Wababa wanalalamika sana kutengwa na watoto wao kimawasliano hata kiuchumi. Je, shida ni nini? Wamama mnaliongeleaje hili? Watoto mnafanya haya kweli?

Wewe sindio unawaharibugi machalii unampondea mshua! Af sahizi unajidai hujui nini sababu 😅😅😅 unawachonganisha madogo na mzee kwa kujidai we unaonewaga sana
Muone sura yake😅😅😅
Hebu acha masihara huko
 
Kumekua na malalamiko mengi kwenye jamii za kitanzania na kiafrika kwa ujumla mara watoto wanapokua na kuanza kujitegemea na umri wa wazazi kusogea, wototo huwa wanakua karibu na mama zao zaidi ya baba zao.
vitu viwili ikubwa
1, Kkwanza ni tabia ya mtot mwenyewe sio kwamba mama anamlisha sumu sijui itu gani kama mtoto mwenyewe hana upendo wa dhati na mzee wake na hana heshima basi huyo sahau maana kwa watoto wa kiume walio wengi unakuta akishapata kifamilia basi anajijua yeye anamshau mzee . HII mambo ya sumu mtu mzima anajitambua anajua hapa ni ukweli au uongo.

2.Wazee wengi sana wamekua na tabia ya kutelekeza watoto unakuta mzee ana za na mwanamke baadae wakitengana mzee anajiuvua majukumu kwa chuki aliyonayo juu ya mke wake matokeo yake mama ndio anahangaika na mtoto kuanzia maisha ya chini mpaka pale anapofanikiwa sasa akisha fanikiwa mzee anajisogeza na kuanza kulia mwanangu . Sasa kwa mtot wa kiume inakua ngumu we mzee ulika wapi kumsiadia mtu alikua anahangaika na uwezo mzee anakua nao unakuta kaoa au anafanya ulevi sasa mtu keshahangaika huko afu unamjua siku za raha mtu hakuelewi.

Mfano
kua mzee mmoja huku kwetu alikua hakimu kipindi hiko hakimu mtaai anaheshimika sasa pamoja na pesa na uhakimu wake kapata mwanamke kaoa kasahau mke mbaya zaidi hadi wattoto kasahau kusomesha yule mama kasomesha wale watoto kwa kupika gongo na kusaidiwa na majirani huku watoto wakikua wakimuona baba yao mzazi anakula raha na hata wakienda kumuomba anawaambia mimi nina familia yangu mwambieni mama yenu . Bbasi mungu si athumani hawa watoto wakasoma waka maliza wengine wakawa wafanyakazi wengine wafanya biashara. mwisho wa siku mzee kastaafu sasa anaanza kulia mimi wanangu hawanijui huku akisahau yeye aliwaacha wakiwa na shida
 
Mimi niwaombe wababa wabebe nafasi zao kwenye kutusimamia sisi wanafamilia, tena wawe wakali kidogo hapa kama mama wa taifa alivyokua mkali kwa chalamila alipoona anaharibu familia ya mwanza

Mkisema mtuachie wamama tufanye tutakavyo tutaharibu tuu...... hata Mungu anajua ndio maana aliwapa nyie mamlaka ya kuwa kichwa ili mtoe malekezo ya wapi tunaelekea kwetu
😁 Ahsante kwa kulijua hili.
 
Mm ninae best yangu 68 yrs ni male anae watoto 6 wa mwisho ndio nalingana nae mm

But anaweza kaa hata 10months hakuna mtoto wake anaempigia simu wala kumuuliza chochote na yy tupo nae hapa kijijini wala hawazi

Anaishia tu kulalamika kuwa watoto hawamjali wala nn wakimtumia pesa mingi sana ni 15k na hata wakija home anaambulia kupewa chupa ya konyag kubwa tu

Watoto wa kuiume jua mnayowafanyia baba zenu sasa hiv,ndio mtakayofanyiwa na nyie mtakapozeeka

What goes around comes around

Sad😥😥
Hata asipolalamika baba Mungu atamlalamikia
 
Unaousema n ukwel mkuu

Ila wababa tuache kulea watoto kikauzu badala yake tubadirike hasa wakat huu ambao ulimwengu unaenda kasi unalea mtoto kwa mifumo ya miaka 1980 wakat dunia inehama huko

Mtoto anakupigia simu anataka kujua nyumban mnaendeleaje wewe unajibu kifupi na hauoneshi kufurah kuwa mtoto kakupigia

Ila ukimpigia mama anaonesha furaha anakueleza mambo muhimu kuhusu nyumban

Unategemea mtoto atampenda au atampigia Nani simu kila wakat pale anapohtaj kujua Jambo fulani

.....wazazi hasa wakiume tubadilike....

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Mtoto ana natural bond na mama hata uwe how nice
 
Mm ninae best yangu 68 yrs ni male anae watoto 6 wa mwisho ndio nalingana nae mm

But anaweza kaa hata 10months hakuna mtoto wake anaempigia simu wala kumuuliza chochote na yy tupo nae hapa kijijini wala hawazi

Anaishia tu kulalamika kuwa watoto hawamjali wala nn wakimtumia pesa mingi sana ni 15k na hata wakija home anaambulia kupewa chupa ya konyag kubwa tu

Watoto wa kuiume jua mnayowafanyia baba zenu sasa hiv,ndio mtakayofanyiwa na nyie mtakapozeeka

What goes around comes around
Waache waone raha ila wakizeeka inakuja pale pale kichapo tu
 
Nafikiri kuna thread yangu niliileta humu wababa wengi wanasababisha haya wao wenywewe,nina mifano iliyo hai kabisa baba anahudumia nyumba ndogo au michepuko zsidi kuliko familia mpaka watoto wapo vyuo, wanajitambua mzee haoni km ni shida ,anaehangaika zsidi na watoto ni mama, mzee akustaafu robo tatu ya hela anatumia na michepuko huku familia inaona na inapata shida then watoto wskipata kazi baba anakuwa na lawama kibao.
 
Nafikiri kuna thread yangu niliileta humu wababa wengi wanasababisha haya wao wenywewe,nina mifano iliyo hai kabisa baba anahudumia nyumba ndogo au michepuko zsidi kuliko familia mpaka watoto wapo vyuo ,wanajitambua mzee haoni km ni shida ,anaehangaika zsidi na watoto ni mama ,mzee akustaafu robo tatu ya hela anatumia na michepuko huku familia inaona na inapata shida then watoto wskipata kazi baba anakuwa na lawama kibao
Hahahhahahaha mzee anakuwa amejitaftia balaa
 
Unfortunately hii inatoke solely kwa African Fathers

Ni kosa entirely kwa African Fathers as a group,kuna pahali turekebishe!

Dictatorship does not work,more love and understanding works better

Ni kweli kabisa hili ni la kiafrika zaidi
Wababa wa sasa na wababa tarajiwa hii comment ya Wyatt Mathewson inawahusu sana

Wamama tusiache kuwasaidia hawa wababa kwa kuwakumbusha kuwa na upendo na ukaribu kwa watoto wetu, na pia tusiache kuwaambia watoto ukweli na umuhimu wa upendo sawa kwa sisi na baba zao
 
Wazazi wanaohisi kutengwa na watoto wao wa kuwazaa, si kwamba inatokea bahati mbaya HAPANA. Ukifuatilia kwa karibu historia ya kizazi chao utagundua kwamba na hawa wanaolalamika waliwaacha wazee/wazazi wao kama wao walivyoachwa.hivyo ule mnyororo bado unaendelea kwenye kizazi kingine.
 
Kiukweli upo sahihi kabisa hata mimi mpaka leo hii nipo zaidi karibu na mama kuliki baba
 
Katika hili wababa tubadilike kimalezi na kimahusiano na watoto wetu;

• Usipende kupewa makosa ya watoto na kuyafanyia kazi wakati hukuwepo makosa yakitendeka. Mama awajibike kuwafundisha watoto kama baba hayupo.

• Baba ukirudi nyumbani jaribu kuwa karibu na watoto wako, waonyeshe upendo na wafundishe, usipende kuwa kauzu kila wakati.

• Toa adhabu kulingana na kosa la mtoto, toa adhabu kwa upendo na ukimaliza kumpa adhabu endelea kuonyesha upendo.

• Usikubali hata kidogo mke aonekane yeye ndio kila kitu ndani, wamama wanapenda sana hii kitu, provider wa kila kitu hata kama baba ndio katoa.

• Watoe watoto for evening walks na hata weekends, let them feel dad's presence yani, wapeleke shopping pia ili wajue kuwa baba is providing for them.

Otherwise utatoa pesa, utatunza nyumba, utajenga mijumba but mama ataonekana kila kitu, wewe kituko tu.
 
Back
Top Bottom