Wabunge wa UKAWA wameshasaini Bungeni!

Wabunge wa UKAWA wameshasaini Bungeni!

Lakini Wabunge wote wataapishwa kwa Jina la Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa TanZania ambaye wao ukawa hawamtabui, sasa hapo itakuwaje?

haa haa tangu lini wabunge wakaapa kwa jina la rais? pole sana mkuu...
 
huyu kijana anayejiita mchange hana kitu kichwani ni sifuri. hata hajielewi...hongereni wana kibaha kwa kumpiga chini....
 
Wewe naona huwa unasikia lakini huelewi. Hivi ulisikia UKAWA wakati wanasema kuwa hawakubaliani na mchakato wa kumpata Rais?

Nakukumbusha kama ulisikia lakini hukuelewa. UKAWA wanajua kuwa matokeo ya upigaji kura za Urais, Ubunge na Udiwani yamechezewa (Hawajasema kuwa matokeo ya kura za ubunge na udiwani yapo sawa). Lakini kwa ubunge na udiwani kuna nafasi ya kwenda kupinga mahakamani, na itafanyika hivyo. Udikteta wa Katiba upo kwenye matokeo ya kura za Urais ambako Tume ikishatangaza mshindi, hairuhusiwi kuhoji katika chombo chochote cha haki.

Kama hata maelezo haya bado hujaelewa, basi hutaelewa kamwe, labda utakuja kuelewa baada ya kuombewa.

Ninyi ni watu wa ajabu sana na mambo mnayoyafanya ni ya kipekee Dunia hii na ndio maana hakuna hata mtu yoyote Dunia anawasikliza kwenye malalamiko yenu kwa maana hamna akili kabisa!

Hivi unawezaje kumueleza Mtu wa nje kwamba hamumkubali Raisi wa nchi kwa kuwa unaamini kwamba Tume iliyopewa mamlaka ya kusimamia Uchaguzi imeiba kura lkn unakubali matokeo ya Ubunge ambayo yanasimamiwa na Tume hiyo hiyo ambayo unasema imeiba kura za Raisi, hivi unawezaje kujenga hoja kama hii na mtu akakuelewa?

Kama unasema Uchaguzi wa Uraisi haukuwa wa haki kwa kuwa kura ziliibiwa na Tume ya Uchaguzi ina maana Uchaguzi wote unapaswa kuwa batili na haupaswi kuchagua matokeo pale uliposhinda unasema ulikuwa wa haki na pale uliposhindwa unasema umeibiwa, Dunia haiendi hivyo, wenzenu huwa wanagomea kila kitu kwa 100% kwa maana Tume ni ile ile, kwa akili kama hizi madaraka TanZania mtasahau na hakuna mtu anayeweza kuwasadia nje ya TanZania kwa maana hata wazungu mkiwaelezea hivi watawaona wa ajabu na hamna akili!
 
Hivi kwa uelewa wako unadhani Rais ni Mkuu wa Jamhuri? Rais ni mkuu wa serikali, ni mkuu wa nchi lakini siyo mkuu wa Jamhuri. Unatakiwa kusoma tena Civics ili uelewe tofauti ya nchi (State) na Jamhuri (Republic).

Mkuu wa Jamhuri ni Wananchi. Mamlaka zote, pamoja na Taasisi ya Urais zinatakiwa kuitii Jamhuri. Mamlaka na uwezo wa Jamhuri huelezwa kwenye Katiba. Na Rais asipoitii Jamhuri, katiba inaeleza namna ya kumuondoa. Mamlaka zote huwekwa na kuondolewa lakini Jamhuri haiwekwi na haiondolewi. Rais wakati wa kiapo anasema atatii na kuilinda katiba (Katiba siyo mali ya chama, siyo mali ya serikali, siyo mali ya mahakama, siyo mali ya Bunge, siyo mali ya Rais, bali ni mali ya Jamhuri).

Kuwa mtiifu kwa Jamhuri maana yake nini? Ni nani Mkuu wa Jamhuri? Unawezaje kuwa mtiifu kwa Jamhuri bila ya kuwa mtiifu kwa Mkuu wa Jamhuri?
 
Wewe naona huwa unasikia lakini huelewi. Hivi ulisikia UKAWA wakati wanasema kuwa hawakubaliani na mchakato wa kumpata Rais?

Nakukumbusha kama ulisikia lakini hukuelewa. UKAWA wanajua kuwa matokeo ya upigaji kura za Urais, Ubunge na Udiwani yamechezewa (Hawajasema kuwa matokeo ya kura za ubunge na udiwani yapo sawa). Lakini kwa ubunge na udiwani kuna nafasi ya kwenda kupinga mahakamani, na itafanyika hivyo. Udikteta wa Katiba upo kwenye matokeo ya kura za Urais ambako Tume ikishatangaza mshindi, hairuhusiwi kuhoji katika chombo chochote cha haki.

Kama hata maelezo haya bado hujaelewa, basi hutaelewa kamwe, labda utakuja kuelewa baada ya kuombewa.

Kwa nini hata wafike huko kwenye kwenda kupinga Mahakamani? Kama uchaguzi umeibiwa maana yake ni kwamba uchaguzi wote bila ya kuchagua ni Batili, ni rahisi kihivyo tu!

Na je huko Mahakamani wanatumia kigezo kipi cha kwenda kupinga? Je, wanafungua kesi dhidi ya Wabunge wote au baadhi tu, na hizo baadhi ni zipi? ni zile tu walizoshindwa au hata walizoshinda?

Tatizo la vyama vya upinzani Tanzania ni vyama vya mfukoni. Hakuna misingi mizuri ya kuvijenga vyama, angalia Chadema ni tamaa ndio wameweka mbele hakuna demokrasi jinsi wanavyochagua viongozi wao. (Tumeona jinsi walivyolikumbatia Jambazi Sugu kwa sababu ya pesa) Bunge lililopita wabunge wa vyama (wa kujichagulia) wengi walikuwepo kwa sababu ya undugu au urafiki sio uwezo wao wa kufanya kazi za kibunge yaani kuwapigania walipa kodi wa sehemu zao na kukidhi shida zao. Je, ni wabunge wangapi wana utaratibu wa kuongea na waliowachagua na kusikilza shida zao kila wiki? Kwa kiingereza wanaita surgeries in their constituency. Hata CCM sidhani kama wanafanya hivyo. Kwa upinzani Tanzania wakitaka washinde jambo la kwanza ni kuweza kuwa na wabunge wengi Bungeni hiyo ndio iwe priority then wanaweza kuanza kufikiria kuongoza nchi.

Chadema imewakatisha tamaa wengi mimi nikiwa moja wapo, Mbowe ana tamaa ya pesa sio mabadiliko ya kuwasaidia Watanzania kuondokana na matatizo yao bali ni yeye tu, ni mbinafsi wa hali ya juu. Chadema walikuwa pazuri lakini huyu tamaa yake imeua chama. Sidhani kama wataweza tena kuwa na mvuto hasa ukitilia maanani kwamba Magufuli na CCM wameshituka na wamejipanga upya na wengi watashangaa na mabadiliko yanayokuja kutoka kwenye chama tawala.
 
Lakini hauoni kama kuna unafiki hapo? Kwamba ukawa hawamtambui Raisi wa JMTZ lkn wanasaini kwenda Bungeni kushiriki ufunguzi wa Bunge utakaofanywa na Raisi wa JMTZ ambaye hawamtambui na kuapa kwa jina lake Raisi wa JMTZ, sasa kama siyo kuchanganyikiwa ni nini?

Wewe kweli kilaza I see!! Wabunge wanaapa kwa Katiba ya nchi sio jina la Rais!! Wenye kuapa Kwa Kuilinda katiba na kuwajibika kwa Rais tena sio kwa kutaja jina la huyo Rais ni wale aliowateua wewe vipii?
 
mchange kura 3000 ni haki yake...akaungane na Mwapumba tu au Kisanduku plus Chakulagani

Mchange baada ya kukimbia shule na kubaki kuwa kasuku wa Zitto, ubongo wake umekuwa kama wa kuku. Hamwoni mwenzake mcubic alivyotulia? Uzuri wa Cubic anaelewa kwamba yeye sio Mkigoma hivyo Zitto alimuingiza cha kike ili NGO yake ionekane ya kitaifa. Maskini ya Mungu swaiba wangu mcubic njaa ikamzidi uzito akaona abalansishe hivyo hivyo kwa kumshabikia zitto . Hongera mcubic kwa kujitambua. Usifuate akili za mende za Mchange
 
Last edited by a moderator:
Ni lazima kama Wabunge wa Ukawa wataapa kwa Jina la Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa TanZania ambaye kwa bahati mbaya hawamtambui sasa hapo inakuwaje tena?

Na isitoshe ili wao walipwe posho ni lazima Serikali iliyo chini ya Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania iliridhie na kukubali kuwalipa sasa kama wao hawaitambui Serikali yake ina maana kwa akili ya kawaida hana mamlaka (Raisi na Serikali yake) ya kuidhinisha fedha ya Umma kwa maana kwa kujibu wa ukawa yeye siyo Raisi hahali!

Wabunge wanaapa kwa Jina la Mwenyezi Mungu tena wakiahidi kuilinda Katiba na sio kwa Jina la Rais wala Cheo cha Rais wewe utakuwa umepatwa na msongoooooooo!!!!
 
Mchange siku ya kuanza kampeni zao wasaliti alimporomoshea matusi lowassa yuko wapi? Mlisema baada ya uchaguzi huu kupita na chadema ikishindwa uchaguzi itasambaratika na act ndo kitakuwa chama kikuu cha upinzani. Yako wapi? Malofa sana nyie
 
Barbarosa hiyo Posho hawalipwi kama hisani bali ni stahili yao inayotokana na wao kuchaguliwa na wananchi, pia Magufuli hana hiyari ya kuwalipa au kutokuwalipa kwani hata yeye hizo pesa hazitokani na kuuza Mifugo ya Familia yao bali zinatokana na Kodi tunazotozwa watanzania wote waliomchagua na wasiomchagua Magufuli!! Na wala hizo Posho hazitokani na fedha zilizopatikana kwa kuuza kadi za CCM hivyo wabunge toka vyama vingine wakose sifa za kupewa!!

Kutokwenda kwenye sherehe za kuapishwa kwa Magufuli hakuko Kikatiba bali hizo posho zinatokana na sheria zilizotungwa kwa kufuatisha Katiba iliyopo inayoshabikiwa na CCM hata kama ni Hovyo kabisa!! Kuna ujinga miongoni mwetu kuona kama serikali inafanya mambo kwa hisani jambo ambalo si sahihi.

Well said bro, usiongeze neno utaharibu.
 
Last edited by a moderator:
Lakini hauoni kama kuna unafiki hapo? Kwamba ukawa hawamtambui Raisi wa JMTZ lkn wanasaini kwenda Bungeni kushiriki ufunguzi wa Bunge utakaofanywa na Raisi wa JMTZ ambaye hawamtambui na kuapa kwa jina lake Raisi wa JMTZ, sasa kama siyo kuchanganyikiwa ni nini?

Kiapo cha Wabunge kwa jina LA raisi? Labda kianze mwaka huu. Pole lakini ndio kujifunza.
 
Ni lazima kama Wabunge wa Ukawa wataapa kwa Jina la Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa TanZania ambaye kwa bahati mbaya hawamtambui sasa hapo inakuwaje tena?

Na isitoshe ili wao walipwe posho ni lazima Serikali iliyo chini ya Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania iliridhie na kukubali kuwalipa sasa kama wao hawaitambui Serikali yake ina maana kwa akili ya kawaida hana mamlaka (Raisi na Serikali yake) ya kuidhinisha fedha ya Umma kwa maana kwa kujibu wa ukawa yeye siyo Raisi hahali!

Usipige kelele jenga hoja kwa misingi ya katiba na sheria. Kama hayo unayopenda yamo. Pole hayamo
 
Is just matter of time mwenye chama Mbowe akishamtambua wote hawa wenye kejeli humu nao watafuatia maana akili zao bado zimefunikwa na ukungu wa zidumu fikra za mwenyekiti wa chama.
 
Back
Top Bottom