Wabunge wa CHADEMA waliohudhuria Bungeni, watakiwa kujiuzulu nafasi za uongozi Bungeni

Wewe ndio unajidanganya.

Waulize Selasini na Komu ambao wamehamia NCCR Mageuzi kinachowabakiza bungeni ni nini?
Watanzania kweli hatufuatilii mambo kwa umakini, Komu na Selasini wamebaki kuwa wabunge kwa sababu Chadema imejali maslahi mapana ya wananchi wa majimbo hayo! Ndo maana hawajawafukuza ili wabaki kuwahudumia wananchi lakini si kwa sababu ya Katiba.
Katiba inasema mbunge akishafukuzwa uanachama anakoma kuwa mbunge. Unakumbuka Zitto Kabwe, alibakiza mwaka mmoja lakini alikoma kuwa mbunge kwa sababu alikosa mwamvuli wa kumuweka bungeni.
 
Wabunge wa Chadema kwa kauli moja wamependekeza kwamba Wabunge wasaliti walioamua kuhudhuria bunge la corona na kupuuza msimamo wa chama chao wa kujitenga na bunge hilo kwa wiki mbili kama mwongozo wa WHO unavyoelekeza ili kuzuia maambukizi ya Virus hatari vya corona , wametakiwa kuachia nafasi zao za uongozi ndani ya chama ukiwemo ujumbe wa kamati kuu

Kauli hiyo imetolewa na Mnadhimu wa Kambi rasmi bungeni Mh Ester Bulaya , amesema kwamba ni aibu kwa kiongozi anayeshiriki vikao vya maamuzi vya chama kwa nafasi yake ya uongozi halafu baada ya muda mfupi anapuuza mambo aliyoshiriki kuyaamua .

Ikumbukwe kwamba Chadema haihangaiki na Ubunge wa mtu yeyote , bali wasaliti wanatakiwa kuachia nafasi za uongozi ndani ya chama , ndio maana mpaka sasa Anthony Komu na Joseph Selasini bado ni wabunge .

Mnadhimu wa Kambi rasmi bungeni Mh Ester Bulaya ameandika hivi kwenye mtandao wa Twitter.

=====

UPDATES:

DAVID Silinde, Mbunge wa Momba, Songwe kupitia Chadema ametangaza kujizulu nafasi ya katibu wa wabunge wa chama hicho kuanzia jana Jumatatu tarehe 4 Mei 2020

Silinde ambaye amekuwa mbunge kwa miaka kumi mfululizo amesema amechukua hatua hiyo ya kujiuzulu na tayari barua yake ya imemfikia Freema Mbowe.

Amesema, licha ya barua hiyo kumpelekea Mbowe, pia nakala yake ameipeleka kwa John Mnyika, Katibu Mkuu wa chama hicho.

“Nilijiuzulu jana nafasi ya Katibu wa Wabunge wa Chadema, kwa sababu nimeshindwa kusimamia maagizo ya chama ya kutohudhuria bungeni,” amesema Silinde. Hata hivyo, Silinde hajaweka wazi kama atakihama chama hicho au la.

Wabunge wengine walioingia bungeni jana ni; Joseph Selasini (Rombo), Anthony Komu (Moshi Vijijini), Peter Lijualikali (Kilombero), Jafary Michael (Moshi Mjini) na wabunge viti maalumu, Ratifa Chande, Mariam Msabaha na Sabrina Sungura.

Baada ya Silinde kuchukua uamuzi huo, wabunge wa Chadema wamemtaka Mariam Sabaha kujiuzulu nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, kufuatia hatua yake ya kukiuka maagizo ya chama.

=======

NYONGEZA :

David Silinde hakutia nia kugombea ubunge kwenye jimbo lake la Momba kama Chadema ilivyowataka wagombea wanaotaka kugombea ubunge na udiwani kupitia chama hicho , bali ametia nia kugombea Jimbo la Tunduma ambalo linaongozwa na Mh Mwakajoka .
October sio mbali Mungu akitulinda.
 
Attachments

  • VITA-KALI-ASKOFU-GWAJIMA-NA-CHADEMA-WAKOSE-UBUNGE-WOTE-DARMPYA-TV_7wqVVvPG2KQ.mp3
    10.1 MB · Views: 1
Chadema inauawa na Mbowe mwenyewe we fikiria Think tank wanaondoka hujirekebishi unawatukana Viongozi wakubwa wanaondoka uanawatukana unasema wamenunuliwa

Kila kinachofanywa na Serikali unapinga unatukana unabeza hiyo ni akili au akili hewa

Badala ya kusaidiana na Serikali kwenye mambo yako wazi na kila mwananchi anaona wewe uko bize kupinga kutukana na kubeza

Badala kuonesha uzalendo kwa nchi yako dhidi ya Mataifa mengine ndo Kwanza unachongea nchi yako kwa Mataifa makubwa unachafua na kutukana

Katika mazingira haya lazima upigwe laana ya hatari
 
Wewe
Watanzania kweli hatufuatilii mambo kwa umakini, Komu na Selasini wamebaki kuwa wabunge kwa sababu Chadema imejali maslahi mapana ya wananchi wa majimbo hayo! Ndo maana hawajawafukuza ili wabaki kuwahudumia wananchi lakini si kwa sababu ya Katiba.
Katiba inasema mbunge akishafukuzwa uanachama anakoma kuwa mbunge. Unakumbuka Zitto Kabwe, alibakiza mwaka mmoja lakini alikoma kuwa mbunge kwa sababu alikosa mwamvuli wa kumuweka bungeni.
Wewe muongo huwezi kumfukuza mbunge lazima ataweka pingamizi kotini
 
Chadema inauawa na Mbowe mwenyewe we fikiria Think tank wanaondoka hujirekebishi unawatukana Viongozi wakubwa wanaondoka uanawatukana unasema wamenunuliwa

Kila kinachofanywa na Serikali unapinga unatukana unabeza hiyo ni akili au akili hewa

Badala ya kusaidiana na Serikali kwenye mambo yako wazi na kila mwananchi anaona wewe uko bize kupinga kutukana na kubeza

Badala kuonesha uzalendo kwa nchi yako dhidi ya Mataifa mengine ndo Kwanza unachongea nchi yako kwa Mataifa makubwa unachafua na kutukana

Katika mazingira haya lazima upigwe laana ya hatari
Adui Wa adui yako Ni adui yako, kiujumla wapinzani Wa mbowe wanashangilia.Ila hawa wabunge Ni wasaliti
 
Zitto kwani naye alifanywa nini? Dk Kitila nae alifanywa nini?

Liondoe kwanza boriti la jicho lako kisha ulisafishe jicho la mwenzio.

Unahubiri demokrasia kila siku lakini ndani ya chama chako hureflect unacho kuhubiri.
Rudia kusoma comment yangu tens.
 
Chama lazima kiheshimiwe huwezi kujiendesha tuu utakavyo bila mashauliano na wenzako nooo hata hivyo nikitake chama kama kuna wenye kutaka kusamehewa wasamehewe kwani chadema ni family moja.
 
Hahhahahaha.... Kwanini wasiwafukuze?

Yani unakaa na nyoka ndani alafu unatoka nje unapiga kelele unasema nataka wewe nyoka utoke huko ndani ya nyumba yangu!

Hizi ni akili au matope? Au mnawaogopa?

Chadema ni mali ya Mbowe, Mdee, Lema na sasa Bulaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nyoka si hao wanatoka wenyewe mkuu.
Nyoka wengine kelele tu zinatosha. Purukushani ya kazi gani
 
NCCR wanapiga jaramba la kuwa chama kikuu cha upinzani! Chadema ndo bye bye..
 
Wabunge wa Chadema kwa kauli moja wamependekeza kwamba Wabunge wasaliti walioamua kuhudhuria bunge la corona na kupuuza msimamo wa chama chao wa kujitenga na bunge hilo kwa wiki mbili kama mwongozo wa WHO unavyoelekeza ili kuzuia maambukizi ya Virus hatari vya corona , wametakiwa kuachia nafasi zao za uongozi ndani ya chama ukiwemo ujumbe wa kamati kuu

Kauli hiyo imetolewa na Mnadhimu wa Kambi rasmi bungeni Mh Ester Bulaya , amesema kwamba ni aibu kwa kiongozi anayeshiriki vikao vya maamuzi vya chama kwa nafasi yake ya uongozi halafu baada ya muda mfupi anapuuza mambo aliyoshiriki kuyaamua .

Ikumbukwe kwamba Chadema haihangaiki na Ubunge wa mtu yeyote , bali wasaliti wanatakiwa kuachia nafasi za uongozi ndani ya chama , ndio maana mpaka sasa Anthony Komu na Joseph Selasini bado ni wabunge .

Mnadhimu wa Kambi rasmi bungeni Mh Ester Bulaya ameandika hivi kwenye mtandao wa Twitter.

=====

UPDATES:

DAVID Silinde, Mbunge wa Momba, Songwe kupitia Chadema ametangaza kujizulu nafasi ya katibu wa wabunge wa chama hicho kuanzia jana Jumatatu tarehe 4 Mei 2020

Silinde ambaye amekuwa mbunge kwa miaka kumi mfululizo amesema amechukua hatua hiyo ya kujiuzulu na tayari barua yake ya imemfikia Freema Mbowe.

Amesema, licha ya barua hiyo kumpelekea Mbowe, pia nakala yake ameipeleka kwa John Mnyika, Katibu Mkuu wa chama hicho.

“Nilijiuzulu jana nafasi ya Katibu wa Wabunge wa Chadema, kwa sababu nimeshindwa kusimamia maagizo ya chama ya kutohudhuria bungeni,” amesema Silinde. Hata hivyo, Silinde hajaweka wazi kama atakihama chama hicho au la.

Wabunge wengine walioingia bungeni jana ni; Joseph Selasini (Rombo), Anthony Komu (Moshi Vijijini), Peter Lijualikali (Kilombero), Jafary Michael (Moshi Mjini) na wabunge viti maalumu, Ratifa Chande, Mariam Msabaha na Sabrina Sungura.

Baada ya Silinde kuchukua uamuzi huo, wabunge wa Chadema wamemtaka Mariam Sabaha kujiuzulu nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, kufuatia hatua yake ya kukiuka maagizo ya chama.

=======

NYONGEZA :

David Silinde hakutia nia kugombea ubunge kwenye jimbo lake la Momba kama Chadema ilivyowataka wagombea wanaotaka kugombea ubunge na udiwani kupitia chama hicho , bali ametia nia kugombea Jimbo la Tunduma ambalo linaongozwa na Mh Mwakajoka .
Wakati mwingine unajiuliza, hivi hiki ni Chama cha Demokrasia au cha Domokrasi
 
Back
Top Bottom