Wabongo waishio majuu kwa sifa!!?


Andika kiswahili, kuna mwingereza nimempa atafsiri kachemka.
 



Ni kweli kabisa na mfano ulio hai ni huyu kijana wetu Hasheem Thabeet. Jamaa licha ya kuwa a bust in the NBA ila anajifanya sana kama vile hajuwi lugha wakati alipokwenda Marekani some years back hata kiingereza alikuwa hajuwi ila sasa anajifanya kasahau kiswahili na wakati hata hicho kiingereza akizungumza utafikiri alikwenda Marekani jana kwa lafudhi ya hajabu ila hapa Bongo watu hawatambui hivyo kwa sababu wengi wao hawajuwi lugha. Watanzania wengi wako feki.
 
Basi ukibahatika kukutananae huyo jamaa (binafsi sijawahi) huko marekani akiwa na wabongo wenzake wanaongea full kiswahili
 

Na wewe uko feki? Na wewe hujui Kiswahili? Mbona umechanganya na Kiingereza hapo?
 
Eti utamsikia aloyyerudi kutoka majuu " yaani africa kunabore sana too much joto i real cant survive here, deeem...."
 
kuchanganya lugha wote sio mpaka hatoke nje.mbona nilienda mtwara wamakonde wanachanganya kimakonde na kiswahili
 

[video=youtube_share;87bx32P2K5A]http://youtu.be/87bx32P2K5A[/video]
 

Acha insecurity ya kishamba na wivu na chuki. Sikia, ukizoea lugha Fulani maneno yanakuwa karibu zaidi hususan ukiwa katika maeneo "formal" ama ukiongea na mtu ambaye unconsciously your mind can tell you having a formal conversation. Tujidai na lugha ya Watu ili tupate nini while our need is to communicate with the our loved ones?
 

hii ni code mixing au code switching??
 
Ukiongea Kinyamwezi kile cha ndani cha Sikonge, hadi RAHA. Enzi hizo nikirudi nyumbani, nikilala Tabora mjini, asubuhi yake nafungulia dirisha ili nikipate chenyewe kabisa cha ndani ndani kule Mibono na Usunga kama Siyo Chabutwa au Tutuo na baadaye unajisukuma Mole, mitaa ya akina TUKUTUKU 🙂

Hao wanaojifanya wamesahau Kinyamwezi ahhh Kiswahili, huwa ni Wachovu fulani ambao Box limegoma kabisa kupanda.
 
Last edited by a moderator:
Jamaa_Mbishi mi mwenyewe swahili yangu mbofu mbofu siishi kukosolewa hapa..Ukiishi muda mrefu nje ya nchi haswa kama ukienda utotoni unasahau au kuchanganya baadhi ya maneno!!!au mfano naweza nijieleze lakini nafikia sehemu naganda sipati njia ya kujieleza kwa kiswahili kwa ufasaha au nakosa maneno ya kuyatumia kujieleza inabidi nitumie kiingereza!!
 
Hiki nacho ni kinini?ngoja niende google translate!
 
mim pia iko sahau sahau hii swahili kwetu Mamen. mimekaa huku mirekani miaka selathini. sasa inategemea mim ntaongea faken swahili vunjavunja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…