Wabunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Pinda?

Kwa mujibu ya taarifa ya habari ya saa saba leo mchana TBC waziri mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kuchukua maamuzi magumu baada ya wabunge wengi kuonyesha kutokuwa na IMANI naye!

Hatua hii inafikiwa baada ya kikao cha wabunge wa CCM kilichokuwa chini ya MH MSEKWA kujadilli kwa kina hili swala na wabunge wengi wa ccm kutaka mzee pinda kuachia ngazi ili kurejesha imani kwa wananchi!

Sambamba na hilo wapo mawaziri watano waliothibitika kuandika barua ya kuachia ngazi kufuatia wizara zao kugundulika na uozo kibao
 
huo uamuzi atautangaza saa ngapi?
mbona hizi habari zinachangany?
mara wamejiuzulu, mara hawajajiuzulu..
Hebu tujuzane Wajameni
 
Duh mbona raha wadau! aachie ngazi tu mtoto wa mkulima FISADI

Tueleze amefisadi nini? au mnataka avunje katiba kwa kuwawajibisha mawaziri ambao hana mamlaka nao?. Yes its the time 4 him to step down and there is something beyond his constitutional authority ambacho kimepelekea haya yote. Lakini ufisadi wa Pinda kama Pinda ni upi jamani
 
acha uzushi mkuu. Unaaibisha JF kwani tupo makini toka asbh tunafuatilia bunge na toka liishe hakuna taarifa ya habari iliyosomwa. So, sii kweli kua Pinda ataongea baadaye TBC kwani hakuna kilichotangazwa hadi sasa. Don't waste time of others for childish jokes like this again!
 
Maamuzi magumu ya mawaziri wetu ni kunga`ngana madarakani.
Kukataa kujiuzuru na hawafanywi chochote!
 
acha uzushi mkuu. Unaaibisha JF kwani tupo makini toka asbh tunafuatilia bunge na toka liishe hakuna taarifa ya habari iliyosomwa. So, sii kweli kua Pinda ataongea baadaye TBC kwani hakuna kilichotangazwa hadi sasa. Don't waste time of others for childish jokes like this again!

W e paulo hii avatar si ya ndallo?
 
Mbona wote wakigoma kujiuzulu ndiyo dili?
Siwaelewi sana wanaofurahia hili suala la Mwenye Sura Ngumu kuachia ngazi wanatoka upande gani.

Anyway, basi kuwajibika kwa serikali iendane na kushuka kwa bei za bidhaa muhimu kwa matumizi ya binadamu, bidhaa ambazo zilipanda bei kiholela kutokana uzembe wa baadhi ya viongozi wa serikali.

Vinginevyo kuwajibika kwao kutakuwa hakuna maana kama hakutakuwa na unafuu wa maisha kwa watanzania, na bado Zitto na wenzake wataendelea kuzishika nyeti za Mkulu mpaka kieleweke!
 
pinda jaman mtu safi bado tunamhitaji ila hao mawzir wapumzike aletewe vifaa vipya achape kazi
 
Kuna raha gani hapo?
Lowassa alipoachia ngazi mambo yalibadilika?
Wabongo bana. Hata hamjui mnachokita.

Gamba lingine hili, maana yake ndio nini wakati unajua kabisa watu ambao hawapendi mabadiliko ni viongozi kutoka katika chama cha MAGAMBA!
 
Back
Top Bottom