Biashara ya Utumwa na Kanisa
Mnamo mwaka 1517, Mmisionari maarufu Bishop Bartholome de Les Cacas, ambaye alikuwa rafiki wa Wahindi Wekundu alimshauri Mfalme wa Hispania kuwa Waafrika toka Afrika ya kati wangefaa sana kwa kazi ya utumwa kuliko wenyeji wa Amerika, ushauri huu ulikubaliwa na mfalme wa Hispania. Mfalme wa Hispania alitoa mkataba kwa raia wake mmoja unaomruhusu kusafirisha watumwa 4,000 kwa mwaka toka Afrika kuwapeleka visiwa vya Caribean na kwa mara ya kwanza utumwa ulianzishwa kati ya Afrika ya Wareno na Marekani ya Wahispania.
Wazungu walitajirika kutokana na nguvu kazi ya utumwa toka ng'ambo kuliko walivyofaidika kutokana na nguvu kazi huru katika nchi zao. Ombi la Bishop Batholeme delas cacas lilikuwa mamilioni ya Waafrika kutiwa utumwani. Mwanasheria P. Dcuntin mwandishi wa kitabu The Atlantic Slave Trade
amekadiria kati ya milioni 15-20. Mwanamapinduzi wa Kimarekani marehemu Malcomx alisema kuwa kiasi cha milioni 100 ya Waafrika walitiwa utumwani na kufikishwa Amerika wakiwa hai. Haijulikani idadi ya waliofia safarini.
John Hawkins alifanya safari tatu Afrika Magharibi katika miaka ya 1560, na kuchukua Waafrika ambao waliwauza kwa Wahispania Marekani. Aliporudi Uingereza baada ya safari kwanza, kwa sababu ya faida kubwa aliyopata, malkia Elizabeth wa kwanza alitamani kushiriki katika safari ya pili; na alitoa meli iitwayo Jesus (Yesu) kwa safari hiyo. Hawkins aliondoka na Jesus (meli) kuchukua watumwa Waafrika zaidi na aliporudi Uingereza alipata faida kiasi kwamba, Malkia Elizabeth alimpa nishani. Hawkins aliamua kuwa nembo ya cheo chake kuwa alama ya Mwafrika aliyefungwa minyororo.(1)
Maaskofu na wachungaji wa kanisa wa ngazi za chini, walikuwa na watumwa wao waliofanya kazi mashambani, kuwabeba machela mabwana zao, wachungaji walipelekwa huko na huko katika safari zao. (2) Hayo yalifanyika sehemu nyingi za Afrika na kwingineko makanisa yalikokuwa yakijengwa enzi hizoza biashara ya utumwa. Na wale watumwa waliokamatwa Marekani walibatizwa kwa mpigo wakati wakipakiwa melini. Askofu alijengewa kiti maalum gatini kwa ajili ya kazi hiyo