Wabunge wa UKAWA wameshasaini Bungeni!

Wabunge wa UKAWA wameshasaini Bungeni!

Kazi ni kubwa na safari ni ndefu, lakini ACT ni wasafiri daraja la pili ndani ya treni ya CCM ndio maana wanajaribu kupotosha mantiki ya pingamizi la CHADEMA kuhusu matangazo ya matokeo ya kura za Uraisi yaliyompa Magufuli Ushindi Haramu.
 
Barbarosa hiyo Posho hawalipwi kama hisani bali ni stahili yao inayotokana na wao kuchaguliwa na wananchi, pia Magufuli hana hiyari ya kuwalipa au kutokuwalipa kwani hata yeye hizo pesa hazitokani na kuuza Mifugo ya Familia yao bali zinatokana na Kodi tunazotozwa watanzania wote waliomchagua na wasiomchagua Magufuli!! Na wala hizo Posho hazitokani na fedha zilizopatikana kwa kuuza kadi za CCM hivyo wabunge toka vyama vingine wakose sifa za kupewa!!

Kutokwenda kwenye sherehe za kuapishwa kwa Magufuli hakuko Kikatiba bali hizo posho zinatokana na sheria zilizotungwa kwa kufuatisha Katiba iliyopo inayoshabikiwa na CCM hata kama ni Hovyo kabisa!! Kuna ujinga miongoni mwetu kuona kama serikali inafanya mambo kwa hisani jambo ambalo si sahihi.

Nini maana ya kutokumtambua JPM na serikali yake? Na je Bunge sio sehemu ya serikali?
 
Nini maana ya kutokumtambua JPM na serikali yake? Na je Bunge sio sehemu ya serikali?

what kind of stupid question is this?ina maana hadi leo hujui kuwa bunge na serikali ni mihimili tofauti!!!!
 
Tofautisha bunge na uwanja wa taifa,huko uwanjani kulikua na kipi cha kusheherekea?
 
what kind of stupid question is this?ina maana hadi leo hujui kuwa bunge na serikali ni mihimili tofauti!!!!

Hawa jamaa wanatia Huruma anaongea jambo ambalo halijui! Hii nchi imeingilia, inawezekana kabisa hajui hata maana ya Muhimili! God forvigove them they know not what they are argueing!
 
what kind of stupid question is this?ina maana hadi leo hujui kuwa bunge na serikali ni mihimili tofauti!!!!
Pengine utakuwa hujanielewa nilichokuwa namaanisha ! Kuna kitu kinaitwa State and the head of state is the President ambaye UKAWA hawamtambui, Sate ni muunganiko wa serikali, bunge na mahakama though kila moja ina majukumu na madaraka tofauti, narudi tena kwenye swali, kama ukawa hawamtambui head of the state kwanini washiriki shughuli za bunge ambalo ni sehemu ya muhimili wa nchi?
 
Hizo posho ni stahiki yao, hazilipwi na CCM. Watafanya kama walivyofanya kwa Kikwete. Wataondoka bungeni kwenye bunge litakalohutubiwa na JPM

Ili iweje? Huyo huyo JPM atawaletea miswada watatoka povu kuijadili, wakibanwa watatoka nje; bado miswada itapita bila tabu yo yote. Ni kujilisha upepo tu...
 
Lakini hauoni kama kuna unafiki hapo? Kwamba ukawa hawamtambui Raisi wa JMTZ lkn wanasaini kwenda Bungeni kushiriki ufunguzi wa Bunge utakaofanywa na Raisi wa JMTZ ambaye hawamtambui na kuapa kwa jina lake Raisi wa JMTZ, sasa kama siyo kuchanganyikiwa ni nini?

Wenyewe wanasign kuhudhuria kikao cha bunge ili kama kweli atakuja, basi watapishana naye ili aonje raha ya kutolewa mfukoni mwa mwenyekiti
 
Mr mchange umeishiwa hoja, kama umekosa ubunge haribu tens after 5
 
Pengine utakuwa hujanielewa nilichokuwa namaanisha ! Kuna kitu kinaitwa State and the head of state is the President ambaye UKAWA hawamtambui, Sate ni muunganiko wa serikali, bunge na mahakama though kila moja ina majukumu na madaraka tofauti, narudi tena kwenye swali, kama ukawa hawamtambui head of the state kwanini washiriki shughuli za bunge ambalo ni sehemu ya muhimili wa nchi?
hapo sasa unazungumzia dola na bunge...may be we can start from there.
 
Nina uhakika mpaka kufikia muda huu zitto atakuwa ameshampa onyo huyu jamaa!! Mwenzao anajitahidi kujenga maadili wao ndo kwanzaaa wanazidi kutibua.

Katibua nini hapo sijaelewa
 
Akil za pdf hiz toleo la kwanza div 5!nan kakwambia wanaapa kwa jina la rais? Kama kitu hujui uliza tu!
Lakini hauoni kama kuna unafiki hapo? Kwamba ukawa hawamtambui Raisi wa JMTZ lkn wanasaini kwenda Bungeni kushiriki ufunguzi wa Bunge utakaofanywa na Raisi wa JMTZ ambaye hawamtambui na kuapa kwa jina lake Raisi wa JMTZ, sasa kama siyo kuchanganyikiwa ni nini?
 
Nilikuwa Kigoma juzi
Ukitafuta chama kinaitwa ACT Wazalendo utakikosa
Sema chama cha Mawese

Kama kinaitwa mawese inamaana ni chama cha watu wa Kigoma.

Ni upuuzi chama kuonekana Kibaha ambako hakuna mawese!!!!
 
Back
Top Bottom