BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,020
Wakuu,
Taarifa niliyoipata toka kwa source wetu ndani ya kikao cha CCM huko Dodoma zinashtua kidogo.
Wabunge wa CCM wamepandisha mori wakitaka Jairo atimuliwe na wakaendelea kutishia kuwa hata Ngeleja naye anatakiwa kuachia ngazi.
Wabunge wa CCM wamemtaka Jairo ajiuzulu kutokana na kashfa ambayo imeletwa na Shelukindo juu ya Barua aliyoandika kuzitaka taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini zitoe 50mil kila moja ili kupata pesa ya ku-lobby ili bajeti ipite.
Wameitaka serikali kupunguza 20% ya bajeti za 'Other Charges' na pesa zote za kujenga majengo ya Wizara ili ziende kwenye UMEME ama vinginevyo bajeti haipiti na Ngeleja atatakiwa kujiuzulu mara moja
Ahsante Mkuu kwa taarifa hii. Mimi bado nadhani huu ni usanii tu wa Wabunge wa CCM ili kujiosha machoni mwa Watanzania lakini hakutakuwa na lolote la maana kwa maana hiyo bajeti ya Nishati itapita na Mawaziri wachovu wa Wizara ile Ngeleja na Malima kuendelea kupeta. Ngoja tusubiri tuone yatakayojiri kule Dodoma.