milioni 100 dukani
   
 8. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #8
  Jan 9, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,258
  Likes Received: 5,635
  Trophy Points: 280
  Kazi ipo
  kagame alitangaza masaa 24 magari ya mawaziri yote yawe kwenye yadi ya serikali kesho yake akaomba kikao na mawaziri na makatibu wa wizara baada ya hapo saa nane aakaomba apate lunch nao kumbe anawapeleka kwenye godown la kampuni ya toyota akaomba kila mtu achague gari yake anayoipenda wenye akili wakashtuka wajinga wakakimbilia kuchagua ya beo gali akawaambia hayo ni yenu tutaanza kukatana kwenye mambo yetu yaleee...so kila mwezi waziri,katibu anapewa kiasi cha fedha za mafuta ukihonga sawa ukigawa sawa na kama ukisema zimeisha kabla ya tar 31 anakupa memo ujieleze wanakaa kikao watu kumi kukufikiria na mwisho unajibiwa ni sawa ama aombi lako limekataliwa....sio takataka yetu loh kazi ipo
   
Loading...