Ufafanuzi wa Hoja ya Gharama za Mradi kwa Kipande cha 3 na 4 cha SGR na Kuisababishia Serikali Hasara ya Tsh. Trilioni 1.7

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942

UFAFANUZI WA HOJA YA GHARAMA ZA MRADI KWA KIPANDE CHA 3 NA 4 CHA SGR KWA WASTANI WA DOLA ZA MAREKANI MILIONI 1.3 NA MILIONI 1.6 MTAWALIA NA KUISABABISHIA HASARA SERIKALI YA TSH. TRILIONI 1.7

Anaandika Mhe. David Kihenzile, Naibu Waziri Uchukuzi

Mheshimiwa Spika, Sheria ya manunuzi ya Umma imeainisha njia mbalimbali za manunuzi ya mkandarasi au Huduma zinazowezwa kutumiwa na Serikali ikiwa ni pamoja na njia ya Single Source .

Aidha, Manunuzi ya Mkandarasi kwa kipande cha tatu (3) na kipande cha Nne (4) yalifuata Sheria za Manunuzi ambayo ni Sheria ya Manunuzi ya Umma Namba 7 ya Mwaka 2011 na kanuni zake Na. 161 (Single source Procurement for works) ya Kanuni za Manunuzi ya Umma ya Mwaka 2013 na Marekebisho yake (Mwaka 2016).

Mheshimiwa Spika, Manunuzi ya Mkandarasi kwa kipande cha tatu (3) na Kipande cha (4), yalifuata sheria manunuzi ya mwaka 2011 na utaratibu wa njia ya Single Source kwa kuzingatia matakwa ya kanuni Na. 161 ya Kanuni za Manunuzi za Mwaka 2013 na Marekebisho ya Mwaka 2016, Naomba kuinukuu kama ifuatavyo:

161-1 (a) there is an urgent need for the works such that there would be insufficient time for a procuring entity to engage in tendering or any other method of procurement, provided that the circumstances giving rise to the urgency could not have been foreseen by the procuring entity and have not been caused by dilatory conduct on its part; or 161-1 (b) there is only one particular contractor which a procuring entity can reasonably expect to undertake the required works; or

161-1 ( c) there are advantages to a procuring entity in using a particular contractor
who has undertaken or is undertaking similar works or who may have already 2 been mobilized with plant, equipment and staff in the vicinity or any other resources as may be appropriate; or

161-1 (d) works which are under execution are to be extended, and the corresponding contract is awarded following national or international competitive tendering

Mheshimiwa Spika, wakati zabuni hii inatangazwa mkandarasi YAPI Merkezi alikuwa akitekeleza ujenzi wa reli kwa kipande cha 1 na Kipande cha pili, ambapo kazi za ujenzi wa tuta zilikuwa zimefikia 97% kwa Lot 1 na 95% kwa Lot 2 na kwa kuzingatia athari zilizokuwepo kipindi kile wakati tenda zinaendelea dunia ikiwa inatoka kwenye mlipuko wa Uviko-19 na baadhi ya Nchi zikiwa bado, kumtumia Mkandarasi au wakandarasi ndani ya Nchi na akiwa na vifaa tayari ilikuwa ina faida kwa nchi na mradi.

Mheshimiwa Spika, Gharama za ujenzi wa reli hizi kwa awamu zote zimetokana
na pembuzi yakinifu zilizofanywa na kampuni mbalimbali kati ya mwaka 2012-
2016 pamoja na mapitio (Review) ili kuona kama kuna mabadiliko yoyote ya makadirio (Engineering estimates) kampuni hizi ni kutoka CANARAIL (Canada), CPCS (Canada), Cowi (Denmark), Gauff Engineering (Ujerumani) na mapitio kwa watalaam wa ndani ya TRC.

Mheshimiwa Spika, gharama za ujenzi kutoka Kipande kimoja hadi kingine
hutotafutiana kwa kutegemea mambo yafuatayo:

(i) Miinuko na Mabonde (terrain) ambayo huathiri ukubwa wa kazi za ukataji milima na ujazaji wa mabonde (Earthworks) mathalani kwa kipande cha 3 kazi hii makadirio ni mita za ujazo milioni 65 na mita za ujazo million 33 kwa kipande cha 4 ikilinganishwa na mita za ujazo milioni 21.3 kipande cha kwanza na mita za ujazo million 24.9 kwa kipande cha 5

(ii) Ujenzi wa mihimili (structures) ikiwemo madaraja, makalavati, na madaraja makubwa mathalani kwa kipande cha 3 ina madaraja makubwa yanayounganika (viaducts), inapita kwenye bonde la ufa kati ya Manyoni na 3 Saranda (kilomita 50) na eneo la uwanda wa chini (swamps) kati ya Malongwe na Nyahua (kilomita 40)

(iii) Uwezo wa udongo (Soil bearing) huathiri ukubwa wa kazi za zege na nondo (Reinforced Concrete Works) wakati wa ujenzi wa misingi ya mihimili (Structures Foundations); mathalani kwa kipande cha 3 reli hii inapita kwenye eneo yowevu la bonde kati ya Malongwe na Nyahua

(iv) Tabaka la kijiologia (Geological nature) huathiri ukubwa wa kazi za udongo wakutolewa na kuwekwa udongo ulisanifiwa, na kuongezeka kwa mifumo ya ishara na mawasiliano (Signal and Telecoms Works) inayopelekewa na ugumu wa kijiografia (Line of Sight); mathalani makadirio ya minara ya mawasiliano ni takribani 42 kwa kipande cha 3 ikilinganishwa na minara 28 kwa kipande cha kwanza;

(v) Ukubwa wa uwanda wa vyanzo vya maji (Hydrological Catchment Size) huathiri kwenye ukubwa na idadi ya madaraja, makalavati na urefu wa mitaro;

(vi) Gharama za usafirishaji wa malighafi na vifaa vya ujenzi (Transportation costs)
huathiriwa na umbali wa mradi kutoka bandarini na viwanda vikuu kuelekea kwenye eneo la kazi husika, mathalani Dar es salaam hadi Tabora ni takribani kilomita 840 kwa njia ya reli ikilinganishwa na kipande cha kwanza kati ya Dar es salaam na Morogoro kilomita 184 kwa barabara na kilomita 210 kwa reli;

(vii) Umbali wa upatikanaji wa malighafi za ujenzi (Haulage distance) huathiri kazi
za ujenzi wa tuta, ujenzi wa mihimili (Structures); changamoto ya upatikanaji wa miamba migumu;

(viii) Urefu wa mradi na mawanda yake (Scope of Works) huathiri wingi wa vifaa ikiwemo reli, mataruma, mifumo ya ishara, mawasiliano na umeme, mitambo ya kuchochea na kupozea umeme (Transformer), wingi njia za kupanga na kuchambua mabehewa, karakana, nguzo, nyaya n.k.;

(ix) Ugumu na changamoto za kihandisi kwenye usanifu wa madaraja, majengo, na miundombinu mingine; mathalani eneo la bonde la ufa lenye matetemeko na plateau mbili

(x) Athari za mabadiliko ya Bei (Price adjustment) ambayo husababishwa na muda wa zabuni moja hadi nyingine na athari za majanga (mathalani Uviko-19 na vita), manunuzi ya kipande (Lot 1 & Lot 2) na kipande cha 3&4 ni miaka 5, mathalani 2017 bei za malighafi kubwa za ujenzi mathalani saruji $125 kwa tani, nondo $ 761.95 kwa tani, Dizeli TZS 1,954 kwa lita na reli $685 kwa tani ikilinganishwa na bei za mwaka 2022 ambazo ni Saruji $154 kwa tani, Nondo 4 $ 1,121.82 kwa tani, Dizeli TZS 2,553 kwa lita na reli $1,295 kwa tani ambapo ongezeko kwa reli ilikuwa saw ana 89.05%.

Mheshimiwa Spika, makadirio ya Ujenzi wa kipande cha 3&4 Makutupora hadi Tabora kwa mujibu wa makadirio ya mtalaam mwelekezi (Consultancy), ni dola za marekani milioni 4.92 kwa kilomita na kipande cha 4 dola za marekani millioni 4.89 kwa kilomita ukilinganisha na gharama halisi tulizosaini ambayo ni dola za marekani milioni 4.051 kwa kilomita kwa kipande cha 3 na dola za marekani millioni 4.32 kwa kilomita kwa kipande cha 4. Gharama zote ni kabla ya Kodi (VAT & Contig. exclusive).

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wataalam wake ilifanya utafiti kujiridhisha na Ujenzi wa miundombinu hii wa reli ya Kiwango cha SGR na nchi zingine Duniani, ikilinganishwa na wastani wa Dola za Marekani milioni 7.9 kwa kilomita Bara la Afrika (rejea UIC Global r ail I nfrastructure j ournal) na wastani duniani kati ya milioni 6 hadi milioni 9 kwa kilomita moja duniani.

Mheshimiwa Spika, Naomba kumfahamisha mheshimiwa Luhaga Joelson Mpina (Mb) na Bunge lako tukufu kuwa hakuna hasara yoyote iliyosababishwa na ununuzi wa mkandarasi wa ujenzi wa njia ya reli kwa kipande cha 3 na kipande cha 4 na ununuzi wa mkandarasi ulifuata taratibu zote za manunuzi ikiwemo majadiliano kwa lengo la kuhakikisha gharama sahihi za mradi zinapatikana. Hata hivyo makadirio ya gharama za kihandisi (Engineering Estimate) bila kodi ilikuwa ni Dola za Marekani bilioni 1.8 kwa kipande cha 3 na Dola za marekani milioni 806.6 kwa kipande cha 4 ukilinganishwa na gharama halisi za bei ya Mkandarasi (Base Price) bila kodi baada ya majadiliano ambayo ni Dola za Marekani bilioni 1.490 kwa kipande cha 3 na Dola za marekani milioni 712.8 kwa kipande cha 4.

Taarifa ya International Union of Railway imeeeleza kwa kina ujenzi wa Reli Barani Afrika ambapo Tanzania imetajwa ndio nchi yenye gharama ndogo zaidi katika ujenzi wa Reli Barani Afrika kwa wastani wa dola 7.9m kwa Kilommeta. Aidha Tanzania imetajwa ndio Nchi imejenga kilometa nyingi zaidi kuliko Nchi nyingine, Kati ya Kilometa 7200 zilizopo Afrika, Takriban Kilometa 2000(27.7%) zimejengwa Tanzania. Wastani wa ujenzi wa Kilometa moja ya reli(SGR) ni kama ifuatavayo:- Kenya dola 7.3m, Nigeria dola 6.1M, Morocco Dola 6.5M, Ethiopia dola 5.9M na Tanzania dola 4.3M.

Naomba nihitimishe kwa kuwaomba watanzania waelewe kuwa Serikali ya awamu ya sita Chini ya Mama yetu Dkt Samia Suluhu Hassan. inania ya dhati ya kuwaletea Maendeleo na Sisi wasaidizi wake tuna ari na nguvu kuhakikisha tunatimiza Adhima yake ya Kuwaletea Maendeleo wananchi.
 
Back
Top Bottom