Wabunge wa UKAWA wameshasaini Bungeni!

Wabunge wa UKAWA wameshasaini Bungeni!

Lakini hauoni kama kuna unafiki hapo? Kwamba ukawa hawamtambui Raisi wa JMTZ lkn wanasaini kwenda Bungeni kushiriki ufunguzi wa Bunge utakaofanywa na Raisi wa JMTZ ambaye hawamtambui na kuapa kwa jina lake Raisi wa JMTZ, sasa kama siyo kuchanganyikiwa ni nini?

Kimwili watakuwepo lakini kimawazo watakuwa wako nje kabisa....!!!!
 
Ni lazima kama Wabunge wa Ukawa wataapa kwa Jina la Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa TanZania ambaye kwa bahati mbaya hawamtambui sasa hapo inakuwaje tena?

Na isitoshe ili wao walipwe posho ni lazima Serikali iliyo chini ya Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania iliridhie na kukubali kuwalipa sasa kama wao hawaitambui Serikali yake ina maana kwa akili ya kawaida hana mamlaka (Raisi na Serikali yake) ya kuidhinisha fedha ya Umma kwa maana kwa kujibu wa ukawa yeye siyo Raisi hahali!

Hivi wewe unamiliki tu kichwa kama nazi au kuna ubongo humu au usaha?

Wanaapa kwa jina la rais. how? Wanaapa kwa lipi?

Kuhurhuria bunge na Posho zipo kikatiba na kisheria sio msaada au hisani ya mtu...
!
Soma vizuri posti za wenye akili ujielelimishe ili uwe unaweka post za maana. No wonder chama chenu kimepata mbunge mmoja tu na ambaye angalau anaakili. Igeni mfano wake vinginevyo hoja za kijinga kama hizi msahau chama chenu kukua.
 
Barbarosa hiyo Posho hawalipwi kama hisani bali ni stahili yao inayotokana na wao kuchaguliwa na wananchi, pia Magufuli hana hiyari ya kuwalipa au kutokuwalipa kwani hata yeye hizo pesa hazitokani na kuuza Mifugo ya Familia yao bali zinatokana na Kodi tunazotozwa watanzania wote waliomchagua na wasiomchagua Magufuli!! Na wala hizo Posho hazitokani na fedha zilizopatikana kwa kuuza kadi za CCM hivyo wabunge toka vyama vingine wakose sifa za kupewa!!

Kutokwenda kwenye sherehe za kuapishwa kwa Magufuli hakuko Kikatiba bali hizo posho zinatokana na sheria zilizotungwa kwa kufuatisha Katiba iliyopo inayoshabikiwa na CCM hata kama ni Hovyo kabisa!! Kuna ujinga miongoni mwetu kuona kama serikali inafanya mambo kwa hisani jambo ambalo si sahihi.

Huitambui serikali halafu serikali hiyohiyo inakupa posho unaichukua then unasema sio hisani ila ni haki yako kwani ni pesa za wananchi,, swali sasa hiyo serikali imechaguliwa na nani?? Kama unaamini serikali ni haramu maana kila kitokanacho na hiyo serikali ni haramu tu!!!
Tuache unafiki
 
Last edited by a moderator:
Lakini wataapishwa kwa Jina la Magufuli (raisi wa JMTZ) ni lazima!

Hakuna kiapo cha utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Kubali usahihishwe. Askari tu ndio huapa utii kwa Rais na viongozi wengine wanaoongoza Taifa. Wabunge wanaapa kutii Katiba ya Jamhuri ya Muungano na kuilinda pia utumishi uliotukuka kwa kufuata Katiba pia.
 
ACT ni vibaraka wa CCM, Nashangaa ni vipi wamekubali matokeo ya urais kirahirahisi kana kwamba hakukuwa na uchakachuaji wa matokeo. Mimi ninaamini kabisa kura za Anna Mgwira zilipelekwa kwa Magufuli. Hainingii akilini kuwa Anna alipata kura 98600 tu nchi nzima. Hawa waliwauzia kura zao CCM.
 
Wabunge wa ukawa wakiongozwa na Mbowe ambao mpaka sasa hivi wamesusia kumtambua Raisi wa JMTZ pmj na serikali yake wameshasaini posho ya kuhudhuria vikao Bungeni itakayolipwa na Serikali ya Rais Magufuli!

11220126_923246657750250_1362120904712811456_n.jpg

Kama magufuli anajiamini na yeye awasusie kuwapa hiyo posho.
 
Huyu Bar - Barosa anajua hata anachokitetea kweli!!?

Is he serious kweli, kwamba wabunge "huapa" (take an oath) kwa jina la "Rais Magufuli?"

Jamaa kashupaa shingo kweli kweli utadhani anajua kumbe ni zero brain!!
 
Mijitu kama wew ipo kwa ajil ya kutafutia watu ban! Unalazimisha kukitetea hakiko popote pale dunian
Pengine utakuwa hujanielewa nilichokuwa namaanisha ! Kuna kitu kinaitwa State and the head of state is the President ambaye UKAWA hawamtambui, Sate ni muunganiko wa serikali, bunge na mahakama though kila moja ina majukumu na madaraka tofauti, narudi tena kwenye swali, kama ukawa hawamtambui head of the state kwanini washiriki shughuli za bunge ambalo ni sehemu ya muhimili wa nchi?
 
Kuna wakati CHADEMA iliwahi kuwa na kila aina ya watu, wakiwemo wajinga, wanafiki, wambea, mamlaki na wengine wengi wa namna yake. Tushukuru tu kuwa ilipatikana nafasi ya kuwaondoa hawa wote, akiwemo Mchange, mtu ambaye hajui kuwa Rais hana pesa, na kuwa pesa ni yetu sisi wananchi maana ndiyo tunaolipa kodi.

Nawashauri UKAWA, wasisusie pesa ya aina yoyote ile inayolipwa na ofisi za serikali au Bunge, waichukue, wairudishe kwa wananchi kwa kuendeleza ukombozi.
 
Wewe inaonekana hujawahi kusikiliza kiapo cha mbunge hata mara moja, na kama umewahi kusikiliza basi unasikia lakini huelewi.

Hakuna anayeapa kwa jina la Rais. Wabunge ni muhimu kuhudhuria vikao vyote vya Bunge. Na ufahamu kuwa Rais ndiye anayeenda kwenye kikao cha Bunge kuhutubia, siyo wabunge wanaenda kwenye mkutano wa Rais.

Pia utambue kuwa UKAWA hawajasema kuwa hawamtambui Rais bali wametamka kuwa hawakubaliani na mchakato wa kumpata Rais ulivyochafuliwa. Ili mtu awe Rais, matakwa ya katiba yetu ni kutangazwa mshindi na Tume, wala siyo lazima uwe umeshinda uchaguzi.

Lakini hauoni kama kuna unafiki hapo? Kwamba ukawa hawamtambui Raisi wa JMTZ lkn wanasaini kwenda Bungeni kushiriki ufunguzi wa Bunge utakaofanywa na Raisi wa JMTZ ambaye hawamtambui na kuapa kwa jina lake Raisi wa JMTZ, sasa kama siyo kuchanganyikiwa ni nini?
 
Kama hujui, inatupasa kukufundisha.

Wabunge wanaapa kuwa watiifu kwa Jamhuri siyo kwa Rais wala siyo kwa Serikali.

Kuwa mtiifu kwa Jamhuri maana yake nini? Ni nani Mkuu wa Jamhuri? Unawezaje kuwa mtiifu kwa Jamhuri bila ya kuwa mtiifu kwa Mkuu wa Jamhuri?
 
Mnataka wasusie ili mkapitishe mavitu yenu ndiyooooo na kugonga meza pwa pwa pwa kama konda anayeliadhibu DCM? Hasusi mtu!
 
huyu mchange kama sio shoga ntashnagaa sana
 
Cjawahi ona watu wenye upeo wa kufikili kama ukawa... ila watanyooka tu... na wakileta zao zile za kugoma watakutana na burn miezi 4,
 
Ni huyuhuyu Mchange ambaye ZZK aliimk alimkanya kwa ulopokaji wake pale Mbagala Zakim katika uzinduzivi wa kampeni. Toka ametimuliwa CDM anafikiri kwa hisia za kutamani Chadema ife
 
Barbarosa hiyo Posho hawalipwi kama hisani bali ni stahili yao inayotokana na wao kuchaguliwa na wananchi, pia Magufuli hana hiyari ya kuwalipa au kutokuwalipa kwani hata yeye hizo pesa hazitokani na kuuza Mifugo ya Familia yao bali zinatokana na Kodi tunazotozwa watanzania wote waliomchagua na wasiomchagua Magufuli!! Na wala hizo Posho hazitokani na fedha zilizopatikana kwa kuuza kadi za CCM hivyo wabunge toka vyama vingine wakose sifa za kupewa!!

Kutokwenda kwenye sherehe za kuapishwa kwa Magufuli hakuko Kikatiba bali hizo posho zinatokana na sheria zilizotungwa kwa kufuatisha Katiba iliyopo inayoshabikiwa na CCM hata kama ni Hovyo kabisa!! Kuna ujinga miongoni mwetu kuona kama serikali inafanya mambo kwa hisani jambo ambalo si sahihi.

umenene ndugu kuna watu wakijengewa barabara au kuletewa bomba la maji bado wanaona hisani huku wanalipa kodi
 
Last edited by a moderator:
Nashauri wachukue bila kuacha hata cent ni haki yao kazi wanayoifanya ni nzito bila wao life could be tough enough.
 
Back
Top Bottom