Wabunge 150 wa CCM wajitosa kumuunga mkono Lowassa

Lazima ccm mtajikojolea kama siyo kujinyea kabisa mwaka huu. Lowassa anawazidi nguvu kwa kuitumia misukule mliyoifuga miaka nenda, rudi, akina Komba, maji marefu, chatanda, ntukamazina nk, sijui kama Lusinde alikosekana hapo. Wenye akili ndani ya ccm wanajua kabisa kuwa wakimteua Lowassa watashindwa kwenye uchaguzi kwa sababu ya kinyesi alichojipakaza, ananuka. Lakini kwa sababu siku nyingi ccm imefuga misukule, ambayo mmeitumia kupandia ngazi, kwa kuimba, kukata viuno hadharani na kuloga, sasa misukule hiyohiyo imeanza kuleta madhala kwa chama, inawaangamiza kwa kushabikia bila kufikiri. Mpitishe awe mgombea ndipo matakapojutia upofu wenu.
 
Lowassa auze zile NyumBa zake Zilizoko uingereza na pia afunge akaunti zote za nje aweke hela zake kwenye benki za hapa nchini kisha achukue fomu.
 
Wabunge wamefanya jambo kubwa na la kuungwa mkono nasi sote, wamechukua hatua.....Pamoja na Lowassa Tutavuka tu.
 
...nimesafisha mawani yangu mara kadhaa nikitumai nitafanikiwa kuona 'future' ya CCM. Sina uhakika endap wabunge hawa 150 wa CCM waking'ang'ania msimamo wao bado tutaendelea kuwa na CCM imara.

Acha niendelee kusafisha mawani yangu ya mbao.
 
Profesa Maji Marefu alimhakikishia lowasa uungaji mkono wa waganga wa kienyezi kama ifuatavyo: nanukuu

“Nasema bila kificho mimi ni mganga wa tiba asilia ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa waganga wote nchini, sisi tutahakikisha tunakuunga mkono ndugu yetu lakini utuhakikishie kama utagombea urais,” alisema Ngonyani.
 
Hadi Chatanda!!! Nimeamini MaCCM yamekaa kimaslahi, yameangalia wapi kumenona yote yamehamia huko. Ndugu yangu La Mdimu ndio basi tena jiandae tu kuwa mkurugenzi wa Hotel ya hela za Ghadaffi
 
Raisi ajae ni Lowasa.

Tumeyachoka majambazi. Mapacha watatu (rostamu Lowasa na kikwete) walijitengenezea kampuni feki isiyo na fedha wala ofisi wala anuani wala utaalamu wala mitambo na walikuwa wakiliibia taifa Tsh.152 mil kila siku. Piga hesabu mwenyewe kwa mwezi na kwa mwaka. Bahati mbaya sn watz ni wagumu kuelewa na wepesi kusahau
 
Katika magazeti ya leo story kubwa ni wabunge kumuunga mkono Lowassa eti watu kama Komba, Chatanda, Ntukamazina wote wamefunguka.

Binafsi mradi huu niliutarajia sema ulichelewa, kinachooudhi ni magazeti yetu kutofanya utafiti kidogo kujua huu ni mradi wa watu.

Kwa hivi sasa hakuna weledi, tunatumikia wenye fedha kuanzia viongozi hadi wataalamu wapo mifukoni mwa wenye fedha ambazo hatukuwahi kujua wamezitoa wapi.

Mtatufanya tusome mitandao maana huku watu wanahoji, wanauliza wanatia mashaka.Eti mtu anafaa kuwa rais kwa sababu aliposhuka kwenye gari alishangiliwa?

NCHI HII BADO SANA.


Chanzo:Mtanzania
Magazeti yetu mengi ni vinywa vya wanasiasa; hayafanyi utafiti hata kidogo kwa kile wanachoambiwa.
 
Wabunge hawa njaa wameshachukua mgao wao "rushwa" kutoka kwa fisadi. Hiki ni kipindi ambacho wenyewe hukiita "kipindi cha neema" ambapo Wabunge hawa wa MACCM ambao maisha yote hawajali maslahi ya Tanzania na Watanzania hufikiria namna ya kutajirika kwa kupokea rushwa toka kwa wagombea mbali mbali wa Urais kwa ahadi za kuwapitisha wawe wagombea wa chama chao cha wahuni na mafisadi.
 
Lowassa auze zile NyumBa zake Zilizoko uingereza na pia afunge akaunti zote za nje aweke hela zake kwenye benki za hapa nchini kisha achukue fomu.
Maji Marefu
Kwa upande wake Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani (CCM) alimwelezea Lowassa kuwa ni binadamu mwenye upendo wa hali ya juu.

Ngonyani maarufu kama ‘Profesa Maji Marefu' alisema yuko tayari kufukuzwa CCM lakini hatoacha kusema ukweli wake wa kile anachokiamini kuhusu Lowassa.

"Huyu mzee mbali ya uwezo mkubwa wa kufanyakazi lakini ana huruma… katika hili nipo tayari kufukuzwa CCM kwa msimamo wangu wa kusema ukweli juu ya kumuunga mkono Lowassa.

"Nasema bila kificho mimi ni mganga wa tiba asilia ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa waganga wote nchini,
sisi tutahakikisha tunakuunga mkono ndugu yetu lakini utuhakikishie kama utagombea urais," alisema Ngonyani.

Alisema kitendo cha kumwona Mbunge wa Viti Maalumu, Marry Chatanda katika hafla hiyo ya chakula cha jioni ni ishara ya kudhihirisha kukubalika kwa waziri mkuu huyo wa zamani.

"Nilipoingia kumwona huyu Chatanda yuko hapa! Haa!! Basi…," alisema Ngonyani.

Hivi Lowasa ni ndugu na Waganga wa kienyeji??
Prof Maji Marefu aliwahi kusema kuwa Prof Muhongo ni mwenzake na kumusifia kama anavyofanya kwa Lowassa
Sijui Kama anayosema yanatoka Moyoni au ni baada ya kupata Mgao

Kama yeye ni mwenyekiti wa Tiba asilia kwa nini hasadii kufichgua wauaji wa Albino??
 
Cheap politics, mtu km Komba hata akiongea point unaona km ni pointless maana yy mwenyewe hajitambui.
mpk hao wanaoshangilia wanakuwa wameshaandaliwa na wamelipwa 5000, hawazidi watu10. Hapo kunakuwa pia na waandishi uchwara wa magazeti uchwara ndio wansosambaza hizo habari.

HIVI NI KWELI tumesha onekana kuwa ni majuha mpaka akina Komba, Maji Marefu na wenzao kutusaidia kumtambua kiongozi mzuri wa nchi hii.
 
HIVI NI KWELI tumesha onekana kuwa ni majuha mpaka akina Komba, Maji Marefu na wenzao kutusaidia kumtambua kiongozi mzuri wa nchi hii.

Sio kweli mkuu afwe, Tanzania ina kundi kubwa sana la watu wajinga na wasiojitambua. Kundi hili linawafaidisha sana wanasiasa kwa kuwadanganya watakavyo.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom