hii itakua nzuri sana, pia wakitembelea huko wawe na majibu ya kwanini huduma muhimu za kijamii hazipo na wakati wao wapo!
nilipata kwenda kijiji kimoja huko kusini, aisee kwanza barabara tu ukiacha ile main road ya rami huko ndani ni udongo na vumbi tu..
hospitali ipo moja tu tena ya mission, nikaulizia kuhusu viongozi wa kule nikaambiwa huyo mbunge wao ni mzawa wa kule kabisa na amekulia kule lkn tangu achaguliwe kumpata ni shida japo amejenga nyumba kule ya kuwazuga wananchi,
safari moja nakumbuka nilichelewa kutoka kule...saa mbili usiku ndio nikaanza kutoka alafu plus na mvua, kuja kuipata barabara kubwa ni saa saba usiku...
hakufai kupeleka gari kipindi cha mvua kule....ukienda jua linawaka mvua ikakukuta kule hautaweza kurudi, pikipiki wengine tunaziogopa.
wabunge waache kutanua tu mjini warudi makwao huko.