Waandishi wanaume wananyanyasika kingono lakini hawasemi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
sexual-harassment-1-.jpg

Unyanyasaji wa kingono katika vyombo vya habari umekuwa ukitajwa kutokea mara kadhaa, mara nyingi waathirika wamekuwa wakiathirika kisaikolojia na wakati mwingine kuwafanya kuwa na msongo wa mawazo, mpaka wengine kuamua kuhamia katika taaluma nyingine.

Takwimu za Chama cha Magazeti na Wachapishaji wa Habari Ulimwenguni (WAN-IFRA) zinaonesha hadi kuelekea mwaka 2022 asilimia 30 ya waandishi wa habari Duniani wamekuwa wahanga wa unyanyansaji wa kingono iwe kwa maneno au kwa vitendo, wanaume wakiwa asilimia 12.

Utafiti uliofanyika Kenya, Aprili 2022 umeonesha kuna wanaume wengi wananyanyasika kingono kutoka kwa wanawake wanaofanya nao kazi au wadau wao wa karibu, lakini hawasemi. Wapo wanaofanyiwa kwa maneno, kushikwashika, kulazimishwa ukaribu usio wa lazima, kuulizwa maswali kuhusu muonekano, staili ya maisha, simu za kukera.

Nchini Kenya, chini ya Kifungu cha 23(1) cha Sheria ya Makosa ya Kujamiiana (2006) unyanyasaji wa kingono unaweza kuadhibiwa kwa kifungo kisichopungua miaka mitatu jela au faini ya Ksh. 100,000 (zaidi ya Tsh 1,982,705).


Source: Nation Africa
 
Ndugu mleta mada. Hebu ongeza nyama kwa takwimu kidogo. Bado hujaeleweka vizuri point yako.
 
Back
Top Bottom