Wabunge wabaini ufisadi mwingine katika Umilikishaji wa Mahoteli

Wambugani

Wambugani

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2007
Messages
1,758
Points
1,225
Wambugani

Wambugani

JF-Expert Member
Joined Dec 8, 2007
1,758 1,225
Wabunge wabaini ufisadi katika umilikishaji hoteli za serikali

Mikataba yote iliyoingiwa kati ya mwekezaji wa Kampuni ya Hotels and Lodges (T) Ltd (Tahi) na iliyokuwa Tume ya Rais ya Kubinafsisha Mashirika ya Umma (PSRC) kwenye hoteli zilizokuwa za serikali, itapitiwa upya na Bunge, baada ya kubainika kuwapo ufisadi katika umilikishwaji wa hoteli hizo. Hali hiyo imeisababishia hasara serikali kwa kupata asilimia 10 ya gharama zote za uendeshaji wa hoteli hizo.

Aidha imebainika kuwa hoteli hizo zinailipa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) dola nane kwa hoteli zenye hadhi ya juu na za chini dola nne, huku wenyewe wakitoza dola 350 kwa zile za kiwango cha chini na dola 700 hadi 1,000 kwa hoteli za juu, gharama ambayo ni ndogo.

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ilibaini hayo ilipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na wajumbe wake kulala katika moja ya hoteli za Lobo na Seronera, ambazo ni miongoni mwa hoteli zilizopewa mikataba isiyo na ukomo.

Akizungumza mbele ya Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa, Allan Kijazi, Mwenyekiti wa kamati hiyo, James Lembeli, alisema hali hiyo haiwezi kuvumiliwa na itawapasa wasitishe mara moja mikataba yote iliyoingiwa kati ya mwekezaji, PSRC na Tanapa ili waione na washauriane cha kufanya kwa maslahi yataifa.

Lembeli alisema kuwapo kwa mikataba hiyo, kumesababisha kiburi kwa baadhi ya wawekezaji na kuwanyanyasa baadhi ya wazawa kwa kuwakatalia kulala kwenye baadhi ya hoteli hizo.

Hoteli, ambazo zilikuwa za serikali na kuuzwa kwa wawekezaji ni Lobo, Ngorongoro, Lake Manyara, Sabasaba, Mount Meru, Ikweta, Dodoma Hotel, New Arusha na New Safari.

Alisema iwapo sheria haimruhusu mtu kumiliki kitu ndani ya hifadhi na kuhoji inakuwaje sheria hiyo hiyo imruhusu mtu kumiliki jengo ndani ya hifadhi na hakuna kilichoendelezwa tofauti na hoteli nyingine kama ya Mount Meru, New Arusha, New Afrika na Dodoma, ambazo zimekarabatiwa vizuri.

"Lakini siyo unyanyasaji huo tu. Hata ukiongea na wafanyakazi kama hapa tulipolala Hoteli ya Lobo, hawa watu wanalipwa Sh. 120,000 tu. Hizi ni fedha kidogo ukilinganisha na kazi wanazofanya usiku na mchana," alisema.

Mjumbe wa kamati hiyo, Christopher Ole Sendeka, alisema mikataba yote inayohusu uwekezaji katika hoteli zilizokuwa za serikali lazima ziitishwe mara moja bungeni, kwa ajili ya kupitiwa upya na kuona kinachoendelea.

Alisema haiwezekani Bunge likakaa kimya, huku mikataba isiyo na maslahi kwa Taifa ikiendelea kutumika bila nchi kunufaika chochote, huku wawekezaji wakinufaika kwa kiwango cha juu.

Sendeka alisema kilichofanyika ni kama uhuni, sababu hoteli nyingi kama ya Lobo, hakuna jipya lililoongezwa, kuanzia ukubwa wa chumba, mataulo na vitu vyote vinavyotumika ni vile vilivyokuwa vya serikali kabla ya kuuza.

"Hawa wawekezaji sana sana wamepaka rangi tu basi. Lakini tangu miaka 10 iliyopita walipochukua hoteli hizi, hakuna jipya kabisa zaidi ya kupaka rangi. Hata ukubwa wa vitanda ni ule ule na mashuka kila kitu ni kile kile," alisema.

Kijazi aliiambia kamati hiyo kwa masikitiko kuwa kiasi wanacholipa wawekezaji ni kidogo sana, cha asilimia 10 ya gharama zote wanazotoza, hali inayowanufaisha zaidi wao kuliko nchi.

"Lakini kibaya zaidi mikataba iliyoingiwa na hawa watu ya ubinafsishaji ni ya milele. Haina ukomo, kiasi kwamba, serikali ikitaka hoteli hizi, lazima wanunue kwa bei watakazopanga wao," alisema.

Alisema hata wao hawakushirikishwa katika mikataba hiyo kama wadau muhimu wa kusimamia rasilimali za Taifa, bali walisikia tu watu wameitana jijini Dar es Salaam na ikasainiwa na wao hawafahamu kwa undani chochote.
CHANZO: NIPASHE
 
Wambugani

Wambugani

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2007
Messages
1,758
Points
1,225
Wambugani

Wambugani

JF-Expert Member
Joined Dec 8, 2007
1,758 1,225
Sijui ni nani anakula na hawa wahindi wa hoteli zilizokuwa za TAHI?
 
TOWNSEND

TOWNSEND

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2011
Messages
2,601
Points
1,225
TOWNSEND

TOWNSEND

JF-Expert Member
Joined May 8, 2011
2,601 1,225
tuone kama kina nape na kinana watasaidia hotel kurudi wakiwa aruchuga au wataenda majukwaani tu na blah blah
 
Thegreatcardina

Thegreatcardina

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2009
Messages
399
Points
225
Thegreatcardina

Thegreatcardina

JF-Expert Member
Joined Mar 29, 2009
399 225
Hizo hotel ni za Watanzania wenzetu wasiovuja jasho. wanajua kila kitu na namna walizivyogawana. Hata serikali inajua kila hotel ni ya nani. Hao Wahindi tusiwasingizie lolote, wapo kama maboya tu hapo. Hivi hata wewe sasa hivi ukapewa U-CEO wa kampuni ambayo mikataba ya siri ilisainiwa Mauritius kukutambulisha kuwa Mr. X wa Tanzania ndiye owner wa kampuni lakini wewe utajulikana kule kwa kila jambo na huruhusiwi kumtaja mpaka ukutane naye huko Mauritius, na unapigwa mshahara wa kufa mtu, utakataa. Na tulivyo na njaa kutokana na kupishana na maisha bora. Ukikumbuka kuwa wewe sio mzawa wa nchi hii.
 
S

swrc

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2012
Messages
442
Points
0
Age
49
S

swrc

JF-Expert Member
Joined Jun 17, 2012
442 0
mambo haya yote yalifanyika kipindi cha mkapa na ni hao hao ccm, sasa leo watatuambiaje kuhusu usafi wao?
 
kijenge

kijenge

Senior Member
Joined
Mar 9, 2012
Messages
177
Points
250
kijenge

kijenge

Senior Member
Joined Mar 9, 2012
177 250
Mkapa ndio aliuza vitu vyote vya nchi hii kuanzia vyumba za serikali,viwanda,mahotel na mashamba,reli huyu niwa kuuwa mbele ya halai na magufuli kwa kuuza nyumba zetu.kinana meli yake inashikwa na meno ya ndovu huko china anapewa ukatibu mkuu wa ccm.
 
Wambugani

Wambugani

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2007
Messages
1,758
Points
1,225
Wambugani

Wambugani

JF-Expert Member
Joined Dec 8, 2007
1,758 1,225
TwinRoom.jpg Vitanda vya Lake Manyara Hotel
 
M

Mndokanyi

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2012
Messages
629
Points
195
Age
42
M

Mndokanyi

JF-Expert Member
Joined Sep 6, 2012
629 195
Kweli CCM na viongozi wake wametufikisha pabaya.Kila jambo wanalogusa lina elements za ufisadi,kweli ni hatari.
 
Takalani Sesame

Takalani Sesame

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2008
Messages
588
Points
170
Takalani Sesame

Takalani Sesame

JF-Expert Member
Joined Jun 24, 2008
588 170
Ufisadi ni kila mahali. Nchi imeoza.
 
S

Savannah

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
239
Points
0
Age
67
S

Savannah

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2012
239 0
waTZ kuendelea na utawala wa CCM tujilaumu wenyewe.
 
commited

commited

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Messages
1,617
Points
1,195
Age
28
commited

commited

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2012
1,617 1,195
ndugu zangu inasikitisha sana nimeiona sasa hivi itv hapa (taarifa ya habari ya sa2.00 usiku, 21/11/2012) , kamati ya lembeli inashangaa kuwa hoteli hizo zilizokuwa za serikali zoote zimeuzwa hata bila tanapa kushirikiswa (kijazi alifunguka), lakini pia inasikitisha jamaa wa mahoteli wanacharge USD 300 kwa kichwa halafu serikali inapata USD 4 TU.

Nakala, kwa rejazo, cuf ngangari, nape, wasira, kinana, mangula,nchemba, lizt1,mdizi, et al....
 
Somoche

Somoche

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2010
Messages
4,164
Points
2,000
Somoche

Somoche

JF-Expert Member
Joined Oct 6, 2010
4,164 2,000
Kwa ufupi mwenye Hotel anapata dola 350 sawa na sh 549500 kwa siku halafu serikali hii chovu dhaifu dhofli Fisadi inapata dola 4 yaani elf 6 na kitu...haya mambo unaweza kujinyonga kwa hasira!!!!!! stuuuuupiiidddd
 
Ciril

Ciril

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2011
Messages
6,914
Points
2,000
Ciril

Ciril

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2011
6,914 2,000
Wabunge wabaini ufisadi katika umilikishaji hoteli za serikali

Mikataba yote iliyoingiwa kati ya mwekezaji wa Kampuni ya Hotels and Lodges (T) Ltd (Tahi) na iliyokuwa Tume ya Rais ya Kubinafsisha Mashirika ya Umma (PSRC) kwenye hoteli zilizokuwa za serikali, itapitiwa upya na Bunge, baada ya kubainika kuwapo ufisadi katika umilikishwaji wa hoteli hizo. Hali hiyo imeisababishia hasara serikali kwa kupata asilimia 10 ya gharama zote za uendeshaji wa hoteli hizo.

Aidha imebainika kuwa hoteli hizo zinailipa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) dola nane kwa hoteli zenye hadhi ya juu na za chini dola nne, huku wenyewe wakitoza dola 350 kwa zile za kiwango cha chini na dola 700 hadi 1,000 kwa hoteli za juu, gharama ambayo ni ndogo.

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ilibaini hayo ilipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na wajumbe wake kulala katika moja ya hoteli za Lobo na Seronera, ambazo ni miongoni mwa hoteli zilizopewa mikataba isiyo na ukomo.

Akizungumza mbele ya Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa, Allan Kijazi, Mwenyekiti wa kamati hiyo, James Lembeli, alisema hali hiyo haiwezi kuvumiliwa na itawapasa wasitishe mara moja mikataba yote iliyoingiwa kati ya mwekezaji, PSRC na Tanapa ili waione na washauriane cha kufanya kwa maslahi yataifa.

Lembeli alisema kuwapo kwa mikataba hiyo, kumesababisha kiburi kwa baadhi ya wawekezaji na kuwanyanyasa baadhi ya wazawa kwa kuwakatalia kulala kwenye baadhi ya hoteli hizo.

Hoteli, ambazo zilikuwa za serikali na kuuzwa kwa wawekezaji ni Lobo, Ngorongoro, Lake Manyara, Sabasaba, Mount Meru, Ikweta, Dodoma Hotel, New Arusha na New Safari.

Alisema iwapo sheria haimruhusu mtu kumiliki kitu ndani ya hifadhi na kuhoji inakuwaje sheria hiyo hiyo imruhusu mtu kumiliki jengo ndani ya hifadhi na hakuna kilichoendelezwa tofauti na hoteli nyingine kama ya Mount Meru, New Arusha, New Afrika na Dodoma, ambazo zimekarabatiwa vizuri.

“Lakini siyo unyanyasaji huo tu. Hata ukiongea na wafanyakazi kama hapa tulipolala Hoteli ya Lobo, hawa watu wanalipwa Sh. 120,000 tu. Hizi ni fedha kidogo ukilinganisha na kazi wanazofanya usiku na mchana,” alisema.

Mjumbe wa kamati hiyo, Christopher Ole Sendeka, alisema mikataba yote inayohusu uwekezaji katika hoteli zilizokuwa za serikali lazima ziitishwe mara moja bungeni, kwa ajili ya kupitiwa upya na kuona kinachoendelea.

Alisema haiwezekani Bunge likakaa kimya, huku mikataba isiyo na maslahi kwa Taifa ikiendelea kutumika bila nchi kunufaika chochote, huku wawekezaji wakinufaika kwa kiwango cha juu.

Sendeka alisema kilichofanyika ni kama uhuni, sababu hoteli nyingi kama ya Lobo, hakuna jipya lililoongezwa, kuanzia ukubwa wa chumba, mataulo na vitu vyote vinavyotumika ni vile vilivyokuwa vya serikali kabla ya kuuza.

“Hawa wawekezaji sana sana wamepaka rangi tu basi. Lakini tangu miaka 10 iliyopita walipochukua hoteli hizi, hakuna jipya kabisa zaidi ya kupaka rangi. Hata ukubwa wa vitanda ni ule ule na mashuka kila kitu ni kile kile,” alisema.

Kijazi aliiambia kamati hiyo kwa masikitiko kuwa kiasi wanacholipa wawekezaji ni kidogo sana, cha asilimia 10 ya gharama zote wanazotoza, hali inayowanufaisha zaidi wao kuliko nchi.

“Lakini kibaya zaidi mikataba iliyoingiwa na hawa watu ya ubinafsishaji ni ya milele. Haina ukomo, kiasi kwamba, serikali ikitaka hoteli hizi, lazima wanunue kwa bei watakazopanga wao,” alisema.

Alisema hata wao hawakushirikishwa katika mikataba hiyo kama wadau muhimu wa kusimamia rasilimali za Taifa, bali walisikia tu watu wameitana jijini Dar es Salaam na ikasainiwa na wao hawafahamu kwa undani chochote.
CHANZO: NIPASHE
watu wanaingia mikataba na wawekezaji kwa maslahi binafsi sio kwa maslahi ya taifa,tusitarajie miujiza kama hatutabadilisha mfumo huu(mmbovu) wote kuanza moja sio ujinga.Wacha nijinywee glasi ya maji walau iniongezee nguvu ktk mwili wangu nikapambane na kibarua changu kariakoo kesho.
 
A

adolay

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2011
Messages
8,952
Points
2,000
A

adolay

JF-Expert Member
Joined Dec 8, 2011
8,952 2,000
Kuna wale jamaa pumbavu hivi ambao hujifanya ccm ni kila kitu, si wajitokeze kutetea upuuzi huu kama kawaida yao

Tukisema wana vichwa vya panzi na kujaza pumba vichwani mwao wanaona tunawaonea.

Jamani tanzania ni yetu wote kwa nini wachache waibe kila kitu? watufanye tulipe makodi makubwa huku fedha zikiibwa usiku na mchana? wanatusababishia mfumko wa bei, elimu na afya duni - choyo,ubinafsi na ulafi vimewatawala.
 
L

lebabu11

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2010
Messages
1,849
Points
2,000
L

lebabu11

JF-Expert Member
Joined Mar 27, 2010
1,849 2,000
Makosa mengi yamefanywa na sasa hivi tunatakiwa kuyarekebisha kama ifuatavyo;

1. Kusitisha mikataba yote ya kifisadi,

2. Kuwashughulikia wote waliotuingiza katika mikataba hiyo kwa kuanzia kuwawajibisha kwa kuwaondoa kwenye ofisi za uma, kuhakikisha kwamba hawapati nafasi yoyote ya kuongoza uma, kuwatangaza kuwa ni maadui wa uma, ikifuatiwa na kuangalia uwezekano wa kuwafungulia mashtaka na kuwafilisi.

3. Kuhakikisha kuwa mambo kama hayo hayarudiwi tena kwa kutekeleza kwa ufanisi mambo tajwa hapo juu (1 na 2) ili iwe fundisho kwao na kwa wengine ambao wana tabia na mawazo kama yao.
 
CHASHA FARMING

CHASHA FARMING

Verified Member
Joined
Jun 4, 2011
Messages
6,436
Points
2,000
CHASHA FARMING

CHASHA FARMING

Verified Member
Joined Jun 4, 2011
6,436 2,000
Inauma sana Nikikumbuka Hizi Hoteli najua wengi watakuwa hawazijui lakini inasikitisha sana Ndo wadanganyika wenzangu

-Hizi hoteli ziliuzwa Bei ya Kutupwa paoja na kwamba ni Moja ya Hoteli nzuri na zente Mandhari ya hali ya Juu
 
CHASHA FARMING

CHASHA FARMING

Verified Member
Joined
Jun 4, 2011
Messages
6,436
Points
2,000
CHASHA FARMING

CHASHA FARMING

Verified Member
Joined Jun 4, 2011
6,436 2,000
Chakusikitisha zaidi ni Kwamba Huyu Mwarabu baada ya Kununu hizo Hoteli alitimua Familia za Wafanyakazi zlizo kuwa zikiishi kwenye Kotazi za Hoteli hizo na Kwa Hoteli ya Lobo kule Serengeti Huyu Mwarabu alifunga kabisa shule ya Msingi iliyo kuwa ikutumiwa na watoto wa Wafanyakazi wa Hizi hoteli, can you imagine mwekezaji anakuja na kuamulu shule ya Msingi ifungwe, Ilikuwa ikiitwa SHULE YA MSINGI LOBO
 
A

adolay

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2011
Messages
8,952
Points
2,000
A

adolay

JF-Expert Member
Joined Dec 8, 2011
8,952 2,000
CCm na siasa za kulindana, ndiyo sababu wakoteyari kulitumikisha jeshi la polisi kiccm kukandamiza demokrasia wakihofu pindi

wakitolewa madarakani lazima washughulikiwe.

Tunakilasababu kuichukia ccm kwa kushindwa kuiletea nchi maendeleo ya kweli wakati tunakila kitu. Hatakama sio kesho wala kesho

kutwa wataondoka tu madarakani, hakika patakuwa na kilio na kusaga meno.
 
Forum statistics

Threads 1,296,628
Members 498,713
Posts 31,254,170
Top