Wambugani
JF-Expert Member
- Dec 8, 2007
- 1,757
- 276
Wabunge wabaini ufisadi katika umilikishaji hoteli za serikali
Mikataba yote iliyoingiwa kati ya mwekezaji wa Kampuni ya Hotels and Lodges (T) Ltd (Tahi) na iliyokuwa Tume ya Rais ya Kubinafsisha Mashirika ya Umma (PSRC) kwenye hoteli zilizokuwa za serikali, itapitiwa upya na Bunge, baada ya kubainika kuwapo ufisadi katika umilikishwaji wa hoteli hizo. Hali hiyo imeisababishia hasara serikali kwa kupata asilimia 10 ya gharama zote za uendeshaji wa hoteli hizo.
Aidha imebainika kuwa hoteli hizo zinailipa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) dola nane kwa hoteli zenye hadhi ya juu na za chini dola nne, huku wenyewe wakitoza dola 350 kwa zile za kiwango cha chini na dola 700 hadi 1,000 kwa hoteli za juu, gharama ambayo ni ndogo.
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ilibaini hayo ilipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na wajumbe wake kulala katika moja ya hoteli za Lobo na Seronera, ambazo ni miongoni mwa hoteli zilizopewa mikataba isiyo na ukomo.
Akizungumza mbele ya Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa, Allan Kijazi, Mwenyekiti wa kamati hiyo, James Lembeli, alisema hali hiyo haiwezi kuvumiliwa na itawapasa wasitishe mara moja mikataba yote iliyoingiwa kati ya mwekezaji, PSRC na Tanapa ili waione na washauriane cha kufanya kwa maslahi yataifa.
Lembeli alisema kuwapo kwa mikataba hiyo, kumesababisha kiburi kwa baadhi ya wawekezaji na kuwanyanyasa baadhi ya wazawa kwa kuwakatalia kulala kwenye baadhi ya hoteli hizo.
Hoteli, ambazo zilikuwa za serikali na kuuzwa kwa wawekezaji ni Lobo, Ngorongoro, Lake Manyara, Sabasaba, Mount Meru, Ikweta, Dodoma Hotel, New Arusha na New Safari.
Alisema iwapo sheria haimruhusu mtu kumiliki kitu ndani ya hifadhi na kuhoji inakuwaje sheria hiyo hiyo imruhusu mtu kumiliki jengo ndani ya hifadhi na hakuna kilichoendelezwa tofauti na hoteli nyingine kama ya Mount Meru, New Arusha, New Afrika na Dodoma, ambazo zimekarabatiwa vizuri.
"Lakini siyo unyanyasaji huo tu. Hata ukiongea na wafanyakazi kama hapa tulipolala Hoteli ya Lobo, hawa watu wanalipwa Sh. 120,000 tu. Hizi ni fedha kidogo ukilinganisha na kazi wanazofanya usiku na mchana," alisema.
Mjumbe wa kamati hiyo, Christopher Ole Sendeka, alisema mikataba yote inayohusu uwekezaji katika hoteli zilizokuwa za serikali lazima ziitishwe mara moja bungeni, kwa ajili ya kupitiwa upya na kuona kinachoendelea.
Alisema haiwezekani Bunge likakaa kimya, huku mikataba isiyo na maslahi kwa Taifa ikiendelea kutumika bila nchi kunufaika chochote, huku wawekezaji wakinufaika kwa kiwango cha juu.
Sendeka alisema kilichofanyika ni kama uhuni, sababu hoteli nyingi kama ya Lobo, hakuna jipya lililoongezwa, kuanzia ukubwa wa chumba, mataulo na vitu vyote vinavyotumika ni vile vilivyokuwa vya serikali kabla ya kuuza.
"Hawa wawekezaji sana sana wamepaka rangi tu basi. Lakini tangu miaka 10 iliyopita walipochukua hoteli hizi, hakuna jipya kabisa zaidi ya kupaka rangi. Hata ukubwa wa vitanda ni ule ule na mashuka kila kitu ni kile kile," alisema.
Kijazi aliiambia kamati hiyo kwa masikitiko kuwa kiasi wanacholipa wawekezaji ni kidogo sana, cha asilimia 10 ya gharama zote wanazotoza, hali inayowanufaisha zaidi wao kuliko nchi.
"Lakini kibaya zaidi mikataba iliyoingiwa na hawa watu ya ubinafsishaji ni ya milele. Haina ukomo, kiasi kwamba, serikali ikitaka hoteli hizi, lazima wanunue kwa bei watakazopanga wao," alisema.
Alisema hata wao hawakushirikishwa katika mikataba hiyo kama wadau muhimu wa kusimamia rasilimali za Taifa, bali walisikia tu watu wameitana jijini Dar es Salaam na ikasainiwa na wao hawafahamu kwa undani chochote.
CHANZO: NIPASHE