Wababa wanalalamika sana kutengwa na watoto wao kimawasliano hata kiuchumi. Je, shida ni nini? Wamama mnaliongeleaje hili? Watoto mnafanya haya kweli?

Wazazi wanaohisi kutengwa na watoto wao wa kuwazaa, si kwamba inatokea bahati mbaya HAPANA. Ukifuatilia kwa karibu historia ya kizazi chao utagundua kwamba na hawa wanaolalamika waliwaacha wazee/wazazi wao kama wao walivyoachwa.hivyo ule mnyororo bado unaendelea kwenye kizazi kingine.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app

Umeongea ukweli Banjuka, lakini sasa huoni kama baba yako alimtenga mzee wake. Na wewe ukamtenga yeye unaacha nafasi ya mtoto wako kutengwa na watoto wake?

Tuvunje hii chain ya laana kwa kusambaza upendo basi
 
Katika hili wababa tubadilike kimalezi na kimahusiano na watoto wetu;

• Usipende kupewa makosa ya watoto na kuyafanyia kazi wakati hukuwepo makosa yakitendeka. Mama awajibike kuwafundisha watoto kama baba hayupo.

• Baba ukirudi nyumbani jaribu kuwa karibu na watoto wako, waonyeshe upendo na wafundishe, usipende kuwa kauzu kila wakati.

• Toa adhabu kulingana na kosa la mtoto, toa adhabu kwa upendo na ukimaliza kumpa adhabu endelea kuonyesha upendo.

• Usikubali hata kidogo mke aonekane yeye ndio kila kitu ndani, wamama wanapenda sana hii kitu, provider wa kila kitu hata kama baba ndio katoa.

• Watoe watoto for evening walks na hata weekends, let them feel dad's presence yani, wapeleke shopping pia ili wajue kuwa baba is providing for them.

Otherwise utatoa pesa, utatunza nyumba, utajenga mijumba but mama ataonekana kila kitu, wewe kituko tu.

Kweli baba akifanya yote haya watoto wake watampenda sana maana atakua karibu nao na atakua rafiki kwao.

Hivi kuna uwezekano wa kibao kugeuka na mama kutengwa hapo?

Maana wamama wengine wakaliiiii kazikazi.... hadi watoto wanatamani tusafiri ili wakule bata na baba zao

🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Kina baba tuache kutegemea zawadi au huduma kwa asilimia kubwa kutoka kwa watoto. Lawama hizi zinakuja kwasababu kinababa wanahangaika ujana wao wote kulisha familia na kutoweza kabisa kwa ajili yao baadae.

Ila kama ukiwekeza huyo mtoto na mama yake watakua na wewe mpaka unafariki, umaskini ni janga jama tuukatae hasa sisi wanaume.

Mwanaume usilee ukategemea eti huyo mtoto atakuja kukulea na wewe uzeeni, aisee we lea tu kama wajibu lakini sio kutegemea malipo baadae.
 
Umeongea ukweli Banjuka, lakini sasa huoni kama baba yako alimtenga mzee wake. Na wewe ukamtenga yeye unaacha nafasi ya mtoto wako kutengwa na watoto wake?

Tuvunje hii chain ya laana kwa kusambaza upendo basi
Hawa watoto hata wakati mwingine wanaweza wasiweze kuwa na majibu ya kutosha kwanini hawapo karibu na baba zao, yaan wanajikuta tu hawana huo ukaribu, kumbe ni ule mnyororo unafanya kazi yake.
 
Kweli baba akifanya yote haya watoto wake watampenda sana maana atakua karibu nao na atakua rafiki kwao.

Hivi kuna uwezekano wa kibao kugeuka na mama kutengwa hapo??

Maana wamama wengine wakaliiiii kazikazi.... hadi watoto wanatamani tusafiri ili wakule bata na baba zao

Hatufanyi hivi ili kumtenga mama, tunafanya ili kupunguza hili tatizo la baba kuonekana sio lolote ndani ya nyumba.
 
Unaousema n ukwel mkuu

Ila wababa tuache kulea watoto kikauzu badala yake tubadirike hasa wakat huu ambao ulimwengu unaenda kasi unalea mtoto kwa mifumo ya miaka 1980 wakat dunia inehama huko

Mtoto anakupigia simu anataka kujua nyumban mnaendeleaje wewe unajibu kifupi na hauoneshi kufurah kuwa mtoto kakupigia

Ila ukimpigia mama anaonesha furaha anakueleza mambo muhimu kuhusu nyumban

Unategemea mtoto atampenda au atampigia Nani simu kila wakat pale anapohtaj kujua Jambo fulani

.....wazazi hasa wakiume tubadilike....

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Binafsi naona kuna cases nyingi katika hili.

Binafsi sikulelewa na baba, nimekuwa nikiwa simjui. Nimekuja kufahamiana naye baada ya kuhitimu kidato cha sita. Kwahiyo sina bond yoyote na baba.

Ila nilipokutana naye nilijihisi kusamehe tu ili maisha yaendelee, nikiamini sasa atachukua majukumu yake kama baba kumbe hana hata huo muda.

Hii ni special case kwangu na kwa wengine wenye case kama yangu na wale waliotelekezwa.

Ila pia, mimi ni mtoto wa kiume naona, ukiachana na kina baba makatili kwa watoto, wapo wanajitahidi sana kujali familia zao.

Tatizo huwa linaanzia kwenye kuweka duscipline ya watoto, mara nyingi hapa ndio kina mama huwa wanakaa pembeni ili kukwepa lawama.

1- Mtoto akienda kucheza akachelewa kurudi nyumbani, baba anampa adhabu au sometimes anamwambia hakuna kula. Tena mnakubaliana vizuri na mama yake, kumbe mama yake kaficha chakula huko jikoni anampatia baadaye baba hajui.
Mtoto anakuwa akijua baba ndio mbaya.

2- Mtoto kumwomba baba pesa kidogo labda nauli ya shule, baba akasema hana. Mama anatoa anampa mtoto huku akimlaumu baba.

Katika mazingira ya hivi, ni rahisi kwa mtoto kuwa na bond kubwa sana kwa mama kuliko mama. Na bond hii huwa ni kubwa mpaka kwa ndugu wa mama.

Mara nyingi undugu wa upande wa mama ndio huwa una nguvu sana kuliko upande wa baba.

Mimi nina Anko wangu, hata akiwaomba wanaye elfu 10 lazima wampigie simu mama yao kwanza. Bila ya mama kutoa go-head anaambulia patupu.
 
Mwanamke by nature ni mbinafsi na mwenye moyo uliojaa tamaa, jambo la msingi wanaume ili tusidharaurike uzeeni ni kuweka assets binafsi zitakazo kupa heshima hata mzeeni mwako pasipo tegemea watoto hata mkeo alikukuacha na kwenda kwa watoto wake anauwezo hata kusogeza mke mdogo akakupa furaha
 
Hili ni la msingi sana, baba jijenge bila kufikiria uzeeni nani atakuangalia au kukutunza, weka assets za kutosha ili usiaibike uzeeni. Lakini wapende watoto wako coz hata wewe una deserve kupendwa hasa uzeeni. Ukionyesha roho mbaya na ukauzu, uzee wako unaweza kuwa wa taabu na dhiki kuu.
 
Wababa lakini si mnaweza kutuzuia kufika huku?
Mmeshindikana mama D. Wanaopika ndo ninyi, mnapakua wenyewe na watoto huku mkiwabembeleza 'kula junia' mwisho wa siku mama amenona, junior shavu hilo, baba suruali linamlegea.
 
Mwanamke by nature ni mbinafsi na mwenye moyo uliojaa tamaa, jambo la msingi wanaume ili tusidharaurike uzeeni ni kuweka assets binafsi zitakazo kupa heshima hata mzeeni mwako pasipo tegemea watoto hata mkeo alikukuacha na kwenda kwa watoto wake anauwezo hata kusogeza mke mdogo akakupa furaha

Na huyo mke mdogo wa kukupa furaha yeye hatokuwa na watoto?
Cha msingi ni kuishi kwa akili kama baba. Hakikisha nidhamu ya familia yako kuanzia kwa msaidizi hadi watoto, na pia hakikisha unasambaza upendo kwao wamjue Mungu kwanza kisha wajue nafasi na baraka zao kupitia familia yenu
Hili ni la msingi sana, baba jijenge bila kufikiria uzeeni nani atakuangalia au kukutunza, weka assets za kutosha ili usiaibike uzeeni. Lakini wapende watoto wako coz hata wewe una deserve kupendwa hasa uzeeni. Ukionyesha roho mbaya na ukauzu, uzee wako unaweza kuwa wa taabu na dhiki kuu.

Hilo la kutafuta mali nakubaliana nalo 100% ila la kutafuta furaha kwa mke mdogo ni kamari🤣🤣
 
Mimi binafsi hayo yalinikuta kumpenda mama pekee na kumuona baba kama sio mtu wa karibu kwangu pale nilipo pata ajira nakuanza kushika pesa, kutokana na kwamba nilikua nikimskia mama akilalama juu ya maovu ya baba kama vile kutokurudi nyumbani, kukesha nje akinywa pombe ama kuwa na familia nyingine nje(ambayo si kweli bali zilikuwa accusations tu). So ikanijengea mazoea yakuona kama mama alikuwa akionewa na baba na kuanza kumuona baba kama mtu ambaye ni waajabu sana.

Nimekuja kutambua umuhimu wa baba na kujuta makosa yangu makubwa niliyo yafanya kumchukulia Baba poa na kutokumthamini wakati alipokuwa hai . Kikubwa ninacho amini sasa hivi ni kwamba mama zetu ndio wanaochochea watoto wao kuwa na dharau kwa baba zao kutokana na mama kuwashirikisha watoto wao matatizo yao ya ndoa. Kama baba anatoa msaada kwa watoto anaspend time na watoto. Matatizo ya ndoa watoto wasishirikishwe bali yatatuliwe baina yenu tena kwa siri pasipo watoto kujua kinachoendelea.
 
Mwanamke by nature ni mbinafsi na mwenye moyo uliojaa tamaa, jambo la msingi wanaume ili tusidharaurike uzeeni ni kuweka assets binafsi zitakazo kupa heshima hata mzeeni mwako pasipo tegemea watoto hata mkeo alikukuacha na kwenda kwa watoto wake anauwezo hata kusogeza mke mdogo akakupa furaha
Mjadala huu nimeukuta kwa wazee wa Kagera. Siku hizi hawatoi mashamba makubwa yenye migomba mizuri badala yake kijana anapewa eneo la kujenga nyumba na choo halafu mzee anabaki na eneo kubwa. Akizeeka anatangaza kuuza sehemu ya shamba lake basi kijana anaanza kujisogeza karibu na mzee ndo anaanza kutoa masharti.....kilo moja ya nyama kila wiki, sukari kila wiki n.k halafu anamhesabia miguu kadhaa ya shamba. Kwa mfumo huu wazee wanakula vuzuri tofauti na zamani kijana anapewa shamba kubwa anavuna utajiri halafu yeye na mke wake wanawatelekeza wazazi.
 
Binafsi naona kuna cases nyingi katika hili.

Binafsi sikulelewa na baba, nimekuwa nikiwa simjui. Nimekuja kufahamiana naye baada ya kuhitimu kidato cha sita. Kwahiyo sina bond yoyote na baba.

Ila nilipokutana naye nilijihisi kusamehe tu ili maisha yaendelee, nikiamini sasa atachukua majukumu yake kama baba kumbe hana hata huo muda.

Hii ni special case kwangu na kwa wengine wenye case kama yangu na wale waliotelekezwa.

Ila pia, mimi ni mtoto wa kiume naona, ukiachana na kina baba makatili kwa watoto, wapo wanajitahidi sana kujali familia zao.

Tatizo huwa linaanzia kwenye kuweka duscipline ya watoto, mara nyingi hapa ndio kina mama huwa wanakaa pembeni ili kukwepa lawama.

1- Mtoto akienda kucheza akachelewa kurudi nyumbani, baba anampa adhabu au sometimes anamwambia hakuna kula. Tena mnakubaliana vizuri na mama yake, kumbe mama yake kaficha chakula huko jikoni anampatia baadaye baba hajui.
Mtoto anakuwa akijua baba ndio mbaya.

2- Mtoto kumwomba baba pesa kidogo labda nauli ya shule, baba akasema hana. Mama anatoa anampa mtoto huku akimlaumu baba.

Katika mazingira ya hivi, ni rahisi kwa mtoto kuwa na bond kubwa sana kwa mama kuliko mama. Na bond hii huwa ni kubwa mpaka kwa ndugu wa mama.

Mara nyingi undugu wa upande wa mama ndio huwa una nguvu sana kuliko upande wa baba.

Mimi nina Anko wangu, hata akiwaomba wanaye elfu 10 lazima wampigie simu mama yao kwanza. Bila ya mama kutoa go-head anaambulia patupu.

Pole Mkaruka
Nina uhakika wewe utakua baba bora, mwenye familia yenye furaha🙏
 
Mimi binafsi hayo yalinikuta kumpenda mama pekee na kumuona baba kama sio mtu wa karibu kwangu pale nilipo pata ajira nakuanza kushika pesa, kutokana na kwamba nilikua nikimskia mama akilalama juu ya maovu ya baba kama vile kutokurudi nyumbani, kukesha nje akinywa pombe ama kuwa na familia nyingine nje(ambayo si kweli bali zilikuwa accusations tu). So ikanijengea mazoea yakuona kama mama alikuwa akionewa na baba na kuanza kumuona baba kama mtu ambaye ni waajabu sana. Nimekuja kutambua umuhimu wa baba na kujuta makosa yangu makubwa niliyo yafanya kumchukulia Baba poa na kutokumthamini wakati alipokuwa hai.

Pole sana, kuwa na roho ya majuto ni wazi unampenda japo hayupo hai
 
Katika harakati nzima ya kulea mama ndio anabeba jukumu kubwa kuliko baba kwa tamaduni za kiafrika hasa kitanzania. Baba yeye analeta mkate yaani anashughulika kuhudumia familia financially lakini yaliyobakia mama anayatendea haki.So kama jukumu kubwa la malezi anabeba mama mtoto atakuwa karibu na mama kuliko baba.

Hata mtoto akiwa na shida yoyote anaenda kwa mama kwasababu hakuna ukaribu,urafiki wala mazoea na baba tena unakuta mtoto anamuogopa hata baba kwasababu anatumika kama chombo cha kuadhibia.Kwa kusema hivo kunakuwa hakuna connection yoyote ya baba zaidi ya genetics na finances which is horrible.Kulea ni zaidi ya huduma ya kifedha na kutoa nidham.
 
Kwa kusema hivo kunakuwa hakuna connection yoyote ya baba zaidi ya genetics na finances which is horrible.Kulea ni zaidi ya huduma ya kifedha na kutoa nidham.

Ukweli unaouma!!!!
Kwanini hii ni zaidi kwa wababa kiafrika na sio Asia au Europe?
 
Katika harakati nzima ya kulea mama ndio anabeba jukumu kubwa kuliko baba kwa tamaduni za kiafrika hasa kitanzania. Baba yeye analeta mkate yaani anashughulika kuhudumia familia financially lakini yaliyobakia mama anayatendea haki.So kama jukumu kubwa la malezi anabeba mama mtoto atakuwa karibu na mama kuliko baba.Hata mtoto akiwa na shida yoyote anaenda kwa mama kwasababu hakuna ukaribu,urafiki wala mazoea na baba tena unakuta mtoto anamuogopa hata baba kwasababu anatumika kama chombo cha kuadhibia.Kwa kusema hivo kunakuwa hakuna connection yoyote ya baba zaidi ya genetics na finances which is horrible.Kulea ni zaidi ya huduma ya kifedha na kutoa nidham.
Hii comment imebeba ujumbe mkubwa sana, unaodhihirisha ubinafsi wa kiumbe cha kuitwa mwanamke!
 
Mimi niwaombe wababa wabebe nafasi zao kwenye kutusimamia sisi wanafamilia, tena wawe wakali kidogo hapa kama mama wa taifa alivyokua mkali kwa chalamila alipoona anaharibu familia ya mwanza

Mkisema mtuachie wamama tufanye tutakavyo tutaharibu tuu...... hata Mungu anajua ndio maana aliwapa nyie mamlaka ya kuwa kichwa ili mtoe malekezo ya wapi tunaelekea kwetu
Hahaaa wamama wenyewe ndo hawa dada zangu kina cariha , Demi etc. utaanza vip kuwasimamia sijui

Si unaona mwenyewe misimamo yao, hadi kidume mwenyewe inasalimu amri, chezeyaaa
 
Back
Top Bottom