Hivi unaamini kuwa habari za Tippu Tip alliandika huyo Jameson peke yake? Hicho kitabu alichoandika mwenyewe kinaitwaje?Unaposema alikuwa mfanyabiashara wa kawaida ulikuwa na maana gani? Huyo unayemuita mmachinga alipataje utajiri wake katika nchi ambamo biashara yake kuu ilikuwa utumwa? Unataka kutuambia alikuwa akifanya biashara gani? Hiyo mizigo ilikuwa mizigo ya nini? Na hao waliombebea aliwatowa wapi na baada ya safari walienda wapi? Ukiangalia umbali alikokuwa akitoa hiyo biashara yake basi hao wafanyakazi wote nao wangakuwa matajiri? Au mnataka kurudia tena uongo wenu kuwa hata biashara ya utumwa haikuweko Zanzibar?
Usitake kuandika historia upya. Hamuwatendei haki wale ambao waliumia kutokana na uovu wa utumwa. Si suala la uislamu au ukristu. Yeyote aliyehusika na biashara hii inabidi alaaniwe, awe mzungu, muarabu au mwafrika. Lakini laana hiyo haihusu vizazi vilivyomfuata.
Amandla........
Hili suala limekushtua,lakini ni tabia ya haki na ukweli hata zikipita karne ngapi huwa vinakuja juu kuzima uongo.
Wewe una hasara gani historia ikiandikwa upya iwapo iliyopo ni ya uongo.Unaposema
Hamuwatendei haki wale ambao waliumia kutokana na utumwa na uovu wa utumwa.Yawezekana wapo lakini wewe wala mimi hatuwajui,kilichobaki ni kisingizio tu cha kuupiga vita uislamu.
Hizi picha za watu waliofungwa minyororo zilizochorwa na wamishionari ni vyema muzibandike makanisani kwenu mutakuwa mumeeleweka lakini kuziingiza mashule zimeidhuru sana Tanzania.Ni sababu ya mapinduzi ya Zanzibar,sababu ya uchafuzi wa uchaguzi wa kidemokrasia,sababu ya vifo vya watu wengi na kadhalika.
Eti kinachotetewa ni kuzuia kurudi kwa waarabu waliowatumikisha mababu zetu.Hakuna aliyetumikishwa kwa nia ya kutumikishwa mbali na mfumo wa maisha wa siku hizo.Hivyo wewe leo ukijenga ghorofa lako Kariakoo ukawalipa kwa kuwapunja vibarua wako,hilo ghorofa litakuwa si la kwako kwa kuwa uliwalipa hivyo.Hapo zitakapokuja mashine za kufanya kazi za kubeba kila kitu bila vibarua itakuwa nongwa kwa wajukuu kwamba babu zao walijenga ghorofa yako.
Nakuhakikishia mashamba yaliyotaifishwa Zanzibar kwamba ni ya mababu zetu,zile zilikuwa mali halali za waislamu zilizochumwa na wenyewe akina Tippu Tip.Ushahidi wa kiroho juu ya hili huna ubavu wa kuupinga.Ikiwa huyu sheikh alifanya makosa katika biashara yake wewe huwezi kuwa hakimu wake na nakushauri ukubali hivyo.
Maelezo hapo juu kuhusu Tippu TIP yako wazi kabisa.Kwanini hutaki kuyaamini na unalazimisha kuamini yaliyoandikwa na akina Livingstone tu!.
Akili yako ikoje wewe?,kwamba huoni kwamba Tippu Tip hakuwa mfanyabiashara ya utumwa?.Kama wako wenzake waliofanya biashara hiyo basi ilikuwa ni wachuuzi tu wa maagent wa biashara hiyo ambao ni wazungu-wakristo na wahindi.Nani mwenye kosa zaidi kati yao.?
Kuwazushia waarabu kwa nia ya kuipiga vita dini ya uislamu vitu ambavyo viko hai ni kutotenda haki zaidi kuliko kutetea kwa uzushi watu ambao huwajui.