Hussein Massanza
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 1,016
- 2,195
Ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu, kila kona sasa wanaotamani kuwa wagombea Urais, Ubunge na Udiwani wanapiga jeramba. Wapo wanaosema wameoteshwa, kuna wanaotangaza kuwa wameombwa, ilimradi kila mmoja na gia yake. Kibongo Flava, wanaita "Nitoke Vipi"
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda, ni mmoja wa waliotangaza dhamira ya kuwania uteuzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi. Anataka kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Miaka saba ambayo amekaa ofisini kama Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ameipima na kugundua kwamba imemtosha kuvaa viatu vya ‘Ukuu wa Kaya', kwa mantiki hiyo, anataka yeye ndiye awe raia namba moja wa Tanzania.
Tanzania ni nchi huru! Shukurani za dhati kwa waasisi wa taifa hili, maana wamelifanya liwe uwanja huria kwa kila mwenye kujiona ana viwango na anakidhi vigezo vya kuongoza. Hii ndiyo sababu matangazo ya kuwania urais ni mengi sana hivi sasa. Tuwaache wajitangaze, ni vizuri sana.
Wakichelewa kutia nia, watafanya hivyo muda ukiwa umeenda na matokeo yake, inaweza kusababisha wasichambuliwe kinaga ubaga! Hizi siyo zama za kuuziana mbuzi kwenye gunia, tunamtaka mgombea tumjue mapema, tumjadili, tumchambue kisha tumwambie nenda mbele wananchi wataamua, au tuwaeleze wapiga kura kwamba huyo hapana.
Upigaji kura kuchagua viongozi siyo mchezo wa karata tatu au ‘ana ana anado', kwamba aliyebahatika ndiye apite, la hasha! Chumba cha kupigia kura ni cha uamuzi, mpigakura anapoingia ndani yake, anakwenda kuamua matarajio ya nchi yake kwa miaka mitano inayofuata.
Kutokana na kukosekana misingi mizuri ya kudadavua wagombea, imekuwa ni kawaida kwa nchi yetu kupitisha wagombea ambao mpaka siku ya uchaguzi, mpigakura anakuwa hajui, huyo anayekwenda kumchagua ajenda yake ni ipi! Anaambiwa tu anafaa, naye anaamini.
Umakini tafadhali; Majaliwa ya nchi yetu yanatokana na aina ya viongozi ambao wanachaguliwa. Mfumo wa sasa umekuwa ukisababisa wananchi kunung'unika chini kwa chini, wakijutia kura zao. Ni wazi walipiga kura bila kumjua hasa wanayemchagua. Wangemjua, wasingepigwa butwaa.
PINDA MTOTO WA MKULIMA;
Ni mwanasiasa hasa, maana ni mvumilivu sana. Ameshaitwa mzigo na wabunge mpaka wa chama chake ambao yeye ndiye mwenyekiti wao (kwenye caucus ya CCM), lakini hajawahi kukunja moyo na kumuwekea kisasi yeyote.
Amekuwa akiruhusu kusemwa waziwazi. Si mtu mwenye makeke. Ni mfanya siasa za kistaarabu ambaye mipango yake haiendani na kumuumiza mwingine. Hapa Mtoto wa Mkulima anajitofautisha na wale wanasiasa ambao ili wajiimarishe lazima wawadhuru wengine kisiasa.
Si mwanasiasa mwenye makundi. Hatakigawa chama chake pale kitakapofanya uamuzi wa kumteua kuwa mgombea Urais, maana amekuwa na sifa ya kupita katikati ya kila kundi. Pinda amewahi kuchukizana na nani? Lini aliendesha siasa za majitaka dhidi ya mwenzake?
Ameonesha ni kiongozi mwenye kuridhika na kiasi. Hana tamaa ya kujilimbikizia mali. Maisha yake yametupa picha ya wazi kuwa endapo atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akistaafu atarudi kijijini kusimamia mashamba yake.
Maisha ya Pinda ni ya Mtanzania wa kawaida sana. Kwa wasifu huo, ni wazi kila mwananchi wa taifa hili ni mwenzake. Alisoma kwa tabu kijijini, jitihada zake ndizo ziligeuza dhiki alizokuwa nazo kuwa neema.
Amefanya kazi Ikulu, ni mwanausalama, alishakuwa Waziri wa Tamisemi, ukiongezea na Uwaziri Mkuu, hutakuwa na shaka kwamba hii nchi anaijua vizuri. Matatizo ya kila mkoa, halmashauri, misingi ya ulinzi na usalama wa nchi, matatizo ya wananchi na Utanzania, hakuna asichokijua.
Ni mwenye huruma sana, alilizwa mno na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino). Alifanya ziara Kanda ya Ziwa ambayo kwa kiwango kikubwa, ilisaidia kupunguza kasi ya mauaji hayo ambayo mkondo wake ni ushirikina.
Kama Urais ungekuwa ni sifa hizi peke yake, kwa hakika ningejitoa bila malipo wala ahadi yoyote, kusambaza ujumbe ili umfikie kila Mtanzania aweze kumchagua, maana akipewa kiti, upele utakuwa umepata mkunaji. Tatizo Urais ni zaidi ya hapo.
MASHAKA YAPO HUKU;
Pinda amekuwa Waziri Mkuu mpole kiasi kwamba Watanzania hawajui rangi yake halisi ni ipi. Hakemei ufisadi, amewaacha mawaziri wafanye wanavyotaka utadhani hawana wasimamizi. Upole huu umesababisha swali hili ambalo halijapata majibu mpaka leo; Je, ni mpole au mwoga?
Pinda akiwa Waziri Mkuu, amekuwa ‘Smart' kupita kiasi, kwamba hataki lawama. Kila jambo anajiweka mbali. Hataki kuingilia majukumu ya Rais, vilevile anakwepea mbali kuonekana mnoko kwa mawaziri, hataki kuwabana hata kidogo.
Miaka saba ya Uwaziri Mkuu wake, amesababisha Rais Jakaya Kikwete asemwe vibaya mno kwamba hachukui hatua. Kuna maeneo mengi ambayo Pinda alibaki bubu bila kuyasemea wala kuyachukulia hatua, akingoja Rais atamke. Pinda ni Mr. Too Much Smart.
Wapo wanaosema kuwa upole wake na kushindwa kwake kuchukua hatua, ni kwa sababu anafanya kazi chini ya mtu. Kwamba akikabidhiwa rungu aongoze nchi, Watanzania watasuuzika na roho zao. Hoja; Akiwa Waziri Mkuu ameshindwa, akichaguliwa kuwa Rais ndiyo ataweza.
Wanaoamini Pinda anaweza, inabidi waje na hoja tofauti ambayo itamuuza mtu wao, haya maneno ya bei rahisi kuwa alishindwa kutekeleza majukumu yake akiwa Waziri Mkuu kwa sababu anafanya kazi chini ya mtu ni ya ovyo sana.
Katika zama hizi, tunahitaji watu ambao wanaweza kuongoza bila vyeo. Kwa kulielewa hili, Pinda angeonesha mfano kwa kushughulikia majukumu yake kwa uimara wa hali ya juu, pale Rais angelega, yeye angewajibika kwa vitendo.
Kama anashindwa kutimiza majukumu yake ipasayo na kumsaidia Rais kwa vitendo, maana yake ni muoga. Hatutaki Rais mficha kucha, eti anasubiri awe pale juu ndiyo achomoe makucha yake. Kwa Jakaya tu anakuwa mnyonge, mkimya, je, utakapofika wakati wa kusuguana na mataifa makubwa kwa ajili ya maslahi ya nchi yetu, si atatugeuza kondoo?
Kikatiba, Waziri Mkuu ndiye Mtendaji Mkuu wa shughuli za kila siku za Serikali, vilevile ndiye msimamizi mkuu wa rasilimali za nchi. Laiti angekitumia cheo chake sawasawa, leo hii kusingekuwa na mtamani Urais mwenye umaarufu kuliko yeye.
Ni kwa sababu hakufunga vizuri kamba za viatu vyake, Uwaziri Mkuu umempwaya na ametokea kuwa Waziri Mkuu asiyeaminika, asiyeeleweka ajenda zake na asiye na umaarufu kuliko watangulizi wake wote? Hesabu halafu atajwe aliyezidiwa umaarufu na Pinda.
Hayati Mwalimu Julius Nyerere, hayati Rashid Mfaume Kawawa, hayati Edward Moringe Sokoine, Cleopar David Msuya, Salim Ahmed Salim, Joseph Sinde Warioba, Fredrick Tluway Sumaye na Edward Ngoyai Lowassa. Kila mmoja kwa zama zake, nani amezidiwa na Pinda?
Akiwa Waziri Mkuu, amenusurika kuondolewa kwenye kiti mara nne. Pengine kwa ustaarabu, angeweza kutangaza kujiuzulu lakini amekuwa sugu, king'ang'anizi. Hoja zote nne ambazo zilitaka kumng'oa, zilikuwa nzito, zinazojitosheleza.
Hoja ya kwanza; Tamko lake kwamba wanaoua albino nao wauawe, lilikuwa baya sana katika nchi inayofuata misingi ya sheria za Kimahakama. Mahakama ndiyo chombo pekee kinachotoa hukumu ya ama kumtia hatiani mtu au la!
Pinda alihamasisha Kanda ya Ziwa kuwaua watu wanaoamini ndiyo wahusika wa mauaji ya albino. Kwa mantiki hiyo, aliruhusu kujichukulia sheria mkononi. Taifa likiwa bado linateswa na mauaji ya vikongwe kwa imani za kishirikina, ikiwa ni mkondo uleule wa kujichukulia sheria mkononi, Waziri Mkuu akatoa kauli hiyo.
Mwaka 2009, aliyekuwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohamed, aliwasilisha bungeni hoja ya kutaka ufafanuzi wa matamshi ya Pinda, ikiwa ni hatua ya awali kabla ya kuanza mchakato wa kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani naye.
Pinda kwa kusoma alama za nyakati, aliomba radhi, akalia bungeni, akasamehewa. Hata hivyo, haikuondoa ukweli kuwa alionesha udhaifu mkubwa kwa tamko lake. Ni kweli alitekwa kihisia na mauaji ya albino, ila alipaswa kujitambua yeye ni kiongozi, hivyo angedhibiti hisia zake kabla ya kutamka.
Mwaka 2012, ili kurahisisha uwajibikaji wa Serikali kuwatimua mawaziri nane walioonekana wamefanya madudu, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, alifanikisha kukusanya saini za wabunge 70 na kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.
Rais Kikwete alimwokoa Pinda kwa kuwatimua mawaziri waliokuwa wanalalamikiwa. Hata hivyo, hiyo haikuondoa ukweli kwamba Pinda alishindwa kutimiza majukumu yake ndiyo maana mawaziri husika walifanya madudu yeye akiwa hajui chochote.
Mwaka 2014, Pinda ataukumbuka sana, maana alinusurika mara mbili. Kashfa ya Oparesheni Tokomeza Ujangili, iliyosababisha vifo vya Watanzania wasio na hatia, wengine kuteswa na kunyanyaswa kijinsia, vilevile wafugaji kuporwa mifugo yao, aliponea chupuchupu.
Wabunge walitaka Pinda awajibike kwa sababu ana kila kitu lakini alishindwa kuzuia unyama huo kutendeka. Hata baada ya matukio yote, hakuwahi kutoa tamko kukemea, alikaa kimya utadhani hakuna kilichotokea.
Hoja ya nne ambayo chupuchupu imng'oe ni kashfa ya uchotwaji wa fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow. Ripoti ya PAC ilimtaka awajibike, wabunge wengi pia walimtaka ang'oke, aliokolewa mwishoni na kamati ya maridhiano iliyotengeneza mapendekezo nane.
Pamoja na kuokoka, itambulike kuwa Pinda alilidanganya bunge kwamba fedha za Tegeta Escrow si za umma na kwamba ni za wabia wa IPTL. Uchunguzi usio na shaka umebaini kuwa kuna fedha za Tanesco (fedha za umma) na nyingine ndiyo za IPTL. Hapo Pinda unamuweka kundi gani?
Pinda hajui mamlaka zinasemaje? Mwaka 2011, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, alibainika kuandika barua ya kuhamasisha rushwa kusaidia bajeti ya wizara yake kupita bungeni. Ilikuwa kashfa kubwa na wabunge walitaka hatua za haraka zichukuliwe.
Waziri Mkuu kama msimamizi wa shughuli za serikali bungeni, alitakiwa kutoa tamko, aliposimama, alisema anangoja kauli ya Rais kwa sababu ndiye pekee mwenye mamlaka ya kumchukulia hatua za kinidhamu Jairo.
Siku iliyofuata, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, aliita waandishi wa habari na kueleza kuwa mamlaka ya kinidhamu kwa makatibu wakuu yapo chini yake, kisha akatangaza kumsimamisha kazi Jairo. Hapo Pinda unamwelezeaje?
Fedha za Escrow zimeporwa akiwa Waziri Mkuu, upande mwingine inatajwa kwamba lipo fungu lilimlenga ili kusaidia mipango yake ya kuukwaa Urais. Je, kwa muktadha huo, unadhani sura ya nchi itakuwaje chini ya Rais Mizengo Peter Kayanza Pinda?
Tuachene na hii hoja mpya kwamba alipokea hongo ya shilingi bilioni 7 kutoka kwa makampuni yanayoingiza sukari nchini ili kumsaidia katika mipango yake ya Urais. Kwa hongo hiyo, naye akaruhusu vibali ambavyo vimeleta kashfa kubwa ya sukari iliyop sasa. Labda hapa wanamsingizia, maana Wabongo kwa kutunga!
Hizo hoja nyingine anazijibu vipi? Tusisahau na ile kauli yake ya "wapigwe tu" ambayo kwa hakika inakwenda kinyume na misingi ya utawala bora, vilevile si rafiki wa haki za binadamu. Akiwa Rais itakuwaje?
SALAMU KWA CCM;
Katika uchaguzi, Wamarekani hutazama sana kitu kinachoitwa "Coattail Effect", ikiwa na maana ya nguvu ya mgombea wa nafasi ya juu kusaidia kura za wagombea wa nafasi za chini katika chama chake. Rais kwa Maseneta na Baraza la Wawakilishi.
Ukiteua mgombea wa nafasi ya juu mwenye nguvu ndogo, inaweza kusababisha chama kipoteze viti vingi vya chini (hii inaitwa Negative Coattail Effect). Mgombea wa nafasi ya juu anapozidiwa kura na wagombea wa chini, inaitwa Reverse Coattail Effect.
Kwa Tanzania, Uchaguzi Mkuu 2010, Chadema kilipata Coattail Effect kwa sababu nguvu ya Dk. Willibroad Slaa ilifanikisha kupata wabunge na madiwani wengi,hivyo kuunda Kambi ya Upinzani Bungeni na kushikilia mamlaka kwenye halmashauri kadhaa.
Uchaguzi Mkuu wa Marekani mwaka 1964, Chama cha Republican kilionja machungu ya Negative Coattail, kilipomsimamisha mgombea dhaifu, Barry Goldwater ambaye alishindwa vibaya, vilevile chama chake kikapoteza viti vingi kwenye Baraza la Wawakilishi.
Kwa matokeo hayo, Rais Lyndon Johnson akawa na kazi nyepesi ya kupitisha ajenda zake kwa sababu wawakilishi wengi wanatokea kwenye chama chake.
CCM wanapaswa kumwangalia sana Pinda kwa sababu umaarufu wake ni mdogo na hang'ai kabisa. Kumpitisha kuwa Mgombea Urais, siyo tu kwamba itawawia rahisi wapinzani kumwangusha, bali pia anaweza kusababisha chama chake kipoteze viti vingi, hivyo kuugulia matokeo ya Negative Coattail.
By Luqman Maloto