Wababa wanalalamika sana kutengwa na watoto wao kimawasliano hata kiuchumi. Je, shida ni nini? Wamama mnaliongeleaje hili? Watoto mnafanya haya kweli?

Mimi niwaombe wababa wabebe nafasi zao kwenye kutusimamia sisi wanafamilia, tena wawe wakali kidogo hapa kama mama wa taifa alivyokua mkali kwa chalamila alipoona anaharibu familia ya mwanza

Mkisema mtuachie wamama tufanye tutakavyo tutaharibu tuu...... hata Mungu anajua ndio maana aliwapa nyie mamlaka ya kuwa kichwa ili mtoe malekezo ya wapi tunaelekea kwetu
Tatizo sio kubeba nafasi zetu. Wamama wanajua ku manipulate akili za watoto sana akipata ata kaupenyo kidogo jua umepigwa
 
Mjadala huu nimeukuta kwa wazee wa Kagera. Siku hizi hawatoi mashamba makubwa yenye migomba mizuri badala yake kijana anapewa eneo la kujenga nyumba na choo halafu mzee anabaki na eneo kubwa. Akizeeka anatangaza kuuza sehemu ya shamba lake basi kijana anaanza kujisogeza karibu na mzee ndo anaanza kutoa masharti.....kilo moja ya nyama kila wiki, sukari kila wiki n.k halafu anamhesabia miguu kadhaa ya shamba. Kwa mfumo huu wazee wanakula vuzuri tofauti na zamani kijana anapewa shamba kubwa anavuna utajiri halafu yeye na mke wake wanawatelekeza wazazi.
Mwanaume lazima uwe na akili kuzid hawa viumbe katika vitabu vitakatifu wanasema tuishi nao kwa akili wanapokuwa mabinti hadi wakizeeka sasa ukimpa akili akushikie atakuonyesha kweli ye ni nani.
 
Mm ninae best yangu 68 yrs ni male anae watoto 6 wa mwisho ndio nalingana nae mm

But anaweza kaa hata 10months hakuna mtoto wake anaempigia simu wala kumuuliza chochote na yy tupo nae hapa kijijini wala hawazi

Anaishia tu kulalamika kuwa watoto hawamjali wala nn wakimtumia pesa mingi sana ni 15k na hata wakija home anaambulia kupewa chupa ya konyag kubwa tu

Watoto wa kuiume jua mnayowafanyia baba zenu sasa hiv,ndio mtakayofanyiwa na nyie mtakapozeeka

What goes around comes around
Huyo mzee aliwalea vipi hao watoto?
 
Hata kama aliwalea vibaya,huwezi lipa ubaya kwa mzazi wako

Hata wazazi wa kike nao wanayo mapungufu ila ya baba ndio wanaona kuwa hayawezi kusameheka sababu ni baba

Hata kama aliwalea vibaya,huwezi lipa ubaya kwa mzazi wako

Hata wazazi wa kike nao wanayo mapungufu ila ya baba ndio wanaona kuwa hayawezi kusameheka sababu ni baba
We jibu swali uliloulizwa. Hayo mambo ya kufikirika achana nayo.
 
Ukweli unaouma!!!!
Kwanini hii ni zaidi kwa wababa kiafrika na sio Asia au Europe?
Ni kwasababu ya mentality, tamaduni zetu na gender roles zilivyogawanywa.Inabidi kubadilishe jinsi tunavyolea watoto,yale majukumu ambayo yalikuwa ya mama tu inabidi baba achangie pia katika makuzi ya mtoto kama kubadili diaper,kulisha,kuogesha,kuhudumia akiwa mgonjwa n.k
 
kwa kifupi usitegemee furaha yako itoke kwa mwanadamu ukifanya hivyo utajuta,ukitegemea watoto waje wakupe furaha nadhani utaishia kuwalaumu sana na hata kuwaingilia kwenye mambo yao ,hao wamama wanaopendana na watoto wao ndio chanzo kikuu leo hii ndoa nyingi kuvunjika utasikia " akikusumbua rudi nyumbani tu achana nae" au " kwani mwanamke yupo peke yake" ila wababa ni mara chache sana kusikia wanahusiswa na migogoro ya ndoa za watoto wao mara nyingi hukuta mama ndie anaeshitakiwa. Pia sishauri sana mtoto kuwa mtoto wa mama kila kitu mama pia wajaribu kumkumbuka baba katika mambo ya hapa na pale.
 
Mwanaume tafuta pesa kwa bidii, wape watoto elimu bora, wape mahitaji yao muhimu, jenga nyumba nzuri waishi vizuri, lakini ukizeeka don't expect too much from them. Enjoy maisha ya uzee kwa pesa zako mwenyewe ulizochuma ujanani.
 
Kumekua na malalamiko mengi kwenye jamii za kitanzania na kiafrika kwa ujumla mara watoto wanapokua na kuanza kujitegemea na umri wa wazazi kusogea, wototo huwa wanakua karibu na mama zao zaidi ya baba zao.

Wababa wengi huumizwa na jambo hili na kujiona kutengwa na watoto wao baada ya watoto hao kupata mafanikio huku wakiamini kabiasa kwamba wake zao (wamama wa hao watoto) wanawafurahia hilo jambo na wana ushirika mkubwa na watoto wao katika kuwatenga

Wamama huwa tunakosea wapi hadi hawa wababa wafikie kulalamika kiasi hiki? Au umri ukienda mapenzi yanaisha na title ya mume inabadilika?

Nini kinawapelekea watoto kuwa na hii distance kubwa kwa baba zao? Je, wanajua kama na wao siku wakizeeka wakatengwa au kuhisi kutengwa itawaumiza?


Ikumbukwe hakuna mtoto wa mzazi mmoja, katika mazingira yoyote yale mtoto atabaki kuwa wa baba na mama unless huyo baba au mama amkatae mtoto

Kwenye imani zetu pia tumeamrishwa kuwaheshimu baba na mama. Hiyo ni amri bila maswali, kazi ni moja tuu kutekeleza. Yaani huwezi sema sababu mama yuko hivi au baba yuko vile sitamheshimu! Matakwa ya amri ni kutekeleza tuu

Familia ni upendo na familia ndio faraja na kimbilio la wakati raha na taabu. Tudumishe upendo

Cc Bushmamy mirisho pm Asprin Sky Eclat 50thebe wahenga wenzangu wote
Wamama wengi hutumia muda mwingi na rasilimali zao kufanya uchochezi kwa watoto dhidi ya baba yao.

Watoto hupandikizwa chuki hasa wanapokuwa vijana wa kuanzia miaka kumi na kuendelea na kwa vile uwezo wao wa kudadavua mambo huwa bado mdogo huamini kile wanacholishwa na mama zao. Pili mtoto akikosa mama hukwepa kumuadhibu na humchongea mtoto kisirisiri kwa baba ili aadhibiwe kwa lengo la kumrekebisha na baba anatekekeza wajibu huo ambapo kama sio mama kuona kosa na kulisema baba asingejua wala kuadhibu. Adhabu hizo nazo huchangia baba kuchukiwa.

Tatu, wamama wengi hugoma kuchangia uendeshaji wa gharana za familia na kumuachia baba, kwa kuwa kipato cha baba ni kidogo wakati mwingine standard ya chakula au huduma zingine huwa za kiwango cha chini, hapo ndipo mama anapojifanya anawapenda na kuwajali watoto kwa kujitokeza na kutumia hela yake ambayo haitumiki katika bajeti kuu ya familia mfano siku hiyo inaweza kuwa imepikwa maharage lakini mama ananunua soseji na matunda au kuku na kuwaletea watoto, au mama kwa kuwa ana hela anawanunulia wanaye simu za bei mbaya. Kumbuka shule za boarding zote zinakataza simu lakini watoto huwa wanakamatwa na simu na mnunuzi wa hizo simu siku zote huwa ni mama.

Njia mojawapo ya kupunguza hili tatizo ni kuhakikisha pesa ya mama nayo inatumika katija bajeti kuu ya familia ili kupunguza pesa anayobaki nayo ambayo ndiyo anayoutumia kuwarubuni kuwa anawapenda zaidi kwa kuwanunulia vitu ambavyo baba hawezi au kumaadili anaona vitawapoteza watoto.

Lingine, inawezekana hawa wababa wanaolia leo kuhusu watoto wao nao waliwafanyia hivyo hivyo baba zao na sasa wanalipia maovu yao maana biblia iko wazi kuhusu hili: ukimheshimu mzazi wako na wewe utawafurahia watoto wako kinyume chake sahau.
 
Kumekua na malalamiko mengi kwenye jamii za kitanzania na kiafrika kwa ujumla mara watoto wanapokua na kuanza kujitegemea na umri wa wazazi kusogea, wototo huwa wanakua karibu na mama zao zaidi ya baba zao.



Cc Bushmamy mirisho pm Asprin Sky Eclat 50thebe wahenga wenzangu wote
Hapa kuna mambo mengi sana ya kuangalia

1.bond kati ya mtoto na mama ni kubwa sana kwa sababu ya shughuli za malezi ambazo kwa kiasi kukubwa zinafanywa na mama, mfano kuanzia kumuogesha mtoto, kumlisha, kuwapeleka shuleni na kuwasimamia homework jioni, wakati mwingine watoto mpaka wanalala baba hajarudi nyumbani

2.huu ukaribu wa mama na mtoto unamfanya mtoto anakua huru kueleza shida yake au mahitaji yake kwa mama, wakati mwingine baba ameacha pesa ya matumizi lakini mtekelezaji ni mama, mtoto yeye hajui kama pesa imaechwa na baba bali anajua my mom does everything for me, ndio pale unasikia mama anapambana ili tupate kila tunachokitaka

3.katika makuzi ya mtoto, baba muda mwingi yupo busy anatafuta, mama yeye anacheza na watoto, na kuwafundisha hata baadhi ya kazi na maisha ya kila siku, mtoto anapoumwa mama yeye yupo bega kwa bega, hii inatengeneza attachment kubwa kati ya mtoto na mama, mindset ya mtoto inakua ikitambua kwamba mama was always there for me

Kitu ambaco hawa baba zetu, au waume zetu hawatambui, ni kwamba mtoto anahitaji sana muda wa mzazi kuliko kitu chochote

Tunajua mpo busy kutafuta kwa ajili ya familia zenu, lakini mjitahidi mtenge muda wa kukaa na watoto na kuwafundisha mawili matatu, wakati mwingine hata kuwafanyia mambo madogo madogo kama kuwalisha/kuwaogesha, kufanya nao homework au kazi za hapa na pale once in a while, hii itasaidia kujenga bond kati ya watoto na baba zao
 
Katika harakati nzima ya kulea mama ndio anabeba jukumu kubwa kuliko baba kwa tamaduni za kiafrika hasa kitanzania. Baba yeye analeta mkate yaani anashughulika kuhudumia familia financially lakini yaliyobakia mama anayatendea haki.So kama jukumu kubwa la malezi anabeba mama mtoto atakuwa karibu na mama kuliko baba.Hata mtoto akiwa na shida yoyote anaenda kwa mama kwasababu hakuna ukaribu,urafiki wala mazoea na baba tena unakuta mtoto anamuogopa hata baba kwasababu anatumika kama chombo cha kuadhibia.Kwa kusema hivo kunakuwa hakuna connection yoyote ya baba zaidi ya genetics na finances which is horrible.Kulea ni zaidi ya huduma ya kifedha na kutoa nidham.
Siku hizi ni 50-50, baba na mama wote wanatoka alfajiri wanarudi magharibi. Jukumu la kukaa na watoto tumewaachia housemaids hivyo hakuna tena sababu ya baba kuchukiwa na watoto, unless awe kauzu.
 
Mimi nafikiri kitu kikubwa ni wazazi was kiume kuangalia familia lakini wasisahau kujiwekee aset zao Ili kama watoto watamtenga aset yake iweze kumsaidia maana unaweza kujali wanao lakini wasikujali ukiwa mtu mzima

Sent from my ONEPLUS A3003 using JamiiForums mobile app
 
Siku hizi ni 50-50, baba na mama wote wanatoka alfajiri wanarudi magharibi. Jukumu la kukaa na watoto tumewaachia housemaids hivyo hakuna tena sababu ya baba kuchukiwa na watoto, unless awe kauzu.
Unajizungumzia wewe au jamii nzima?Hata kama watu wanafanya kazi 50-50 bado wanatakiwa kusaidiana majukumu wakiwa nyumbani ya malezi so haibadilishi fact ya kwamba wababa waliowengi wanakitoka kazini wanaishia bar au wanakojua wao na mama ndo anabeba mzigo wa ulezi!
 
Mtoto kalelewa na dada wa kazi na movie za Mnet series ataanzaje kumpenda baba yake uzeeni wakati amefunzwa na movie
 
Mtoto kalelewa na dada wa kazi na movie za Mnet series ataanzaje kumpenda baba yake uzeeni wakati amefunzwa na movie

Hata waliolelewa bila dada wa kazi na movie wanafanya hayohayo
 
Back
Top Bottom