Waandishi wa habari wa Tanzania nao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waandishi wa habari wa Tanzania nao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Boss, Oct 25, 2009.

 1. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Ukiangalia nchi za watu......hasa marekani
  utakuta watu wanaoandika vitabu mbbalimbali pamoja na
  vitabu vya maisha ya watu maarufu,viongozi na wengineo

  utakuta wengi wa wandishi hao ni waandishi wa habari au
  wana background ya uandishi wa habari

  sasa hapa kwetu suala la waandishi wetu na
  wahariri wao kuandika vitabu ni kama vile haliwahusu...

  Binafsi natamani kusoma vitabu
  biography au autobiography za watu wafuatao but sijui
  lini vitakuja kuandikwa.....

  Jakaya kikwete
  salma kikwete
  lowassa
  mkapa
  mwinyi
  kawawa
  salmin
  salma salmin
  regina lowasa
  makamba
  kingunge
  zito kabwe
  dr slaa
  mbowe
  lipumba
  fundikira
  mtikila
  mrema
  marando
  lamwai
  mengi
  rostam
  samuel sitta
  msekwa
  mangula
  malecela
  anna kilango
  mwakyembe  orodha ni ndefu.......
  Kwa ufupi tunahitaji vitabu vingi sana..
  Mtu unaweza andika kitabu topic zifuatazo pia

  inside bot
  the last days of mkapa ikulu
  ten years of mwinyi ikulu
  the last days of nyerere
  the truth about daudi balali
  who is anna mkapa?
  The secrets behind barrick co.
  Buzwagi the real thruth.
  Salim a salim.the president who never was.
  Inside chadema.

  Kwa ufupi ujumbe wangu kwa waandishi wa habari na wengineo

  tunahitaji vitabu vingi iwezekanavyo kwa urithi wa vizazi vijavyo
  so please andikeni vitabu
   
 2. m

  mwanamasala JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2009
  Joined: Jun 20, 2009
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hatuna independent journalists,wato walitokea TSJ ,an offshoot of CCM and government propaganda!Mtu akitokea kuandika Unauthorised biography ya kiongozi wa tanzania ,say tupate uhuru,watamwua mara moja.Maana ataandika makahaba na watoto wa nje etc
   
 3. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  the latter might make sense to write about, i dont know about the biographies of dull politicians who are almost similaar.

  Another thing would they be able to gather enough evidence to write about some of the scandals, have they got enough wit to be investigatives writers under the current administration. coming to think of all these you have given me the idea Lowasa here i come.
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280

  hilo la kumuua sidhani....
  Tatizo waandishi wenyewe ni kama wamelala...
  Hata biography ya mtikila au mrema inawashinda???????
   
 5. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Surely sio tu waandishi wa habari, bali hata wasomi wetu wana share yao kubwa.

  Samuel Huntington was not a journalist, but a scholars of international relations.
  Hapa lawama inaanzia kwa wananchi kwa kutokuwa na culture ya kusoma mpaka serikali kwa kutotoa incentive.Bada ya WW2 serikali kama ya UK ili commission an official history of WW2, reasonably independent, from the British.

  Sisi tumepigana vita ya Kagera hamna hata vi pamphlet tu vya who was who and did what, mwishowe watu muhimu wote wa kuwa interviewed wanajifia tu, tutabaki na speculation.Ditto to so many things.

  Data not available, even when available sabotaged due to incriminating evidence. Tatizo letu kila kitu kiko so centralized na serikali kuu ina control kila kitu, wtu waoga, hatuna culture ya expose kwa kiwango hicho.
   
 6. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2009
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Kifo ndugu, hao wa kina mtikila wenyewe unaowachukulia poa yawezakana ni wana mtandao. bado hatuna ule uhuru wa kweli kwa waandishi wa habari wetu, afu bongo kila mtu ni zaidi ya umjuavyo siunajua palipo na njaa?
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Oct 25, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  wasiwasi wangu blueray ni kwamba...tutakuja amka wakati
  tumeshachelewa saana......

  Juzi nilimwambia mtu kuwa tanu haikuwa chama kipya bali kulikuwa na taa iliyo zaa tanu alinishangaa kama naongea miujiza

  halafu hata watu wadogo kama madereva na wapishi wa ikulu
  na sehemu zingine za nchi hii wana mengi ya kuzungumza yenye faida but no one care.
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Oct 25, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  sio lazima kuandika yaliyojificha.japo waandike yaliyoruhusiwa basi kwa kuanzia......
   
 9. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #9
  Oct 25, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  please do that...
  Only write the truth....
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Oct 25, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  hakuna mwandishi alieuwawa kwa kuandika kitabu.wasomaji wenyewe wako wapi?
   
 11. W

  Wasegesege Senior Member

  #11
  Oct 25, 2009
  Joined: Oct 22, 2009
  Messages: 107
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu suala la Waandishi wa Habari wa Tanzania kinachowasumbua ni UKIHIYO. Taaluma ya Waandishi wa Habari imevamiwa na "MAKANJANJA" watu ambao walifanya vibaya kwenye Mitihani yao ya Kidato cha Nne au cha sita na hawakuwa na mwelekeo ndipo wakakimbilia kwenye taaluma ya Uandishi wa Habari.

  Ngoja niwachekeshe - Hebu ngoja chukua Gazeti lolote lile na angalia Habari, utakuta waandishi wa Habari - wanaandika alisema, aliendelea kusema, akasema, na pia aliongeza, aliendelea kusema n.k. Hivyo ndivyo waandishi wa Habari wetu wa Tanzania. Hawana uwezo wa kumsikiliza Mtu na kuweza kuyachambua mawazo au maelezo yake na kuyaweka kwenye habari. Ndiyo maana siku hizi watu wengi wananunua magazeti ya Udaku ili wasome taarifa za kufumaniana n.k.

  Sikiliza Redio zetu, utacheka na utavunjika mbavu.

  Hakuna waandishi waliobobea au walio na taaluma mfano za Mazingira, Uhandishi, Sheria na Michezo. Utakuta Mtu anaandika habari za Mahakama wakati hana hata taaluma au ufahamu wa Taaluma ya Sheria n.k.

  Mie huwa napata wasix2 sana kwa sababu ya Waandishi wetu.

  Sasa kama Uandishi wenyewe ni wa "COPY AND PASTE" ya maneno ya watu hao waandishi wa Habari watapata uwezo gani wa kuandika Vitabu au taarifa za Viongozi wetu?

  Mafunzo wanapata miezi mitatu baada ya hapo anakwenda kuandikia Gazeti fulani au Redio fulani.
   
 12. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #12
  Oct 25, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,599
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  wakiandika hivyo vitabu mtasoma??Tanzania watu hawana utamaduni wa kusoma vitabu, zaidi ya magazeti ya shigongo, ukitoa vithibitisho kuwa kuna wasomaji wengi wa vitabu Tz, mimi nitaandika changu japo si mwandishi wa habari ni mhandisi.
   
 13. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #13
  Oct 25, 2009
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tunalaumu wasomi bila kutafakari mfumo uliozaa wasomi hao. Unatarajia wasomi wa aina gani wakati elimu yetu ya sasa ni kukariri, kusoma katika mazingira duni na kujali wingi wa wanafunzi bila kujali ubora wa elimu? Kama tusipobadili mfumo huu tutaendelea kuwa na waandishi na wasomi wanaoganga njaa kwani mfumo umedumaza akili na uwezo wetu wa kufikiri. Hata waliosomea nje, wakirudi wanamezwa na mfumo nao wanaanza kukimbizana na shilingi bila kuwa na ubunifu na mikakati yoyote ya kuiendeleza nchi.
   
 14. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,721
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  mkuu big boss, unadhani wamelala, tatizo ni uwezo.

  simaanishi uwezo wa kipesa, lahasha, bali wa kuchanganua mambo na kujua lipi lianze na lipi lifate, lipi la muhimu na lipi la kijinga. na hii imesababishwa na ukweli kuwa fani hii imejaa vilaza na vihiyo.

  yaani katika fani zilizojaa watu wa aina hiyo, hii na uwalimu, zinaongoza na nyingine zinafuatia.
   
 15. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #15
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  leo kwa mara ya kwanza nimekuelewa, huwa unaonngea point sana tatizo lugha yako anyway umezungumza kila kitu sina cha kua add.
   
 16. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #16
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,721
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  umenena mkuu...
   
 17. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #17
  Oct 26, 2009
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,276
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Umenikumbusha pale mzee John Malecela kuna wakati aliiita fani ya uandhishi wa habari kwamba ni "cheque book journalism" au uandishi unaoendana na kupata hongo ili uandike uzuri.

  Halafu juzijuzi raisi Kikwete nae akaja na msamiati mwingine wa waandishi habari makanjanja.

  Uandishi ni kazi nzuri sana na inayolipa uzuri sana na waandishi wazuri ni wale wanoelewa mambo mengi.

  Namaanisha kwamba kwa mfano unakuwa dakrari na hapohapo uankuwa mwandishi wa habari za udaktari wa (mfano moyo).

  Nchi yetu imejaa televisheni nyingi tu na zote huonesha kazi za waandishi wengine wa nje na televisheni zao, ni lini tutatengeneza za kwetu?

  Hata uandishi wa "biography" unataka mtu anaesoma historia kwa sana. Sasa kama hawapo waandishi wa kuandika habari na vitabu na hata pia kutengeneza "documentaries" mbalimbali na kuziweka kwenye televisheni basi hatuna waandishi.
   
 18. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #18
  Oct 26, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Mkuu, labda vitabu vyenyewe havina mada inayouzika ndiyo maana havinunuliwi. Lakini kama mtoa mada alivyoshauri baadhi ya mada ]siyo biographies] vitabu vitauzika.
   
 19. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #19
  Oct 26, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,599
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  Vya mapenzi na udaku vitauzika sana. Ila vya jiografia, afya, histori, hamna kitu.

  Mkuu Nkrumah, nimesoma UDSM wakati nasoma wanafunzi wengi huwa hawaendi Library kusoma au kutafuta vitabu, achilia mbali matangazo tu , hawasomi mkuu,

  Tabia ya kujisomea inaanzia utotoni, ndugu, huku ughaibuni nawaona akina mama wazee sana, lakini wanasoma novo ndani ya vasi au wakati wanasubiri huduma!

  Shule zetu hizi za tuition, past paper na kuotea maswali hazimfanyi mwanafunzi kuwa msomaji mzuri wa vitabu.
   
 20. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #20
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mkuu Waberoya,

  Hii ni habari ya "kati ya kuku na yai kipi kilianza?".

  Media ina influence kubwa sana, watanzania si kweli kwamba hawana culture ya kusoma, watu wamesoma sana tangu vitabu vya Adili na Nduguze mpaka Willy Gamba, Hammie Rajab, Ben Mtobwa na Agoro Anduru.tena mpaka mayaya walikuwa wanasoma hadithi hizi kwa hiyo si swala la kwamba hatuna critical mass.na kama watu wanaweza kufuatilia fiction, non fiction ikiandikwa for the general public, kwa mfano mtu aamue kuandika kuhusu vyombo vya habari Tanzania vilivyokuwa independent in the sixties licha ya perception ya mkono wa chuma wa Nyerere, kitabu kikapewa colorful anecdotes za kutosha, kikapewa thematic flow, kitauzika tu.

  Tatizo wala si uwezo kiasi hicho, ni kweli waandishi wetu wengi wa sasa ndio hao makajanja, lakini mbona tunao ma giants? Wako wapi kina Uli Mwambulukutu, waandishi waliokuwa sio tu wanaandika katika kiwango cha kimataifa na kufuatilia international media kama New York Times wanasemaje kuhusu Tanzania, bali pia waliandika kukosoa articles za New York Times zilizokuwa na makosa, this was around 1980, bila internet !. Wako wapi hawa wazee wenye uzoefu mkubwa serikalini na kwenye nyanja nyingine?

  Hisia zangu ni kwamba hawataki kuandika kwa sababu wanajua kuandika kwao kutafichua mabaya mengi.Hatutaki critical analysis kwa sababu tunaogopa what will be exposed.
   
Loading...