Wabunge CHADEMA wamedanganyika?

Kwa hili hata mimi Dilunga sikuelewi,maana hata hao wabunge waliobaki bungeni katika michango yao wote ni kutufahamisha wananchi kuwa wako pale kupitisha muswada na si kutunga katiba kama wabunge CDM na wanaarakati wanavyo dai.Sisi wananchi kutoingia bungeni sikana kwamba hatuna akili tunaelewa vizuri kinachoendelea bungeni.CDM na wananchi wengine ambao si wa chama chochote cha siasa tunapinga huo muswada kuodhiwa na serikali.Bunge liliagiza kamati ya kudumu ya bunge kupita katika mikoa mbalimbali kupata maoni ya wananchi lakini spika aliikatalia tume kufanya hivyo kisa eti yeye yuko India kwahiyo hilo haliwezekani,kwahiyo maoni ya wananchi hayajachukuliwa.Kitu kikubwa na cha kutisha ni madaraka makubwa aliyopewa raisi katika kuteua kamati ya kuratibu mchakato wa kuchukua maoni.Sio siri viongozi wetu siku zote wamekuwa na mawazo ya enzi za "ZIDUMU FIKRA SAHIHI ZA MWENYEKITI WA CCM"Sasahivi huko tumeisha toka
 
Kwa hakika nilipitia kwa umakini makala ya Dilunga lakini nimeona analysis ambayo inaangalia upande mmoja tu wa shilingi! amedandia hoja ambayo haifahamu vizuri! sijui kwa dilunga tatizo la cdm kutoka nje ni nini! ni vema akatueleza kilichomkera yeye! suala ni muswada kusomwa kwa mara ya kwanza na si mara ya pili! Kijana unaonekana smart lakini ushabikli huu! au unatafuta uteuzi kutokwa kwa bwana mkubwa?
 
Naona kinachoendelea ni usanii wa kisiasa, hata hiyo 'WALK OUT' ya cdm inaonekana kama jambo lilipangwa mapema. Hapa upande utakaofaidika na mchezo huu ni wale watakaofanya propaganda ya kutosha; naona ccm wakisaidiwa na cuf wameanzia Bungeni, itajukua juhudi za ziada cdm wafanye hayo maandamano hadi wananchi wawe upande wao.
 
Baada ya kusoma makala hyo ya Dillunga, pia nikasoma makala ya Msomaji Raia (naomba mtu aiweke hapa) yenye jina "Twaweza kuwapuuza CHADEMA, hatuwezi kupuuza matokeo ya upuuzi wetu"
katika makala hyo ya Msomaji Raia naomba ninukuu kifungu kidogo hapa, anasema
"..... Mpaka hapa jambo moja ni wazi: kwamba tunaweza kuwapuuza CHADEMA na wanaharakati wa Jukwaa la katiba, tunaweza kuwazomea wabunge waliotoka nje kupinga na kugoma kushiriki katika mjadala bandia, lakini hatuwezi kupuuza matokeo ya upuuzi wetu huu. Tuna uhuru wa kuchagua njia ya kufikia kupata katiba mpya, lakini hatuna uhuru wa kuchagua madhara yatakayotokana na uchaguzi wetu mbaya....."
Naomba nisiongeze kitu tena,
Tupime wenyewe!
 
Godfrey Dilunga-Raia Mwema

NOVEMBA 14, mwaka huu, Serikali kupitia kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani, iliwasilisha Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba mpya.

Muswada ambao utakaoongoza wananchi kutoa maoni yao kuhusu Katiba mpya. Tukio hilo lilitanguliwa na kazi nyingine ya uwasilishaji, mjadala na uridhiaji wa Muswada wa Sheria ya Manunuzi ya Umma.

Katika taswira ya Bunge, hasa kwa mujibu wa kanuni zake, Muswada wa Sheria ya Manunuzi na Muswada wa Mabadiliko ya Katiba, yote ni miswada. Mbele ya kanuni za Bunge, ina nguvu sawa.

Majukumu ya mbunge na Bunge ni pamoja na kutunga sheria. Mpiga kura anayekwenda kituo cha upigaji kura kumchagua mbunge, anatambua moja ya kazi ya atakayemchagua ni kutunga sheria, kwa niaba yake.

Ni makosa kwa mbunge au kundi la wabunge kudhani au kujenga dhana kwamba muswada fulani si muhimu kwa kulinganisha na muswada mwingine.

Dhana hii ni potofu kwa sababu tafsiri inayoweza kujitokeza ni kwamba, wabunge wenye mtazamo huo ni kama wanawaaminisha Watanzania kuwa zipo sheria ambazo ni mbovu wameshiriki kuzitunga. Kwamba ipo miswada wameiridhia isiyo na umuhimu kwa Watanzania.

Naam, siku hiyo ya Novemba 14, wabunge wa CHADEMA (si wote, bali waliokuwapo ukumbi wa Bunge siku hiyo) walitoka nje ya ukumbi wa Bunge, mara baada ya Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria, Tundu Lissu, kuwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani, kuhusu muswada huo unaohusu mchakato wa Katiba mpya.

Wabunge hawa walitoka nje katika kile kinachoelezwa kuwa kutokukubaliana na uamuzi wa Serikali kusoma muswada huo kwa mara ya pili bungeni, kwa sababu haujatoa fursa kwa maoni ya wananchi kuzingatiwa.

Maoni ambayo hata hivyo kwa namna fulani, mbunge pia anapaswa kuyajua kupitia mikutano na wananchi wake.

Ni sahihi kwa wabunge kuhimiza maoni ya wananchi kuzingatiwa katika mchakato wa kutunga sheria yoyote si tu muswada huu wa Katiba mpya. Naunga mkono, wote wanaopigania haki ya wananchi kusikilizwa.

Hata hivyo, kasoro ambayo hata Kambi ya Upinzani haijawahi kuhoji ni kwamba; je, ni wakati gani au ni vigezo gani vinatumika kulifanya Bunge kuamini kuwa wananchi wameshirikishwa au kusikilizwa kiasi cha kutosha?

Ni idadi gani ya wananchi inapaswa itoe maoni yao au kusikilizwa? Ni wakulima, wafanyakazi au wanafunzi wangapi? Nini hasa vigezo vya Bunge, kama taasisi kujiridhisha kwamba sasa wananchi wametoa maoni yao kiasi cha kutosha?

Kwa mfano, wabunge wa CHADEMA wameshiriki kikamilifu katika Muswada wa Sheria ya Manunuzi ya Umma. Sikusikia wakishinikiza kwa nini maoni ya wananchi hayakusikilikizwa kwa kiasi cha kutosha.

Hapa bado izingatiwe kuwa mbele ya kanuni za Bunge, miswada yote ni sawa na inakusudia kulinda maslahi ya wapiga kura.

Binafsi, nimesikia zaidi maoni ya wananchi kuhusu Muswada wa Katiba mpya kuliko ambavyo nimesikia kuhusu Muswada wa Sheria ya Manunuzi ya Umma. Tatizo langu kama ilivyo kwa Watanzania wengine, bado hatuna kipimo iwe kwa kanuni za Bunge au vyovyote, kujiridhisha kuwa idadi ya waliotoa maoni inatosha au la.

Na kwa hiyo, siwezi kusema waliosikilizwa wanatosha ingawa najua baadhi ya hoja za waliotoa maoni yao zimezingatiwa na nyingine kupuuzwa.

Suala la pili la kutafakari ni je, kuna udhaifu wowote uliowahi kuelezwa wazi wazi na Kambi ya Upinzani Bungeni au hata wabunge wa CCM kwamba, mchakato wa kikanuni katika kutunga sheria umekuwa na kasoro? Kwamba ni mchakato usiotoa fursa kwa mbunge kutimiza wajibu wake kikamilifu, tena usiotambua kiasi cha ushiriki wa wananchi?

Kwa hiyo, kuna mawili yanajitokeza. Mosi, miswada yote mbele ya Bunge kikanuni ina nguvu sawa kwa sababu inalenga kumlinda mwananchi. Pili, mchakato wa kutunga sheria kwa mujibu wa kanuni za Bunge bado haujalalamikiwa katika mwelekeo unaojitokeza sasa? Tuendelee na mjadala ifuatavyo.

Ombwe la uongozi wabunge wa CHADEMA

Kuna dalili za ombwe la kiuongozi katika Kambi ya Wabunge wa CHADEMA. Kama si ombwe la uongozi, inawezekana ni ombwe la busara linaloibuka kwa msimu.

Kwanza, wabunge wa CHADEMA ingawa wanaweza kuwa ni wanaharakati, lakini bungeni hawako kwa ajili ya uanaharakati. Wapo kwa sababu wamepigiwa kura na wananchi (ukiondoa vitimaalumu ambao hata hivyo, bungeni wana fursa sawa na wengine).

Kama wabunge, jukumu lao la kwanza ni wananchi, si mkakati binafsi au wa chama kisiasa, ingawa udhaifu huu unajitokeza hata kwa wabunge wa CCM.

Hivyo, walipaswa kushiriki kuandaa mchakato wa muswada wa Katiba mpya kikamilifu baada ya kubaini wananchi wao majimboni hawakushirikishwa vya kutosha.

Kwa mfano, ni matarajio ya wengi mbunge anapokwenda bungeni bila shaka na hasa katika masuala ya miswada anakuwa tayari amesikiliza maoni ya wananchi jimboni anakotoka.

Kwa hiyo, kwa sababu hoja ya msingi ya wabunge wa CHADEMA ni wananchi kutosikilizwa, angalau wao wangeonesha hao wa majimbo yao waliowasilikiza wanasemaje. Wasingekimbia na maoni ya wananchi wao na kutoka nje ya ukumbi.

Wangesema kwanza, wangepigania maoni hayo kwanza yasikike kwa Watanzania wengine wote, katika chombo rasmi (Bunge). Baada ya maoni hayo, kusikika kwa Watanzania wote na kumbukumbu rasmi za Bunge (hansard) kuhifadhi, wangekwenda kusema majukwaani. Ni busara zaidi kutumia chombo rasmi kwanza.

Wangeweza kuwasilisha mapendekezo ya mabadiliko (amendments) katika baadhi ya vifungu ambavyo wananchi wao majimbo wanataka iwe hivyo.

Uwezo huu si tu wanao kwa mujibu wa kanuni za Bunge, lakini pia tumeshuhudia Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, akiutumia vizuri katika Muswada wa Sheria ya Manununi ya Umma, siku hiyo hiyo, Novemba 14, 2011, bungeni.

Kwa hiyo, kama ambavyo waliwasilisha maoni yao kupitia hotuba ya Tundu Lissu, ndivyo hivyo hivyo mbunge mmoja mmoja, hasa wa majimbo wangeeleza maoni ya wananchi wao na si kuyahodhi na kukimbia nayo, nje ya ukumbi wa Bunge.

Lakini hawakufanya hivyo, hawakuonesha mwelekeo kama wapinaji mahiri wenye mikakati kamili. Si tu wamehodhi na kukimbia na maoni ya wananchi wao majimboni, lakini wamewanyika fursa Watanzania kujua ili hatimaye wapime, wenzao hao wanasemaje.

Kwa hiyo, Watanzania kupitia Bunge, wameshindwa kujua maoni ya wananchi wa majimbo ya wabunge wa CHADEMA, ambayo kwa mujibu wa malalamiko yao, Bunge limeshindwa kuwapa fursa ya kusema. Hili ni kosa la kiufundi, linalohitaji mkakati mkubwa wa kisiasa kulifunika.

Binafsi ni mpiga kura wa Jimbo la Ubungo, Dar es Salaam. Nimuulize Mnyika; je, kitendo chake cha kukwepa kutumia kanuni za Bunge kupigania maoni yetu ambayo yeye na wenzake CHADEMA wanasema hatukusilizwa, kinatulinda kwa namna gani katika taswira hii ya ‘uovu’ wa Serikali?

Wakati gani wangeweza kutoka nje?


Hata hivyo, kwa sababu kususa ni haki ya wabunge, lakini swali la msingi na busara zaidi ni kujiuliza; je, ni wakati gani wa kufanya kitendo hicho?

Je, ni kabla ya kupigana kwa kutumia fursa za kikanuni zilizopo? Au ni kukimbia kwa kupuuza fursa hizo ambazo ni kushiriki mjadala na hata kuwasilisha mapendekezo ya mabadiliko (amendments)?

Kwa kuzingatia matakwa ya busara, naamini wakati muafaka kwa wabunge wa CHADEMA kutoka nje ya ukumbi wa Bunge ulikuwa ni baada ya mapendekezo yao (amendments) kuwasilishwa na kupuuzwa.

Kwa sasa, hawana ushahidi wa kumbukumbu rasmi za Bunge (hansard) kwamba, wamepuuzwa kwa kuzingatia kanuni za Bunge. Kizazi kijacho miaka mingi baadaye kama si hiki, kinaweza kuwashangaa kwa kukimbia fursa za kikanuni, kama kweli wao ni wapigania haki mahiri.

Kitendo cha kutoka nje ya ukumbi wa Bunge kilipaswa kuwa hatua ya mwisho. Yaani rufaa, inayowaunganisha wao na wananchi hasa wa majimbo wanayowawakilisha.

Tunajua maana ya rufaa. Rufaa ni lazima itanguliwe na juhudi nyingine ngazi za chini. Kwa suala la utungaji sheria, ngazi za chini kabla ya rufaa ni mosi; kushiriki mjadala ili kutoa maoni ya wananchi wako; pili, kupendekeza mabadiliko ili kulinda maoni ya wananchi wako; tatu, kama yote yameshindikana nadhani ndipo hatua ya kutoka nje ya ukumbi ingefuata.

Hata hivyo, hatua hii ya kutoka nje ya ukumbi nayo inapaswa kufanyika wakati muafaka ambao kwa suala hili ni pale Spika anapomwita Waziri, kuhitimisha hoja.
Hapa, wabunge wa CHADEMA wangekuwa wameonesha si tu uvumilivu mkubwa bali busara za kiwango cha juu. Yaani watakuwa wamepigana kwa kutumia fursa zote na mwishowe, rufaa ambayo ni majukwaa ya kisiasa.

Wangekuwa wametumia fursa ya kushiriki mjadala, kupendekeza mabadiliko, lakini kubwa zaidi, kusikiliza maoni ya wananchi wengine, kupitia wabunge wenzao nje ya majimbo yao na mwishowe, wangetoka nje.

Leo hii CHADEMA wanapotangaza maandamano nchi nzima watu wenye busara wanatafakari; je, wamejipatia fursa ya kutosha kusikiliza maoni ya wananchi wengine kupitia wabunge wengine na hasa kule walikosimamisha wagombea walioshindwa kura za ubunge?

Tafakari hii inatusogeza hatua nyingine ya kuanza kujiuliza kama kuna ombwe la uongozi katika Kambi ya CHADEMA? Kama lipo, linasababishwa na nini au nani? Je, hakuna uhuru wa maoni ili kurekebishana kwenye vikao vya ndani?

Hata hivyo, nimpongeze Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali (NCCR-Mageuzi), ambaye hakuwa katika mkumbo wa ombwe la ghafla la busara.

Alibaki bungeni, ingawa mwenzake, Felix Mkosamali alitoka nje baada ya dakika chache ili kuwafuata wabunge wa CHADEMA.

Machali ametambua kuwa anaweza kupigana katika dakika za mwisho kwa kuwasilisha maoni ya wapiga kura wake. Anaweza kupigana kupitia mjadala, kupitia mapendekezo ya mabadiliko (amendments) na mwishowe, kupigana kwa kuwasilisha hisia za wananchi wake kama maoni yao yatapuuzwa kwa kutoka nje wakati Waziri akihitimisha hoja ya muswada.

Hakika, tunahitaji viongozi vijana wenye akili za kutosha kiasi hiki, watulivu wa fikra, wepesi kutoa uamuzi wa busara. Hongera ‘mseminari’ Machali.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika

Bwana dilunga kumbe upepo wa Rai bado unao? Kwa Chadema kuendelea kukaa ndani ya Bunge ni sawa na kuwa kwemye chumba kimoja na wahalifu wakimbaka msichana wa shule na wewe ukisubiri tendo hilo la kinyama limalizike ili upata ushahidi wa kuripoti kituo cha polisi. Utabaki kuwa sehemu ya hao wahalifu, acha analysis za kiCCM panua wigo na angalia vitu kwa sura ya nyuma.
 
Tangu lini Mama Kinda akaruhusu hoja zinazoua CCM?
CDM wangeruhusiwa kutoa hoja zao kama walivyoomba unafikiri mjengoni pangetosha?
Dilunga huna hoja,usibeze na kutoa uchambuzi feki hapa wakati unajua fika kuwa CDM wangeruhusiwa kutoa hoja zao mama kinda na CCM yake huenda ndo ingekuwa inasaini cheti chake cha kufa wewe.

Acha CDM watoke nje ili angalau tupate wosia wa CCM kabla haijafa.
 
Mada yako imejaribu kugusa suala lilivo ila utakubaliana na mm kua impact kubwa kwa watanzania inapatikana kwenye muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba mpya zaidi ya muswada wa manunuzi ya umma ambao pia bunge kupitia nguvu kubwa ya ccm iliyoko bungeni walipitisha kitu ambacho madhara yake tutayaona miaka ijayo.

Hapa kwenye katiba ndipo palikua na maoni mengi yalioyokwishatolewa na taasisi na wanaharakati mbalimbali wakiwemo wanasheria wenyewe ndio maana spika alipokua anafungua mjadala alikua akijaribu kutengeneza mazingira ya kusomwa kwa muswada kwa mara ya pili na si kwa mara ya kwanza akiwa anajibu hoja na maoni yaliyokua tayari yametolewa kwenye media na kilichokua kikizungumzwa mitaani waliko wananchi na si kujibu hoja ya chadema peke yao ambao walikua na interest za kusikilizwa kwa huyo mtanzania aliye mtaani.

Bunge lifikie wakati lirealize kua kama kutokusikilizana, kejeli za spika na maneno machafu yanaweza yakajenga amani na uhuru wa maoni, ni bora kutoka bungeni kuliko sisi wananchi kuona thamani ya hao wabunge wetu inashushwa angali tumewapeleka pale kwa kura zetu.

Kwa mfano mbunge kuambiwa kaa chini unatupotezea muda ningependa niseme spika kama huyo hawezi kutoa mwongozo kwa kutumia kanuni angali yeye mwenyewe anazivunja kanuni na sheria za bunge, pia ni kinyume cha hata hiyo katiba tunayoitaka mabadiliko.
 
Nimesomaaa nilipofika sehemu anapoulinganisha muswada huu na ule wa sheria ya manunuzi ya uma nimechoka kabisa. Mwandishi asiyejua tofauti ya miswada hii miwili, asiyejua maana ya muswada huu kuwasilishwa mara ya kwanza au ya pili, asiyejua taratibu za haki za uundwaji wa katiba...

Masikini Watanganyika, hii makala ilivyofinyangwa itasomwa, na kwa hakika watu wasiotaka kushughulisha bongo zao wataikubali na hawataona hila iliyofichwa hapo!

Baada ya ule upinzani mkubwa waliopata toka kwa wananchi wakati ule wamejua watakachopata safari hii na wamekwepa kurudi kwa wananchi, wanataka waje ikiwa sheria tayari,halafu mnataka tufuate mkumbo kama mazezeta?
 
Naungana na Dilunga, wabunge wa cdm walitakiwa kuwepo na kujadili na kufanya marekebisho juu ya yale yaliyomo kwenye mswada huo, mi najua kabisa wanajua serikali yetu au CCM isingeweza hata iweje kuahirisha jambo hili hasa kwa sababu wao wamesusa lingewashushia wao credit. Kwa maana hii basi wamekubaliana na ubovu uliopo na hawajawawakilisha vema wananchi wao.
 
Chadema wameninyima fursa ya kuwasikiliza kuhusu hoja ya katiba wameniudhi kweli..

Nilitamani kusikiliza hoja zao na jinsiy wanavyowapelekesha ccm kwenye mambo ya sheria na kanuni lakini eti wanatoka nje..


Dilunga bado una hoja ya msingi sana, cdm wametunyima fursa yao ya kutupa mtazamo mbadala..
 
..at first niliona kama CDM wamekosea kutoka nje.

..lakini kama Spika hayuko tayari kuwa-treat fairly wakati wa mjadala mzima ni vizuri tu walivyotoka nje.

..sasa ninachowaomba CDM wapite nchi nzima wakihamasisha na kuelimisha wananchi kuhusu suala zima la katiba.

..tatizo kubwa zaidi ni wabunge wa chama tawala, ambao tungewategemea wawe na nidhamu zaidi, waliishia kuwashambulia na kuwasimanga wabunge wa CDM, particularly Tundu Lissu, badala ya kujadili hoja iliyokuwa mbele yao.

NB:

..mwandishi Godfrey Dilunga anakosea sana kulinganisha mswada wa Katiba na mswada wa sheria ya manunuzi.
 
at first niliona kama CDM wamekosea kutoka nje.

=Hadi sasa mimi naona chadema wamekosea kwasababu nilikuwa nafuatilia hiyo hoja in fact nilikuwa nataka michango ya upinzani zaidi wakaniyima fursa hiyo..

lakini kama Spika hayuko tayari kuwa-treat fairly wakati wa mjadala mzima ni vizuri tu walivyotoka nje.

=Hizo ni assumption kwasababu wangekuwepo ndani (luninga zingeonyesha halafu wangekuwa na sababu ya kuwashataki kwa wananchi)

sasa ninachowaomba CDM wapite nchi nzima wakihamasisha na kuelimisha wananchi kuhusu suala zima la katiba.

=Hii fursa ni wajibu baada ya hatua hii ya kwanza ya kuwepo chombo cha kusimamia maoni ya wananchi na pengine ingekuwa baada ya kujadiliana bila mafaniko (kama anavyosema dilunga wangepata watu wengi)..

tatizo kubwa zaidi ni wabunge wa chama tawala, ambao tungewategemea wawe na nidhamu zaidi, waliishia kuwashambulia na kuwasimanga wabunge wa CDM, particularly Tundu Lissu, badala ya kujadili hoja iliyokuwa mbele yao.

=Kweli kabisa wanaboa sana hasa kwenye issue ya katiba..hovyo kabisa

mwandishi Godfrey Dilunga anakosea sana kulinganisha mswada wa Katiba na mswada wa sheria ya manunuzi

= Mwandishi hajakosea alikuwa analinganisha ushirikiswaji wa wananchi kwenye muswada ya bungeni zote zinakuwa sawa ..kwasababu huu ulikuwa utaratibu wa kupata namna ya kupata katiba tu..na si vinginevyo..
 
Ama kweli Ufahamu wa Mtazania unatia shaka sana ktk kuelewa nguvu ya Katiba Mpya na muswada mwingine wowote ndani ya katiba iliyopo. Ni sawa na kushindwa kuelewa hoja na umuhimu wa tatizo la kufungisha watu ndoa na ule wa manunuzi ya vitu kwa wanandoa. KATIBA MPYA ipo juu ya yote haya na muswada wake lazima itokane na hali halisi. Huwezi kuweka sheria ya haki za binadamu ikiwa kwanza huelewi ni haki zipi zinazodaiwa au takikana. Chukulia hata mabadiliko ya kikatiba ya Apartheid. Bunge la SA halikukaa lenyewe likaamua kutunga sheria, ama rais wao kutoa mchakato wa kutunga sheria mpya bila kuelewa kwanza tatizo ni kitu gani.

Sasa jambo ambalo sisi wananchi tunalolalamikia kuhusu katiba iliyopo hawalifahamu na viongozi wa chama na wanasheria wameonyesha mara nyingi kutoona kasoro ya katiba iliyopo japokuwa wanadai kutatazama haki za wananchi zilizopelekea wao kuomba katiba mpya. Sasa mwanzo tu unalipeleka swala hili kisiasa ambako wanafahamu wazi kuwa wao wana uwakilishi mkubwa zaidi, hawa watu wataweza vipi kujenga hata kamati ya mchakato ikiwa hawaelewi makosa yako ndani ya katiba na hata kama yapo hawaoni sababu ya kuandikwa katiba mpya isipokuwa kufanyiwa marekebisho?. Je, mmesahau jinsi Makaburu walivyoshindwa kupitisha bungeni kuondoka kwa Apartheid hadi walipolazimishwa na mataifa?

Jamani tuwe wakweli na nafsi zetu, sielewi kabisa kwa nini mapendekezo ya katiba mpya yamekwenda kwanza bungeni kabla hujawapitia wananchi wenyewe. CCM wanajua fika kwamba Katiba mpya ni kuondoa life support ya chama kuweza kuongoza kwa mabavu. Katiba iliyopo ni ya chama kimoja ambayo ni sawa na katiba ya CCM wenyewe (kundi la watawala) na inawapa mamlaka makubwa sana uongozi wa CCM kitaifa..
 
Topical,

..siyo lazima wasemee ndani ya bunge ndiyo wananchi tupate kuwasikia.

..zaidi, walikuwepo ndani ya bunge na wakaomba mswada usomwe kwa mara ya kwanza, Spika akakataa.

..mswada ungesomwa kwa mara ya kwanza, ungetoa fursa kwa wananchi kuujadili nje ya bunge, kabla ya kupitishwa rasmi kwa utekelezaji.

..pia kuna hotuba ya msemaji mkuu wa masuala ya katiba na sheria wa kambi ya upinzani, Mh.Tundu Lissu. Hiyo ndiyo dira ya nini wapinzani wanakitaka ktk mchakato mzima wa kuandika katiba.
 
Topical,

..siyo lazima wasemee ndani ya bunge ndiyo wananchi tupate kuwasikia.

..zaidi, walikuwepo ndani ya bunge na wakaomba mswada usomwe kwa mara ya kwanza, Spika akakataa.

..mswada ungesomwa kwa mara ya kwanza, ungetoa fursa kwa wananchi kuujadili nje ya bunge, kabla ya kupitishwa rasmi kwa utekelezaji.

..pia kuna hotuba ya msemaji mkuu wa masuala ya katiba na sheria wa kambi ya upinzani, Mh.Tundu Lissu. Hiyo ndiyo dira ya nini wapinzani wanakitaka ktk mchakato mzima wa kuandika katiba.
Unajua Tropical mhuni au analeta tabia za kihuni...Mtu kuepuka confrontation basi kwake yeye ni udhaifu yaani unapokutana na mtu mgonvi, amekosea ukamsahihisha akasema so what? ukamua kuondoka basi wewe mwoga ulitakiwa kupambana naye hadi kieleweke palepale..
Kuondoka kwa Chadema bungeni wametumia hekima kubwa..wananchi tunamjua sasa mkorofi nani.
 
Unajua Tropical mhuni au analeta tabia za kihuni...Mtu kuepuka confrontation basi kwake yeye ni udhaifu yaani unapokutana na mtu mgonvi, amekosea ukamsahihisha akasema so what? ukamua kuondoka basi wewe mwoga ulitakiwa kupambana naye hadi kieleweke palepale..
Kuondoka kwa Chadema bungeni wametumia hekima kubwa..wananchi tunamjua sasa mkorofi nani.

Mkuu acha hizo bana mimi si mhuni ...nina heshima zangu kwanza kwa wake zangu wawili (wewe naamini kuongoza hao watu wawili) pili watoto, tatu taifa...

Huo msimamo wa chadema kweli unanipa tabu si kwasababu nawafurahia ccm NO ..niliweza kujianda kusikiliza nondo za chadema wakakimbia nikaogopa kwamba hawa jamaa vipi tena ndio wakati wa kutoa reservations zangu kuhusu wao ndio wakaingia kwenye mtego big time???

wamefanya makosa makubwa sana..
 
Topical,

..siyo lazima wasemee ndani ya bunge ndiyo wananchi tupate kuwasikia.

..zaidi, walikuwepo ndani ya bunge na wakaomba mswada usomwe kwa mara ya kwanza, Spika akakataa.

..mswada ungesomwa kwa mara ya kwanza, ungetoa fursa kwa wananchi kuujadili nje ya bunge, kabla ya kupitishwa rasmi kwa utekelezaji.

..pia kuna hotuba ya msemaji mkuu wa masuala ya katiba na sheria wa kambi ya upinzani, Mh.Tundu Lissu. Hiyo ndiyo dira ya nini wapinzani wanakitaka ktk mchakato mzima wa kuandika katiba.

Naomba nikuulize waziri kivuli alijua lini kwamba muswada huu utasomwa mara pili bungeni na si mara ya kwanza????

Waziri taarifa hizi anazo prior to bunge session kwanini asingeleta hoja hiyo kwa umma mapema????
 
Godfrey Dilunga-Raia Mwema

NOVEMBA 14, mwaka huu, Serikali kupitia kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani, iliwasilisha Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba mpya.

Muswada ambao utakaoongoza wananchi kutoa maoni yao kuhusu Katiba mpya. Tukio hilo lilitanguliwa na kazi nyingine ya uwasilishaji, mjadala na uridhiaji wa Muswada wa Sheria ya Manunuzi ya Umma.

.................................
Hayo ni maoni yake mkuu. Wasikilize vizuri viongozi wa CHADEMA na hoja zao. Mpaka sasa hatua walizochukua tunaziunga mkono. Ila viongozi na Wabunge walioshiba vipesa vya serikali wanadiliki kutetea muswada ambao hata majority ya wataalamu wa sheria wameu-criticize.
Namuheshimu sana jenerali Ulimwengu, aangalie hao wanahabari wake wasije kumwaribia la CCM imeshaanza kumwingilia na hali najua hana chama.
 
Topical,

..tetesi kwamba mswada utasomwa kwa mara ya pili zilikuwepo na wananchi walikuwa wanajua.

..suala hilo lilijadiliwa pia ktk kamati ya sheria na katiba na wabunge wa upinzani walioeleza msimamo wao.

..hatua ya mwisho ilikuwa busara za Spika kuokoa jahazi kwa kuelekeza kwamba mswada usomwe kwa mara ya kwanza.

..kwa wakati huu kwanini usitupe mtizamo wako kuhusu hotuba iliyotolewa na msemaji wa kambi rasmi ya upinzani kuhusu mswada huu?
 
Back
Top Bottom