Wabunge CHADEMA wamedanganyika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge CHADEMA wamedanganyika?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Nov 17, 2011.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Nov 17, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Godfrey Dilunga-Raia Mwema

  NOVEMBA 14, mwaka huu, Serikali kupitia kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani, iliwasilisha Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba mpya.

  Muswada ambao utakaoongoza wananchi kutoa maoni yao kuhusu Katiba mpya. Tukio hilo lilitanguliwa na kazi nyingine ya uwasilishaji, mjadala na uridhiaji wa Muswada wa Sheria ya Manunuzi ya Umma.

  Katika taswira ya Bunge, hasa kwa mujibu wa kanuni zake, Muswada wa Sheria ya Manunuzi na Muswada wa Mabadiliko ya Katiba, yote ni miswada. Mbele ya kanuni za Bunge, ina nguvu sawa.

  Majukumu ya mbunge na Bunge ni pamoja na kutunga sheria. Mpiga kura anayekwenda kituo cha upigaji kura kumchagua mbunge, anatambua moja ya kazi ya atakayemchagua ni kutunga sheria, kwa niaba yake.

  Ni makosa kwa mbunge au kundi la wabunge kudhani au kujenga dhana kwamba muswada fulani si muhimu kwa kulinganisha na muswada mwingine.

  Dhana hii ni potofu kwa sababu tafsiri inayoweza kujitokeza ni kwamba, wabunge wenye mtazamo huo ni kama wanawaaminisha Watanzania kuwa zipo sheria ambazo ni mbovu wameshiriki kuzitunga. Kwamba ipo miswada wameiridhia isiyo na umuhimu kwa Watanzania.

  Naam, siku hiyo ya Novemba 14, wabunge wa CHADEMA (si wote, bali waliokuwapo ukumbi wa Bunge siku hiyo) walitoka nje ya ukumbi wa Bunge, mara baada ya Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria, Tundu Lissu, kuwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani, kuhusu muswada huo unaohusu mchakato wa Katiba mpya.

  Wabunge hawa walitoka nje katika kile kinachoelezwa kuwa kutokukubaliana na uamuzi wa Serikali kusoma muswada huo kwa mara ya pili bungeni, kwa sababu haujatoa fursa kwa maoni ya wananchi kuzingatiwa.

  Maoni ambayo hata hivyo kwa namna fulani, mbunge pia anapaswa kuyajua kupitia mikutano na wananchi wake.

  Ni sahihi kwa wabunge kuhimiza maoni ya wananchi kuzingatiwa katika mchakato wa kutunga sheria yoyote si tu muswada huu wa Katiba mpya. Naunga mkono, wote wanaopigania haki ya wananchi kusikilizwa.

  Hata hivyo, kasoro ambayo hata Kambi ya Upinzani haijawahi kuhoji ni kwamba; je, ni wakati gani au ni vigezo gani vinatumika kulifanya Bunge kuamini kuwa wananchi wameshirikishwa au kusikilizwa kiasi cha kutosha?

  Ni idadi gani ya wananchi inapaswa itoe maoni yao au kusikilizwa? Ni wakulima, wafanyakazi au wanafunzi wangapi? Nini hasa vigezo vya Bunge, kama taasisi kujiridhisha kwamba sasa wananchi wametoa maoni yao kiasi cha kutosha?

  Kwa mfano, wabunge wa CHADEMA wameshiriki kikamilifu katika Muswada wa Sheria ya Manunuzi ya Umma. Sikusikia wakishinikiza kwa nini maoni ya wananchi hayakusikilikizwa kwa kiasi cha kutosha.

  Hapa bado izingatiwe kuwa mbele ya kanuni za Bunge, miswada yote ni sawa na inakusudia kulinda maslahi ya wapiga kura.

  Binafsi, nimesikia zaidi maoni ya wananchi kuhusu Muswada wa Katiba mpya kuliko ambavyo nimesikia kuhusu Muswada wa Sheria ya Manunuzi ya Umma. Tatizo langu kama ilivyo kwa Watanzania wengine, bado hatuna kipimo iwe kwa kanuni za Bunge au vyovyote, kujiridhisha kuwa idadi ya waliotoa maoni inatosha au la.

  Na kwa hiyo, siwezi kusema waliosikilizwa wanatosha ingawa najua baadhi ya hoja za waliotoa maoni yao zimezingatiwa na nyingine kupuuzwa.

  Suala la pili la kutafakari ni je, kuna udhaifu wowote uliowahi kuelezwa wazi wazi na Kambi ya Upinzani Bungeni au hata wabunge wa CCM kwamba, mchakato wa kikanuni katika kutunga sheria umekuwa na kasoro? Kwamba ni mchakato usiotoa fursa kwa mbunge kutimiza wajibu wake kikamilifu, tena usiotambua kiasi cha ushiriki wa wananchi?

  Kwa hiyo, kuna mawili yanajitokeza. Mosi, miswada yote mbele ya Bunge kikanuni ina nguvu sawa kwa sababu inalenga kumlinda mwananchi. Pili, mchakato wa kutunga sheria kwa mujibu wa kanuni za Bunge bado haujalalamikiwa katika mwelekeo unaojitokeza sasa? Tuendelee na mjadala ifuatavyo.

  Ombwe la uongozi wabunge wa CHADEMA

  Kuna dalili za ombwe la kiuongozi katika Kambi ya Wabunge wa CHADEMA. Kama si ombwe la uongozi, inawezekana ni ombwe la busara linaloibuka kwa msimu.

  Kwanza, wabunge wa CHADEMA ingawa wanaweza kuwa ni wanaharakati, lakini bungeni hawako kwa ajili ya uanaharakati. Wapo kwa sababu wamepigiwa kura na wananchi (ukiondoa vitimaalumu ambao hata hivyo, bungeni wana fursa sawa na wengine).

  Kama wabunge, jukumu lao la kwanza ni wananchi, si mkakati binafsi au wa chama kisiasa, ingawa udhaifu huu unajitokeza hata kwa wabunge wa CCM.

  Hivyo, walipaswa kushiriki kuandaa mchakato wa muswada wa Katiba mpya kikamilifu baada ya kubaini wananchi wao majimboni hawakushirikishwa vya kutosha.

  Kwa mfano, ni matarajio ya wengi mbunge anapokwenda bungeni bila shaka na hasa katika masuala ya miswada anakuwa tayari amesikiliza maoni ya wananchi jimboni anakotoka.

  Kwa hiyo, kwa sababu hoja ya msingi ya wabunge wa CHADEMA ni wananchi kutosikilizwa, angalau wao wangeonesha hao wa majimbo yao waliowasilikiza wanasemaje. Wasingekimbia na maoni ya wananchi wao na kutoka nje ya ukumbi.

  Wangesema kwanza, wangepigania maoni hayo kwanza yasikike kwa Watanzania wengine wote, katika chombo rasmi (Bunge). Baada ya maoni hayo, kusikika kwa Watanzania wote na kumbukumbu rasmi za Bunge (hansard) kuhifadhi, wangekwenda kusema majukwaani. Ni busara zaidi kutumia chombo rasmi kwanza.

  Wangeweza kuwasilisha mapendekezo ya mabadiliko (amendments) katika baadhi ya vifungu ambavyo wananchi wao majimbo wanataka iwe hivyo.

  Uwezo huu si tu wanao kwa mujibu wa kanuni za Bunge, lakini pia tumeshuhudia Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, akiutumia vizuri katika Muswada wa Sheria ya Manununi ya Umma, siku hiyo hiyo, Novemba 14, 2011, bungeni.

  Kwa hiyo, kama ambavyo waliwasilisha maoni yao kupitia hotuba ya Tundu Lissu, ndivyo hivyo hivyo mbunge mmoja mmoja, hasa wa majimbo wangeeleza maoni ya wananchi wao na si kuyahodhi na kukimbia nayo, nje ya ukumbi wa Bunge.

  Lakini hawakufanya hivyo, hawakuonesha mwelekeo kama wapinaji mahiri wenye mikakati kamili. Si tu wamehodhi na kukimbia na maoni ya wananchi wao majimboni, lakini wamewanyika fursa Watanzania kujua ili hatimaye wapime, wenzao hao wanasemaje.

  Kwa hiyo, Watanzania kupitia Bunge, wameshindwa kujua maoni ya wananchi wa majimbo ya wabunge wa CHADEMA, ambayo kwa mujibu wa malalamiko yao, Bunge limeshindwa kuwapa fursa ya kusema. Hili ni kosa la kiufundi, linalohitaji mkakati mkubwa wa kisiasa kulifunika.

  Binafsi ni mpiga kura wa Jimbo la Ubungo, Dar es Salaam. Nimuulize Mnyika; je, kitendo chake cha kukwepa kutumia kanuni za Bunge kupigania maoni yetu ambayo yeye na wenzake CHADEMA wanasema hatukusilizwa, kinatulinda kwa namna gani katika taswira hii ya ‘uovu' wa Serikali?

  Wakati gani wangeweza kutoka nje?


  Hata hivyo, kwa sababu kususa ni haki ya wabunge, lakini swali la msingi na busara zaidi ni kujiuliza; je, ni wakati gani wa kufanya kitendo hicho?

  Je, ni kabla ya kupigana kwa kutumia fursa za kikanuni zilizopo? Au ni kukimbia kwa kupuuza fursa hizo ambazo ni kushiriki mjadala na hata kuwasilisha mapendekezo ya mabadiliko (amendments)?

  Kwa kuzingatia matakwa ya busara, naamini wakati muafaka kwa wabunge wa CHADEMA kutoka nje ya ukumbi wa Bunge ulikuwa ni baada ya mapendekezo yao (amendments) kuwasilishwa na kupuuzwa.

  Kwa sasa, hawana ushahidi wa kumbukumbu rasmi za Bunge (hansard) kwamba, wamepuuzwa kwa kuzingatia kanuni za Bunge. Kizazi kijacho miaka mingi baadaye kama si hiki, kinaweza kuwashangaa kwa kukimbia fursa za kikanuni, kama kweli wao ni wapigania haki mahiri.

  Kitendo cha kutoka nje ya ukumbi wa Bunge kilipaswa kuwa hatua ya mwisho. Yaani rufaa, inayowaunganisha wao na wananchi hasa wa majimbo wanayowawakilisha.

  Tunajua maana ya rufaa. Rufaa ni lazima itanguliwe na juhudi nyingine ngazi za chini. Kwa suala la utungaji sheria, ngazi za chini kabla ya rufaa ni mosi; kushiriki mjadala ili kutoa maoni ya wananchi wako; pili, kupendekeza mabadiliko ili kulinda maoni ya wananchi wako; tatu, kama yote yameshindikana nadhani ndipo hatua ya kutoka nje ya ukumbi ingefuata.

  Hata hivyo, hatua hii ya kutoka nje ya ukumbi nayo inapaswa kufanyika wakati muafaka ambao kwa suala hili ni pale Spika anapomwita Waziri, kuhitimisha hoja.
  Hapa, wabunge wa CHADEMA wangekuwa wameonesha si tu uvumilivu mkubwa bali busara za kiwango cha juu. Yaani watakuwa wamepigana kwa kutumia fursa zote na mwishowe, rufaa ambayo ni majukwaa ya kisiasa.

  Wangekuwa wametumia fursa ya kushiriki mjadala, kupendekeza mabadiliko, lakini kubwa zaidi, kusikiliza maoni ya wananchi wengine, kupitia wabunge wenzao nje ya majimbo yao na mwishowe, wangetoka nje.

  Leo hii CHADEMA wanapotangaza maandamano nchi nzima watu wenye busara wanatafakari; je, wamejipatia fursa ya kutosha kusikiliza maoni ya wananchi wengine kupitia wabunge wengine na hasa kule walikosimamisha wagombea walioshindwa kura za ubunge?

  Tafakari hii inatusogeza hatua nyingine ya kuanza kujiuliza kama kuna ombwe la uongozi katika Kambi ya CHADEMA? Kama lipo, linasababishwa na nini au nani? Je, hakuna uhuru wa maoni ili kurekebishana kwenye vikao vya ndani?

  Hata hivyo, nimpongeze Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali (NCCR-Mageuzi), ambaye hakuwa katika mkumbo wa ombwe la ghafla la busara.

  Alibaki bungeni, ingawa mwenzake, Felix Mkosamali alitoka nje baada ya dakika chache ili kuwafuata wabunge wa CHADEMA.

  Machali ametambua kuwa anaweza kupigana katika dakika za mwisho kwa kuwasilisha maoni ya wapiga kura wake. Anaweza kupigana kupitia mjadala, kupitia mapendekezo ya mabadiliko (amendments) na mwishowe, kupigana kwa kuwasilisha hisia za wananchi wake kama maoni yao yatapuuzwa kwa kutoka nje wakati Waziri akihitimisha hoja ya muswada.

  Hakika, tunahitaji viongozi vijana wenye akili za kutosha kiasi hiki, watulivu wa fikra, wepesi kutoa uamuzi wa busara. Hongera ‘mseminari' Machali.

  Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika
   
 2. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #2
  Nov 17, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Dilunga ukiwa ccm huwezi kuona upande mwingine kuwa upo sawa.Kilichowatoa cdm ni unyanyasaji wa spika na mazingira aliyoyatengeneza huyo mama kinda kwa kuonyesha wazi kuwa matokeo yameshapangwa kwa hiyo hata wangesema vp wasingebadilisha chochote.

  Kile walichokifanya kiko sahihi kabisa kwa context hiyo.IMPACT ZAKE MABALOZI WA EU WAMEANZA KULIFUATILIA KWA UKARIBU SUALA HILI NA SERIKALI IMEANZA KUHAHA eti mabalozi wanasaidia vyama vya siasa kuvuruga amani.
   
 3. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Tayari waliomba mingozo ikakataliwa bora wamejitokea zao nje kuliko washiriki ku2chimbia kaburi,
   
 4. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #4
  Nov 17, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,133
  Likes Received: 7,382
  Trophy Points: 280
  Ndio maana nakupenda sana!!!!!
   
 5. only83

  only83 JF-Expert Member

  #5
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Analysis nzuri lakini isiyotambua mazingira ya siasa za fitina na CCM na serikali yake......Wakati mjadala haujaanza wabunge kadhaa waliomba mwongozo au taarifa kwa spika wa bunge...lakini kwa kiburi cha uzima spika akawanyima haki hiyo..Je, katika mazingira hayo unategemea nini?

  Mbunge wa NCCR-Mageuzi ndugu Mkosamali alijitahidi kuomba mwongozo wa spika kabla hajatoka,spika kwa kiburi hakakataa na jibu la mkosamali ilikuwa basi na mimi natoka.......

  Jamani tukubaliane kuwa siasa za CCM na serikali yake hazina nia njema na watanzania.Lakini pia ni kweli kuwa miswada yote ni sawa lakini huyu mwandishi akumbuke kuwa KATIBA ni sheria mama uwezi kumfananisha mama na shangazi ukasema wote ni sawa na wanauzito sawa machoni mwa watu....
   
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Nov 17, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Kauli mbiu ya CHADEMA: WAO WANA PESA, SISI TUNA MUNGU!

  Kwa kauli mbiu hiyo utaona kwamba chadema hawadanganyiki!
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  hivi katiba unaweza kulinganisha na sheria ya manunuzi...
   
 8. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #8
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Dilunga, kutoka nje ndo kutowakilisha wananchi eeh? Kubaki ndani ya bunge na kuhalalisha mchakato haramu, tena wa hila na wa kidekteta kwa maslah ya ccm na kundi fulani wenye maslah binafsi ndo uwakilishi sahihi?

  Labda unge-define uwakilishi ujuavyo wewe & ccm ndipo hiyo "analysis" yako ingetumika; LAKINI ktk hali halisi huo uozo ulioweka ktk maandishi ni petrol kwenye moto.
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  Nov 17, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nilifikiri yule Profesa anayetumiwa na CCM ndio mtu pekee aliyekubali kidhalilisha taaluma kumbe kuna huyu Godfrey Dilunga! Hivi huyu mwandishi anaweza kusema nini maana ya muswada kusomwa kwa mara ya kanzwa, au mara ya pili?

  Mara ya kwanza ina maana muswada unakuwa kwa wananchi kuujadili, mara ya pili unaenda kwa wabunge kujadili baada ya kupata maoni ya wananchi? Sasa ni lini wananchi wa Tanzania walipewa nafasi ya kujasidili muswaada wa kutunga katiba mpya? Asije na porojo za muswada wa Mwezi March maana hata bungeni serikali ilitimuliwa nao kwa sababu ulikuwa mbovu mno. Na wananchi wengi wasingeweza kuujadili kwa sababu kwanza ulikuwa kwa lugha ya kiingereza. Hivi mtu ukiwa darasa la pili lakini kutokana na maendeleo mabaya walimu wakakurudisha darasa la kwanza utaendelea kusema unasoma darasa la pili wakati ukweli unasoma darasa la kwanza?

  Huyu mwandishi anataka atambue kuwa wananchi wametuma wabunge kuwawakilisha, lakini wananchi wanataka wawakilishe hoja/maoni baada ya kuwasiliana/kujadiliana nao. Ni mbunge yupi (CCM, CUF, CHADEMA, TPL etc) aliyekaa na wananchi wake wakaupitia huu muswada kabla ya kwenda bungeni kujadili. Sasa kama mbunge hujakaa na wananchi wako mkazungumza mambo yaliyomo ndani ya muswada unawezaje kusema unawakilisha maoni yao? YEPI? Na hapa ndio CCM wanatakiwa watueleze kama wanatumia nguvu za majini au za roho mtakatifu kujua nini wananchi wa majimbo wanayotoka wanasema kuhusu huu muswada!

  Hivyo hoja ya CHADEMA ina nguvu kimamlaka na kimantiki kwamba kabla wawakilishi wa wananchi hawajajadili ni lazima wawe wamepata maoni ya wapiga kura wao. Na kama tulikuwa na spika anayejua nini maana ya katiba na utawala bora basi angetoa nakala ya huu muswada kwa kila mbunge na kuwaambia warudi kwenye majimbo yao wakaongee na wananchi na kupata maoni yao. Hivyo kama kuna umbwe la uongozi basi ni kwenye kiti cha U-spika sio CHADEMA.
   
 10. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #10
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,649
  Likes Received: 4,751
  Trophy Points: 280
  Hivi gazeti la Raia mwema limenunuliwa na nani vile?
   
 11. J

  Jobo JF-Expert Member

  #11
  Nov 17, 2011
  Joined: May 15, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Huyu Dilunga ni nani ati? Akili zake mbona kama zimesinzia vile?
   
 12. N

  Nyamanoro JF-Expert Member

  #12
  Nov 17, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 577
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 60


  Uzoefu walionao CHADEMA kwa Bunge hili wana kila sababu za kutoka nje. Kitendo cha kuwepo kwenye mjadala wa muswada ambao hauna baraka za wananchi ni usaliti. Tasnia ya habari nchini imevamiwa na wanahabari washabiki ambao hawatusaidii sisi wananchi hata kidogo.
   
 13. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #13
  Nov 17, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kazi ya mbunge bungeni ni pamoja na:
  • kuwawakilisha wananchi bungeni - yaani anakuwepo kwa niaba ya wananchi walio wengi ammao si rahisi wote kuingia bungeni kwa pamoja kwa sababu mbalimbali.
  • kuwasilisha maoni ya wananchi - Mbunge kabla hajaenga bungeni anapaswa akutane na wananchi wake wampe hoja zao kuhusiana ajenda za kikao husika sasa ktk hili ni mbunge gani aliye kaa na wananchi wake hata akapata maoni yao ya kuwasemea huko namna ya kuunda kamati ya kusimamia maoni ya uundwaji wa katiba mpya
  Spika anapo kataa mapendekezo aonekane vipi yeye ni mungu, Bila kumng'unya maneno hawa tayari katiba wanayoitaka wanayo hii yote ni geresha tu. Labda tusitumie garama kubwa sana watusomee hiyo waliyo iandaa kama kuna marekebisho yanawezekana basi tuyarekebishe
   
 14. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #14
  Nov 17, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Dilunga na umahiri wake ameshindwa kuliona hili, du sasa nimeamini waandishi wote wachumia tumbo.
   
 15. TECHMAN

  TECHMAN JF-Expert Member

  #15
  Nov 17, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 2,677
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  Kama mbunge ni muwakilishi wa wananchi bungeni, anaposimama mbunge na spika akakataa kumpa fursa ya kuzungumza, inamaana kuwa amewanyima wananchi mawazo yao kuwakilishwa. huyu anatakiwa kuadhibiwa na wananchi. cha ajabu ni kuwa jambo hili spika huwafanyia watu wa upinzani tu.
   
 16. U

  UMPUUTI Member

  #16
  Nov 17, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mdau mimi binafsi napenda nikupongeze kwa uchambuzi makini juu ya tafrani hii iliyojitokeza. Kimsingi nakubaliana na hoja zote katika makala yako.Ni hoja zinazojielekeza kwenye uhalisia wa mambo na wala sio ushabiki ndani yake.Sasa, najua sio lazima kila mtu atakuunga mkono maana ni hulka ya baadhi ya watu kupinga kila kitu ingawa nafsi zinakuwa zinawasuta waziwazi juu ya kile wanachokipinga. Kiukweli, wadau makini wa harakati za kisiasa hapa nchini tukubali,tusikubali kuna kosa kubwa sana la kiufundi limefanywa na wabunge wa Chadema katika jambo hili. Sasa mimi nashindwa kuelewa kama kweli waheshimiwa hawa huwa wanakubaliana kwa pamoja kufanya maamuzi kama haya au la.Napata tabu kuaamini kwamba kweli hakuna hata mbunge mmoja kati yao aliyeweza kushtuka kwamba litakuwa ni kosa la kiufundi kuchukua uamuzi ule kwa haraka kiasi kile? Mdau umefafanua vizuri sana juu wakati gani muafaka ungefaa kuchukua uamuzi waliouchukua,wala sina haja ya kurudia. Sasa,tunasema ni kosa la kiufundi.Kwa kuongezea tu kwenye uchambuzi wako utaona kwamba, tangu mjadala umeanza,wenzao wa CCM na CUF wamekuwa wakiwapiga vijembe,kuwashambulia,na kuwashutumu mno.Wamekuwa wakikibebeshwa kila aina ya tuhuma. Hivyo basi,imekuwa ni shauku ya watanzania kutaka kusikia upande wa pili unaobebeshwa hizo shutuma,wanajiteteaje? Bahati mbaya wanaotuhumiwa hawapo bungeni kujibu tuhuma hizo,wametoka nje ya ukumbi. Na kwa bahati mbaya sana ni kwamba, ni watanzani wachache sana waliofuatilia maoni ya kambi ya upinzani siku yaliposomwa na msemaji wao Mh.Tundu Lisu na hivyo kujua nini hasa yalikuwa maoni yao.Baada ya hapo Kilichotokea ni kwamba, wananchi wengi walianza kuufutilia mjadala huu baada ya wabunge wa Chadema kususia mjadala.Sasa, walichokutana ncho ni mashambulizi makali kutoka kwa wabunge wa CCM na CUF.Mashambulizi hayo kwa kweli yamevuta hisia za wananchi wengi maana kila mbunge anayesimama kuchangia lazima kwanza aanze na vijembe na kisha kutoa uafafanuzi na kujitahidi kuwaelewesha wananchi juu nini kinachoendelea.Sasa hapa ndipo kosa la kiufundi linapojitokeza maana watuhumiwa wako nje ya ukumbi wakiruhusu mashambulizi makali yawaaendee biila ya wao kuwepo na hivyo kujibu mapigo kwa hoja zile zile wanazosimamia. NCCR Mageuzi wamekuwa wajanja ndio maana zaidi ya Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali kuchangia lakini jana pia tulimuona Mheshimiwa Buyogera Mbunge wa Kasulu Vijijij (NCCR-Mageuzi) akipambana. Naamini waheshimwa wa NCCR walishashtuka kuwa kuna kosa la kiufundi lilifanyika siku ya kwanza.Sasa,Kuna hoja kwamba spika alizuia miongozo kwa wabunge.Sawa,inaweza kuwa ni hoja.Lakini siamini kwamba hilo lilikuwa ni tatizo kubwa sana kwani kama ingekuwa ni tatizo,basi hata msemaji wa kambi ya upinzani Mh.Tundu Lisu asingekubali kuwasilisha maoni yao mpaka Spika kwanza akubali kutoa miongozo iliyoombwa kutolewa na wabunge ndipo aendelee na kusoma maoni ya kambi ya upinzani.Lakini ni kwa kutambua kuwa halikuwa tatizo ndio maana alipoitwa na Spika kutoa maoni yao alifanya hivyo. Kwa hiyo,nadhani itakuwa ni busara zaidi kukiri kwamba kweli kilichofanywa na wabunge wa Chadema lilikuwa ni kosa kubwa la kiufundi katika mapambano yanayohitaji uungwaji mkono wa umma. Na wala hamna kuona haya katika hili,kwa kuwa makosa ya kiufundi yapo na huwa yanatokea.Cha msingi ni kujipanga na kusonga mbele! Mungu ibariki Tanzania na watu wake!!
   
 17. U

  UMPUUTI Member

  #17
  Nov 17, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mdau mimi binafsi napenda nikupongeze kwa uchambuzi makini juu ya tafrani hii iliyojitokeza. Kimsingi nakubaliana na hoja zote katika makala yako.Ni hoja zinazojielekeza kwenye uhalisia wa mambo na wala sio ushabiki ndani yake.Sasa, najua sio lazima kila mtu atakuunga mkono maana ni hulka ya baadhi ya watu kupinga kila kitu ingawa nafsi zinakuwa zinawasuta waziwazi juu ya kile wanachokipinga. Kiukweli, wadau makini wa harakati za kisiasa hapa nchini tukubali,tusikubali kuna kosa kubwa sana la kiufundi limefanywa na wabunge wa Chadema katika jambo hili. Sasa mimi nashindwa kuelewa kama kweli waheshimiwa hawa huwa wanakubaliana kwa pamoja kufanya maamuzi kama haya au la.Napata tabu kuaamini kwamba kweli hakuna hata mbunge mmoja kati yao aliyeweza kushtuka kwamba litakuwa ni kosa la kiufundi kuchukua uamuzi ule kwa haraka kiasi kile? Mdau umefafanua vizuri sana juu wakati gani muafaka ungefaa kuchukua uamuzi waliouchukua,wala sina haja ya kurudia. Sasa,tunasema ni kosa la kiufundi.Kwa kuongezea tu kwenye uchambuzi wako utaona kwamba, tangu mjadala umeanza,wenzao wa CCM na CUF wamekuwa wakiwapiga vijembe,kuwashambulia,na kuwashutumu mno.Wamekuwa wakikibebeshwa kila aina ya tuhuma. Hivyo basi,imekuwa ni shauku ya watanzania kutaka kusikia upande wa pili unaobebeshwa hizo shutuma,wanajiteteaje? Bahati mbaya wanaotuhumiwa hawapo bungeni kujibu tuhuma hizo,wametoka nje ya ukumbi. Na kwa bahati mbaya sana ni kwamba, ni watanzani wachache sana waliofuatilia maoni ya kambi ya upinzani siku yaliposomwa na msemaji wao Mh.Tundu Lisu na hivyo kujua nini hasa yalikuwa maoni yao.Baada ya hapo Kilichotokea ni kwamba, wananchi wengi walianza kuufutilia mjadala huu baada ya wabunge wa Chadema kususia mjadala.Sasa, walichokutana ncho ni mashambulizi makali kutoka kwa wabunge wa CCM na CUF.Mashambulizi hayo kwa kweli yamevuta hisia za wananchi wengi maana kila mbunge anayesimama kuchangia lazima kwanza aanze na vijembe na kisha kutoa uafafanuzi na kujitahidi kuwaelewesha wananchi juu nini kinachoendelea.Sasa hapa ndipo kosa la kiufundi linapojitokeza maana watuhumiwa wako nje ya ukumbi wakiruhusu mashambulizi makali yawaaendee biila ya wao kuwepo na hivyo kujibu mapigo kwa hoja zile zile wanazosimamia. NCCR Mageuzi wamekuwa wajanja ndio maana zaidi ya Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali kuchangia lakini jana pia tulimuona Mheshimiwa Buyogera Mbunge wa Kasulu Vijijij (NCCR-Mageuzi) akipambana. Naamini waheshimwa wa NCCR walishashtuka kuwa kuna kosa la kiufundi lilifanyika siku ya kwanza.Sasa,Kuna hoja kwamba spika alizuia miongozo kwa wabunge.Sawa,inaweza kuwa ni hoja.Lakini siamini kwamba hilo lilikuwa ni tatizo kubwa sana kwani kama ingekuwa ni tatizo,basi hata msemaji wa kambi ya upinzani Mh.Tundu Lisu asingekubali kuwasilisha maoni yao mpaka Spika kwanza akubali kutoa miongozo iliyoombwa kutolewa na wabunge ndipo aendelee na kusoma maoni ya kambi ya upinzani.Lakini ni kwa kutambua kuwa halikuwa tatizo ndio maana alipoitwa na Spika kutoa maoni yao alifanya hivyo. Kwa hiyo,nadhani itakuwa ni busara zaidi kukiri kwamba kweli kilichofanywa na wabunge wa Chadema lilikuwa ni kosa kubwa la kiufundi katika mapambano yanayohitaji uungwaji mkono wa umma. Na wala hamna kuona haya katika hili,kwa kuwa makosa ya kiufundi yapo na huwa yanatokea.Cha msingi ni kujipanga na kusonga mbele! Mungu ibariki Tanzania na watu wake!!
   
 18. ngorope

  ngorope JF-Expert Member

  #18
  Nov 17, 2011
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 1,113
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Waganga njaa utawajua wanajidai wema machoni pa umma kumbe wanapiga kelele ili mafisadi wawaone kuwa wanatetea maslahi yao ili wawakatie kitu kidogo usishangae kusikia Dilunga kapewa u-DC au kanunua kigari kipya kutokana na hii habari yake
   
 19. k

  kada1 Member

  #19
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chadema wanajikaanga kwa mafuta yao wenyewe, hoja za huyu ngugu yangu nimezisoma vizuri sana. Kama umemsikia Lissu anasema anadhani hao mabalozi wa EU na Marekani wanhofia Investment zao" Political Risks" na si kuguswa kwao na mwenendo wa cdm katika hili. Chukueni huo ushauri utawasaidia msiwe rigid tu kwenye misimamo isyo leta matunda. Usidhani mabalozi wamevutiwa na siasa mpaka wa pay attention, hapana wanaona tishio la kukosa busara kwa kuitisha maandamano nchi nzima hivyo kuhatarisha Investments zao. Upo hapo.
   
 20. M

  Meshili Member

  #20
  Nov 17, 2011
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dilunga ana hoja!
   
Loading...