Swali unalokwepa kujibu ni: "jee waarabu walihusika na biashara ya utumwa?" Je waarabu walikuwa na watumwa? Jee waarabu walinunua na kuuza binadamu wenzao kama watumwa? Kama waarabu hawakuwa wafanyabiashara wakubwa hapa kwetu, nani alikuwa basi ndiye aliyemiliki biashara ya watumwa hapa kwetu.
Ubaguzi wa rangi umetoka wapi? Tippu Tip alikuwa anajihesabu muarabu pamoja na kuwa alikuwa na damu ya kiafrika. Sikujui kwa hiyo siwezii kujua mwenyewe unajiweka katika kundi gani. Lakini siwezi kuamini kuwa mtu anayetetea biashara ya utumwa kiasi unavyofanya, mtu anayesema kuwa anayenishangaa mimi kuona uchungu katika hao waliochukuliwa katika utumwa. Rangi yako inawezekana ikawa nyeusi lakini roho yako ni ya kiarabu.
Unajua kweli kusoma? Mara ngapi nimekazania kuwa watu wa rangi zote walihusika na biashara hii haramu? Niliwataja wachaga na wachina. Kwani wachaga wana rangi gani? Kwani wagogo waliotoza ushuru kwa waliofanya hii biashara walikuwa na rangi gani? Tofauti na wewe ambae uko tayari kukubali kuhusika kwa rangi nyingine yeyote katika hii biashara isipokuwa waarabu, mimi sitofautishi. Wote walihusika; waarabu, wazungu, wahindi, wachina, waafrika n.k.
Hapana. Kwa nini lazima tumuamini Tippu Tip? Kwa vile alikuwa muarabu na muislamu? Abdul Sheriff amesema kuwa alikuwa na watumwa 10,000! Hao watumwa aliwapata vipi? Umechagua aya zinazokutetea na kuacha nyingine. Soma aya ya 14. Alienda Ndegereko na Mbezi na sehemu zote za uzaramu akakamata watu 800 na kuwafunga minyororo. Hao wapagazi unaowazungumzia walirudi baada ya Tippu Tip kuwakamata ndugu zao na viongozi wao karibu 200. 800 aliwakamata baada ya wapagazi kurudi! Hao 800 aliwakamata kwa ajili ya nini kama sio utumwa?
Livingstone alitaka sifa kwa kupinga biashara ya utumwa? Hawa jamaa hawakupinga utumwa Afrika tu bali hata uingereza walikotoka. Henry Stanley hakuwa na sifa ya kupinga utumwa. Yeye alikuja ni mwandishi wa habari kumtafuta Livingstone na hakuwa mmishionari. Kuna ubaya gani wakina Livingstone kutaka kuingiza ukristu hapa kwetu? Mbona waarabu nao walifanya hivyo hivyo? Au unataka kutuambia kuwa uislamu ni dini ya asili ya hapa kwetu? Wote hao, waislamu na wakristu walikuja kwetu na ajenda zao. Hakuna aliye bora kuliko mwingine. Pamoja na kupinga biashara ya utumwa mbona Livingstone alishirikiana na wafanya biashara hiyo, wakina Mpamari? Mbona Stanley ndiye aliyependekeza nduguyo Tippu Tip awe Gavana wa Kongo? Wote hawa, waarabu na wazungu, walituona watu weusi kuwa watu wa kutawaliwa tu.
Hakuna mtu anaekana ushiriki wa nchi za magharibi katika biashara ya watumwa. Ukienda Marekani, ukienda uingereza utakuta makumbusho yakielezea ushiriki wao. Leo hii mwanasiasa yeyote Marekani hawezi kuzungumzia historia ya Marekani bila kuelezea utumwa. Bill Clinton na George W. walipokuja Afrika, waliomba msamaha kuhusu ushiriki wao katika biashara hiyo haramu. Ni lini na wapi waarabu wamekiri kuhusu kuhusika kwao? Ni lini Sultan Qaboos amezungumzia ushiriki wa waliomtangulia katika biashara hii? Hivi unategemea kweli kuna siku atakuja Afrika kuomba msamamha? Na ukiangalia, kwa nini afanye hivyo wakati apologists wake mmejaa humu mkiamini kuwa waarabu kama yeye ni haki yao kutufanya sisi watwana zake! Bila aibu unawatetea watu waliotufunga minyororo, kutuhasi na kutuuza kama njegele kwa vile tu ni waislamu wenzako! Sio siri kuwa wakristu na wazungu walishiriki na waliwafanyia mababu na mabibi zetu mabaya lakini hiyo haiwaondolei waarabu responsibility kuhusu unyama waliotufanyia. WAZUNGU WAKRISTU NA WAARABU WAISLAMU WOTE WALISHIRIKI KATIKA BIASHARA YA UTUMWA NA WOTE WANASTAHILI KULAANIWA KWA VITENDO WALIVYOWAFANYIA WALIOTUTANGULIA. Wewe unaweza kusema hivyo? Au unaona wakristu peke yao? Sasa mbaguzi ni nani, mimi au wewe?
Nilikuwepo!
Amandla....