Naamini malengo ya utekaji ni kupeleka ujumbe wa hofu zaidi ya kudhuru au kuua. Utawala huu naona unafanyia kazi dhana ya kuwa ukifanikiwa kuwajengea maadui wako hofu, tayari una nusu ya ushindi. Mfano maandamano ya UKUTA yalizimwa kwa mazoezi yaloyolenga kujenga hofu. Kauli mbalimbali za watawala mfano kuvitishia vyombo vya habari, kamata kamata ya wapinzani na kesi zisizoisha zina nia ya kujenga hofu nk.
Dalili ya mtawala aliye na hofu na asiyejiamini ni kutishia na kufanya na kuamuru matendo yanayolenga kuleta hofu kwa anaowaongoza. Mtu jasiri anatakiwa awe huru kupambana na hofu kama Tundu Lissu. Kama ni kutekwa na kukamatwa huwa namwona Tundu Lissu akikamatwa kila siku. Ila bado sijaona mwanachama wa chama cha kijani akilala sero hata lisaa limoja tu la mfano.
Huyu Bashe bado anaamini kuwa akivaa kijani basi yeye ni nusu mungu au "untouchable" hagusiki!!. Ni wakati sasa ajifunze na aachane na huo mtazamo. Anatakiwa kwanza kutambua kuwa binadamu wote ni sawa. Watanzania wote ni sawa, wana thamani iliyo sawa. Haijalishi kama anaunga mkono upinzani au ccm.
Kama ni mkweli, Hussen Bashe tungemwona anapinga matendo yote machafu ya utawala kuanzia mwanzo. Sio mpaka achukuiwe kwa mahojiano masaa machache, ndio aanze kupiga kelele kama mtoto aliyezaliwa jana.
G