Wabunge Festo Sanga na Subira Mgalu mbona mnahangaika kumtetea Waziri Makamba kauli ya Umeme Laki 8?

Mtumishiwetu

Senior Member
Jul 13, 2022
187
334
Siku ya leo mitandao yote ya kijamii inazunguka Clip ya Waziri wa Nishati, Januari Makamba ikisema kuanzia sasa gharama ya kuunganisha umeme iwe mjini iwe kijijini gharama ya kuletewa umeme ni laki 8.

Clip hiyo imetokana na sehemu ya mahojiano ya ITV katika Kipindi cha Dakika 45 Makamba akihojiwa na Mtangazaji Benjamin Mzinga, ambaye alizunguka naye kwenye ziara yake mikoa ya Kanda ya Ziwa ya kugawa mitungi ya gesi.

Kwanini wabunge hawa wamekuwa mbele kutetea clip hiyo ambayo haina upotoshaji kwani imemuonesha mzungumzaji mwenyewe?
 
Siku ya leo mitandao yote ya kijamii inazunguka Clip ya Waziri wa Nishati, Januari Makamba ikisema kuanzia sasa gharama ya kuunganisha umeme iwe mjini iwe kijijini gharama ya kuletewa umeme ni laki.

Clip hiyo imetokana na sehemu ya mahojiano ya ITV katika Kipindi cha Dakika 45 Makamba akihojiwa na Mtangazaji Benjamin Mzinga ambaye alizunguka naye kwenye ziara yake mikoa ya Kanda ya Ziwa ya kugawa mitungi ya gesi.

Kwanini wabunge hawa wamekuwa mbele kutetea clip hiyo ambayo haina upotoshaji kwani imemuonesha mzungumzaji mwenyewe
Wewe ndo hukumwelewa Makamba. Umefuata ushabiki ama kwa makusudi au kwa kutojua. Alichosema Makamba ni hivi " gharama ya kuingiza umeme ni laki 8 iwe mijini au vijijini, lakini kwa kijijini inakuwa elfu 27 maana tayari TANESCO/Serikali inatoa ruzuku ya kiasi kinachobaki". Hivyo, gharam halisi ni laki 8 na siyo 27. Sijui nimeeleweka!!!!
 
Kwahyo na mjin ni sh ngap..
 
Acha kuingia kwenye ujinga huu.

Kuweka Ile waya na Ile LUKU ndio laki nane?
 
Hao wanabwabwaja tu hata hawaelewi. Kesho waziri akisema laki nawao wamo. Akisema milioni na wao wamo.

Hawatumii hata common sense.
 
Acha kuingia kwenye ujinga huu.

Kuweka Ile waya na Ile LUKU ndio laki nane?
Siyo waya tu. hiyo bei haianzi leo. labda kama unaishi kwa baba na mama au kwa mjomba au umepanga. waliojenga na kuingiza umeme wamezoea.
 
Wewe ndo hukumwelewa Makamba. Umefuata ushabiki ama kwa makusudi au kwa kutojua. Alichosema Makamba ni hivi " gharama ya kuingiza umeme ni laki 8 iwe mijini au vijijini, lakini kwa kijijini inakuwa elfu 27 maana tayari TANESCO/Serikali inatoa ruzuku ya kiasi kinachobaki". Hivyo, gharam halisi ni laki 8 na siyo 27. Sijui nimeeleweka!!!!
Ushabiki na chuki ni maradhi mabaya sana
 
Wewe ndo hukumwelewa Makamba. Umefuata ushabiki ama kwa makusudi au kwa kutojua. Alichosema Makamba ni hivi " gharama ya kuingiza umeme ni laki 8 iwe mijini au vijijini, lakini kwa kijijini inakuwa elfu 27 maana tayari TANESCO/Serikali inatoa ruzuku ya kiasi kinachobaki". Hivyo, gharam halisi ni laki 8 na siyo 27. Sijui nimeeleweka!!!!
Yaan wewe ndio umenikoroga kabisa
 
Siku ya leo mitandao yote ya kijamii inazunguka Clip ya Waziri wa Nishati, Januari Makamba ikisema kuanzia sasa gharama ya kuunganisha umeme iwe mjini iwe kijijini gharama ya kuletewa umeme ni laki.

Clip hiyo imetokana na sehemu ya mahojiano ya ITV katika Kipindi cha Dakika 45 Makamba akihojiwa na Mtangazaji Benjamin Mzinga ambaye alizunguka naye kwenye ziara yake mikoa ya Kanda ya Ziwa ya kugawa mitungi ya gesi.

Kwanini wabunge hawa wamekuwa mbele kutetea clip hiyo ambayo haina upotoshaji kwani imemuonesha mzungumzaji mwenyewe
Sisi tulishasema ukimuweka kilaza mwenye Elimu ya kuungaunga kwenye wizara kama hii unategemea nn zaidi.Wizara hii inajiendea tu haina waziri.
 
Siyo waya tu. hiyo bei haianzi leo. labda kama unaishi kwa baba na mama au kwa mjomba au umepanga. waliojenga na kuingiza umeme wamezoea.
Mazoea ya uonevu tu.

Usikubali kupumbazwa na wasaka pesa za kampeni za Urais 2025.

Ukishaweka umeme Bei yenyewe ya unit Iko juu sana.
 
Acha kuingia kwenye ujinga huu.

Kuweka Ile waya na Ile LUKU ndio laki nane?
Kwanza wengi hawakumuelewa Makamba,
Hoja ya makamba alikua akieleza kwamba hata hizi bei za sasa ambazo watu wanalalamika kwamba ni kubwa bado serikali inaweka ruzuku.

Makamba ameeleza kwa makadirio tu kwamba gharama kwa wastani yakuunganisha umeme kama ukiutaka uhalisia inafika 800,000,hivyo hizi gharama za sasa ile ya 27000 kwa vijijini na hii ya mijini ambayo ni laki tatu na point nafikiri serikali inalazimika kuongeza ruzuku.

Makamba ameeleza mita moja ya waya ule unaotumika kuvuta umeme kutoka kwenye nguzo kuja kwenye nyumba inauzwa tsh 35,000/=.Sasa hemu fanya makadirio mfano nyumba yako ipo umbali 16m kutoka kwenye nguzo 35000×16=560000.Hizi ni gharama za waya kwa makadirio.

Na bei ya mita makamba amesema ni 250,000 hivyo ukijumlisha na 560,000 ya waya ndipo hapo alipokadiria gharama ya 800,000/=.

Kimsingi zipo nyumba zinaumbali hata wa 5m kutoka kwenye nguzo hivyo utaona gharama hazitafika 800,000/=.Alichotoa Makamba ni makadirio hakuna sababu yakuhukumiwa.

Chamsingi hapa wanaobisha wanapaswa waende madukani wakaulizie bei ya waya kwa kila useful wa mita moja pia waulize na bei ya mita waone kama makamba anadanganya ndipo mmuite mwongo kinyume cha hapo kaeni kimya.
 
Siyo waya tu. hiyo bei haianzi leo. labda kama unaishi kwa baba na mama au kwa mjomba au umepanga. waliojenga na kuingiza umeme wamezoea.
Mimi niliweka umeme na matumizi ya nguzo moja kwa 300k. Hiyo ya 800k imeanza lini
 
Kwanza wengi hawakumuelewa Makamba,
Hoja ya makamba alikua akieleza kwamba hata hizi bei za sasa ambazo watu wanalalamika kwamba ni kubwa bado serikali inaweka ruzuku.

Makamba ameeleza kwa makadirio tu kwamba gharama kwa wastani yakuunganisha umeme kama ukiutaka uhalisia inafika 800,000,hivyo hizi gharama za sasa ile ya 27000 kwa vijijini na hii ya mijini ambayo ni laki tatu na point nafikiri serikali inalazimika kuongeza ruzuku.

Makamba ameeleza mita moja ya waya ule unaotumika kuvuta umeme kutoka kwenye nguzo kuja kwenye nyumba inauzwa tsh 35,000/=.Sasa hemu fanya makadirio mfano nyumba yako ipo umbali 16m kutoka kwenye nguzo 35000×16=560000.Hizi ni gharama za waya kwa makadirio.

Na bei ya mita makamba amesema ni 250,000 hivyo ukijumlisha na 560,000 ya waya ndipo hapo alipokadiria gharama ya 800,000/=.

Kimsingi zipo nyumba zinaumbali hata wa 5m kutoka kwenye nguzo hivyo utaona gharama hazitafika 800,000/=.Alichotoa Makamba ni makadirio hakuna sababu yakuhukumiwa.

Chamsingi hapa wanaobisha wanapaswa waende madukani wakaulizie bei ya waya kwa kila useful wa mita moja pia waulize na bei ya mita waone kama makamba anadanganya ndipo mmuite mwongo kinyume cha hapo kaeni kimya.
Ndio maana nguzo zinabaki kuwa mali yao. Huyu anatafuta kutupiga hela tu.

Mbona barabara zinaletwa bule?

Isitoshe tunanunua umeme kwa bei ya juu, wanapata faidi nyingi. Kimsingi walitakiwa kutuleta bure afu tununue umeme.
 
Back
Top Bottom