Wabunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Pinda?

Ole wao ambao majina yao hayaonekani hapa,kwa wale ambao hawatatia mkono hapa wajue wapiga kura wao watawahukumu kwa usaliti wao,wajiandae kuanza maisha mapya ya uraiani,CDM hongereni kwa kazi nzuri mnayofanya tumeona
 
ila sas tumepigwa chini eti siku hazitatufikisha, sasa sijui itakuwaje? lakini nafikir tusubir hadi bunge la bajeti siku ya kwanza iwasilishwe na hapo sasa sijui hayya majina ya leo yataweza kutumika au watatafuta wengine . this is tanzania
 
Du hii ndo CCM, jana walikuwa wanaongea vile leo kwenye saini wamekula kona, MIMI Nazani haya majina yawekwe wazi watanzania wote wajue walio sini hapa hamuna siri,
 
Kura nne zilizobaki ningependa nitakaowataja watie sahihi zao, kwani huwa wanaongea bungeni kwa hisia sana.

1. Anne Kilango Malecela- "Mheshimiwa waziri Mkuu naomba majibu ya uhakika...."
2.John Pombe Magufuli -
 
Anne K Malecela
John Pombe Magufuli
Livingstone Lusinde
Mary Nagu

Hawa ni viongozi muhimu sana kujazia kura
 
Nadhani kweli habari ... kwani mmoja mafisadi waliokodisha ndege hiyo baada ya kulipwa chake, amekuwa anatumbua kishenzi mjini hapa na amefungua chuo cha muziki anakiita "Wallis" kwa shukrani..... tutafika kweli!.
 
MNYISANZU kwan Mbunge wako hayupo mjengoni?
Mkuu, mbunge wangu yuko mjengoni ila ni gamba gumu mwanzo mwisho, ni mtu wa aina ya " zidumu fikra za mwenyekiti"!. Ni mtu wa kujali maslahi binafsi na ku-preserve status quo. Hivyo basi sina matumaini hata kidogo ya yeye kushiriki ktk hii mission ya kumng'oa PM na mawaziri wengine viwavi.
 
hon myika amesema waliokwisha sain wameshafikia 67 pls still tunaomba tuwafahamu wenye nia njema na taifa letu
 
Ingawa siku zote nasisitiza zaidi mabadiliko ya kitaasisi na kisera, naweza pia kuona umuhimu wa kwaondoa viongozi wasioheshimu utawala wa sheria, misingi ya taasisi na wasiofuata sera zilizopo.

Jamii inayotaka kuendelea haina budi kuwa na kuutumia mchakato wa kuwakataa viongozi wabovu.

Hakuna maana ya bunge kuwa na haki ya kumwondoa waziri mkuu kwa kura ya kukosa imani naye, halafu waziri mkuu anapoharibu moja kwa moja au kwa kushindwa kuwajibisha wengine, aachiwe tu.

Na bado, mpaka iwe kama Japan, waziri mkuu abadilishwe kila miezi 18 kama hatii adabu. Tutaona wenyewe adabu inapanda.
 
WanaJF habari za asubuhi.
Wakuu mimi ninamtazamo tofauti kidogo kuhusu kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu. Ni kweli kuwa bunge linauwezo wa kupiga kura kwa pm lakini pia wanauwezo wa kupiga vote of no confidence hata kwa president.
Sasa wasiwasi wangu hivi hata waziri mkuu akijiuzulu hivi kutakuwa na mabadiliko ya kiutendaji kama Rais atabaki huyuhuyu?
Mimi sioni kama kutakuwa na mabadiliko kama tutabaki na mkwe.re akiwa president. Mimi nionavyo chanzo cha utendaji mbovu wa serikali ni rais mwenyewe hata pm nguvu yake inategemea sana mkuu wa kaya yupoje. Coz siyo pm anatoa msimamo fulani afu anaambiwa kwa nini umefanya hivyo. Kwani rais hajui ubadhirifu unaofanywa na mawaziri wake aaa wapi anajua na yeye mwenyewe anashiriki. Ubadhirifu uliopo nchini sasa mtandao ambao unaanzia ikulu hadi wilayani.
Hivyo mimi ningekuwa Zito nivema kupiga ya kutokuwa na imani na Rais kuliko kumpigia PM ili tufanye mabadiliko ya rais kabisa kwa kufanya uchaguzi upya.
Huu ni mtazamo wangu nipo tayari kurekebishwa.
 
Mkuu umesema yaliyokweli kabisa,kwasababu ukitaka kuung'oa mti lazima uanzie kwenye mzizimkuu otherwise utaakuwa unaproon matawi ambapo bado mti huo utachipua tena. Ila mimi nachokiona hapa nikwamba watanzania hatuna uthubutu, we are never daring to take risk and thus why we are at risk!
 
ni kweli mkuu, ila jamaa anazunguka duniani kulisha virus alionao basi coz virus vinahitaji vitu vinono ndo maana hata hajali yanayotokea.
Mke wangu hapa ananiambia miaka ingekuwa inaendeshwa kwa remote tungeforwad ili Jk aondoke madarakani.
 
Mkakati wa kukusanya majina 70 ya wabunge kama sehemu ya kukamilisha utaratibu wa kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, umepamba moto na hadi kufikia jana jioni, wabunge 75 walikuwa wameunga mkono hatua hiyo, watano kati yao, wakitokea chama tawala CCM. Endapo mchakato huo utakamilika, Pinda atakuwa ameingia katika historia ya kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupigiwa kura ya kutokuwa na imani na Bunge

Soma taarifa yote hapa
 
Back
Top Bottom