Wabunge wakomaa: Ngeleja, Jairo watakiwa kuondoka; Pinda ataka mjadala uahirishwe kwa siku 21

Status
Not open for further replies.
Wakuu,

Taarifa niliyoipata toka kwa source wetu ndani ya kikao cha CCM huko Dodoma zinashtua kidogo.

Wabunge wa CCM wamepandisha mori wakitaka Jairo atimuliwe na wakaendelea kutishia kuwa hata Ngeleja naye anatakiwa kuachia ngazi.

Wabunge wa CCM wamemtaka Jairo ajiuzulu kutokana na kashfa ambayo imeletwa na Shelukindo juu ya Barua aliyoandika kuzitaka taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini zitoe 50mil kila moja ili kupata pesa ya ku-lobby ili bajeti ipite.

Wameitaka serikali kupunguza 20% ya bajeti za 'Other Charges' na pesa zote za kujenga majengo ya Wizara ili ziende kwenye UMEME ama vinginevyo bajeti haipiti na Ngeleja atatakiwa kujiuzulu mara moja

Ahsante Mkuu kwa taarifa hii. Mimi bado nadhani huu ni usanii tu wa Wabunge wa CCM ili kujiosha machoni mwa Watanzania lakini hakutakuwa na lolote la maana kwa maana hiyo bajeti ya Nishati itapita na Mawaziri wachovu wa Wizara ile Ngeleja na Malima kuendelea kupeta. Ngoja tusubiri tuone yatakayojiri kule Dodoma.
 
Wakuu,

Taarifa niliyoipata toka kwa source wetu ndani ya kikao cha CCM huko Dodoma zinashtua kidogo.

Wabunge wa CCM wamepandisha mori wakitaka Jairo atimuliwe na wakaendelea kutishia kuwa hata Ngeleja naye anatakiwa kuachia ngazi.

Wabunge wa CCM wamemtaka Jairo ajiuzulu kutokana na kashfa ambayo imeletwa na Shelukindo juu ya Barua aliyoandika kuzitaka taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini zitoe 50mil kila moja ili kupata pesa ya ku-lobby ili bajeti ipite.

Wameitaka serikali kupunguza 20% ya bajeti za 'Other Charges' na pesa zote za kujenga majengo ya Wizara ili ziende kwenye UMEME ama vinginevyo bajeti haipiti na Ngeleja atatakiwa kujiuzulu mara moja

Kumbe wakiamua kukomaa wanaweza? Sasa kwanini wanatuzingua suku zote hizi?
 
Poor Ngeleja. Ningekuwa mimi ndo yeye ningeachia tu hiyo wizara halafu tuone huyo atakayekuja atafanya nini. Manake mimi binafsi sioni wapi Ngeleja alipokosea.
Umeme unakatika kwa saa 24, wizara inatuhumiwa kutoa rushwa bado unaona Ngeleja hajakosea? Uwajibikaji ndio nini?
 
Poor Ngeleja. Ningekuwa mimi ndo yeye ningeachia tu hiyo wizara halafu tuone huyo atakayekuja atafanya nini. Manake mimi binafsi sioni wapi Ngeleja alipokosea.
Ngeleja siyo mbunifu na hana jipya katika ile wizara, sasa anataka abaki kufanya nini? Aende bwana, aje mwingine ambaye akichemka, na yeye anaondoka. Though mimi ningefurahi kama wabunge wangekomaa kumtaka Kikwete ajiuzulu. Maana anapwaya kwelikweli.
 
Wabunge wa CCM wamemtaka Jairo ajiuzulu kutokana na kashfa ambayo imeletwa na Shelukindo juu ya Barua aliyoandika kuzitaka taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini zitoe 50mil kila moja ili kupata pesa ya ku-lobby ili bajeti ipite.

Wameitaka serikali kupunguza 20% ya bajeti za 'Other Charges' na pesa zote za kujenga majengo ya Wizara ili ziende kwenye UMEME ama vinginevyo bajeti haipiti na Ngeleja atatakiwa kujiuzulu mara moja

Kwanini Jairo pekee yake? Na sio wale akina Ngeleja na Malima ambao kuna uwezekano mkubwa na wao kuhusika kutoa rushwa ili bajeti ya Wizara yao ipitishwe?
 
Wakitimiza hili (ccm) la kuikataaa bajeti ya wizara ya madini na nishati...baba wa taifa anafufuka.
Nakubaliana na wewe mkuu siamini kwa magamba kufanya hivyo> naamini wabunge wengi wa ccm ni vilaza tuu!
 
Poor Ngeleja. Ningekuwa mimi ndo yeye ningeachia tu hiyo wizara halafu tuone huyo atakayekuja atafanya nini. Manake mimi binafsi sioni wapi Ngeleja alipokosea.

au, in other words, anachoweza kufanya hasa....
 
Hapa 'mbuzi wa kafara' atakuwa Ngeleja, ... na hivi mfadhili wake mkuu RA kajivua Gamba, angekuwa na busara ajiusulu mapema.
 
La Ngeleja kutakiwa kujiuzulu ni sawa tu kutokana na kiwango cha juu cha incompetence alichoonyesha kam kiongozi wa wizara ..issue kubwa ni bajeti ya wizara hiyo haiaddress tatizo lilopo sasa inazungumzia miradi ya 2015.

Either hata akijiuzulu ndio bajeti ipite bado shida itakuwa pale pale cha msingi ni kuwa bajeti ifanyiwe kazi upya period.
 
Poor Ngeleja. Ningekuwa mimi ndo yeye ningeachia tu hiyo wizara halafu tuone huyo atakayekuja atafanya nini. Manake mimi binafsi sioni wapi Ngeleja alipokosea.
Kazi yake ilikuwa ni kugawa giza..?, when things go wrong the man ontop inabidi uwajibike thats life, as sad as it maybe...,
 
Ngeleja siyo mbunifu na hana jipya katika ile wizara, sasa anataka abaki kufanya nini? Aende bwana, aje mwingine ambaye akichemka, na yeye anaondoka. Though mimi ningefurahi kama wabunge wangekomaa kumtaka Kikwete ajiuzulu. Maana anapwaya kwelikweli.

Haya matatizo hayajaanza mwaka huu nyinyi. Ni ya miaka nenda rudi. Hata Kikwete aliwahi kuongoza hiyo wizara. Je, yeye alikuja na mikakati gani iliyo forward-looking? Na baadaye mtu huyo huyo mkaja kumchagua kwa kishindo cha sunami kuwa raisi....plizzzzzz
 
Wakuu,

Taarifa niliyoipata toka kwa source wetu ndani ya kikao cha CCM huko Dodoma zinashtua kidogo.

Wabunge wa CCM wamepandisha mori wakitaka Jairo atimuliwe na wakaendelea kutishia kuwa hata Ngeleja naye anatakiwa kuachia ngazi.

Wabunge wa CCM wamemtaka Jairo ajiuzulu kutokana na kashfa ambayo imeletwa na Shelukindo juu ya Barua aliyoandika kuzitaka taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini zitoe 50mil kila moja ili kupata pesa ya ku-lobby ili bajeti ipite.

Wameitaka serikali kupunguza 20% ya bajeti za 'Other Charges' na pesa zote za kujenga majengo ya Wizara ili ziende kwenye UMEME ama vinginevyo bajeti haipiti na Ngeleja atatakiwa kujiuzulu mara moja
Shukurani mkuu,mimi naona wangeanza na ngeleja kwanza huyo jairo afatie baadae.
 
Poor Ngeleja. Ningekuwa mimi ndo yeye ningeachia tu hiyo wizara halafu tuone huyo atakayekuja atafanya nini. Manake mimi binafsi sioni wapi Ngeleja alipokosea.

Angekuwa na ubavu huo basi angeshafanya hivyo siku nyingi sana kwa jinsi anavyosakamwa na Watanzania kuhusu hali ya umeme nchini.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom