Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,505
- 16,006
Msigwa alishawahi kusema 'huwezi kutatua kosa kwa kutumia akili hiyo hiyo iliyosababisha kosa hilo'....akaendelea 'haiwezekani akili kubwa kutawala akili ndogo'. Akakazia 'wanaomuunga mkono Lowassa wakapimwe akili'.
Katika kampeni za Mwaka jana hoja kuu ya Chadema ilikuwa 'mabadiliko' ati wote walioongoza serikali katika kipindi cha miaka 50 iliyopita waondolewe sababu 'hawajafanya chochote ndani ya miaka 50 ya uongozi wao. Katika kuhakikisha wanaelekea katika mabadiliko hayo sasa wanalazimika kutumia 'akili ileile iliyosababisha matatizo ili kutatuta matatizo yale yale'. Kwa sasa Chadema hawawezi kufanya lolote bila kupata malekezo toka kwa Lowassa na Sumaye. Sasa akili ndogo inatoa ushauri kwa akili kubwa', wanapewa hadi maneno ya kuzungumza bungeni na kwenye mikutano ya siasa. Amri ni moja tu, ole wake mbunge wa chadema atakayezungumza kauli tofauti na maelekezo ya Sumaye na Lowassa...'atakiona cha mtema kuni'.
Ajizi nyumba ya njaa, wabunge wa chadema wamekubali yaishe kuwa Hemedi Alli ndiye mkuu mpya wa idara ya Habari na Propaganda Chadema. Tafsiri yake ni kwamba Tundu,Lema,Sugu na wenzao watalazimika kujifunza mila na tamaduni za chadema kutoka kwa Hemedi Ali. Hemedi Ali alijiunga Chadema tarehe 29.07.2015 siku Lowassa anatambulishwa kwa wanahabari kama Mgombea wa Chadema na baadaye Ukawa. Huyu alikuwa ni mwenyekiti wa 4U Movement. Ole wake Tundu aropoke, atawajibishwa..Msemaji ni mmoja tu Hemedi Ali.Bavicha mpya inakuja, vijana wa 4U,Ulipo Tupo na TeamLowassa kutawala nafasi za uongozi Chadema.
Katika hatua nyingine wabunge wa CUF wametengwa katika mazungumzo yaliyosimamiwa na Lowassa na Sumaye. Sasa ni kama watoto 'yatima', Seif hana habari nao.
Hakika wiki katika siasa ni sawa na mwaka katika maisha mengine, siku zinaenda kasi.