Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,703
- 218,239
Wabunge wa Chadema kwa kauli moja wamependekeza kwamba Wabunge wasaliti walioamua kuhudhuria bunge la corona na kupuuza msimamo wa chama chao wa kujitenga na bunge hilo kwa wiki mbili kama mwongozo wa WHO unavyoelekeza ili kuzuia maambukizi ya Virus hatari vya corona , wametakiwa kuachia nafasi zao za uongozi ndani ya chama ukiwemo ujumbe wa kamati kuu
Kauli hiyo imetolewa na Mnadhimu wa Kambi rasmi bungeni Mh Ester Bulaya , amesema kwamba ni aibu kwa kiongozi anayeshiriki vikao vya maamuzi vya chama kwa nafasi yake ya uongozi halafu baada ya muda mfupi anapuuza mambo aliyoshiriki kuyaamua .
Ikumbukwe kwamba Chadema haihangaiki na Ubunge wa mtu yeyote , bali wasaliti wanatakiwa kuachia nafasi za uongozi ndani ya chama , ndio maana mpaka sasa Anthony Komu na Joseph Selasini bado ni wabunge .
Mnadhimu wa Kambi rasmi bungeni Mh Ester Bulaya ameandika hivi kwenye mtandao wa Twitter.
Wabunge wa Chadema wamemtaka David Silinde ajiuzulu Nafasi zake zote za Uongozi kwa kushindwa kusimamia makubaliano ya wabunge na Maelekezo ya Chama . Kama Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Naunga Mkono anapaswa kujiuzulu.
Wabunge wa Chadema pia Wamemtaka Mh Mariam Msabaha Ajiuzuru nafasi yake ya ujumbe wa Kamati Kuu kwa kushindwa kufuata makubaliano ya wabunge na Maelekezo ya Chama, Mariamu Msabaha alipata nafasi hiyo kwa kuchaguliwa na Wabunge . Mimi kama Mnadhimu Naunga mkono
=====
UPDATES:
DAVID Silinde, Mbunge wa Momba, Songwe kupitia Chadema ametangaza kujizulu nafasi ya katibu wa wabunge wa chama hicho kuanzia jana Jumatatu tarehe 4 Mei 2020
Silinde ambaye amekuwa mbunge kwa miaka kumi mfululizo amesema amechukua hatua hiyo ya kujiuzulu na tayari barua yake ya imemfikia Freema Mbowe.
Amesema, licha ya barua hiyo kumpelekea Mbowe, pia nakala yake ameipeleka kwa John Mnyika, Katibu Mkuu wa chama hicho.
“Nilijiuzulu jana nafasi ya Katibu wa Wabunge wa Chadema, kwa sababu nimeshindwa kusimamia maagizo ya chama ya kutohudhuria bungeni,” amesema Silinde. Hata hivyo, Silinde hajaweka wazi kama atakihama chama hicho au la.
Wabunge wengine walioingia bungeni jana ni; Joseph Selasini (Rombo), Anthony Komu (Moshi Vijijini), Peter Lijualikali (Kilombero), Jafary Michael (Moshi Mjini) na wabunge viti maalumu, Ratifa Chande, Mariam Msabaha na Sabrina Sungura.
Baada ya Silinde kuchukua uamuzi huo, wabunge wa Chadema wamemtaka Mariam Sabaha kujiuzulu nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, kufuatia hatua yake ya kukiuka maagizo ya chama.
=======
NYONGEZA :
David Silinde hakutia nia kugombea ubunge kwenye jimbo lake la Momba kama Chadema ilivyowataka wagombea wanaotaka kugombea ubunge na udiwani kupitia chama hicho , bali ametia nia kugombea Jimbo la Tunduma ambalo linaongozwa na Mh Mwakajoka .