Waandishi wa habari Iringa wamgomea Robert Manumba!

Nadhani cha msingi ni kugomea habari za wizara ya mambo ya ndani na jeshi la polisi.

yani huu mwaka hawatausahau kwani ndio kaburi lao na maovu waliyoyatenda yanadhidi kuwarudia wenyewe.

Fear not.
 
Kuna Mwana mbeya mmoja (sina uhakika lakini pengine anajiita tu) kazi yake ni mc wa maharusi na redio moja ya ngono,music na pombe. wenyewe wanaita redio kiburudisho! tena anasemaga ni wa huko huko Tukuyu! Ukimsikia anavyoshabikia dhulma wanayofanyiwa raia daaah! Huwezi kuamini kama kweli huyu jamaa ni mmbeya kweli au kiraka.

kasha** yule
 
TBCCM si watakuwa wameenda ? Poleni ndugu zangu wa mbeya najiulizaga sana kwa nini mnaandamwa nyie tu.

Mwandosya, Mwakyembe, Mwaikusa,Ulimboka,Mwambigija, Mwangosi!!!!! What a coincidence? System ya mkweree ina mkono wake humo sio bure; chungeni sana nyie wanyak..........!!!!! Na hiyo M4C ikienda huko Mbeya ndio utasikia kiama kwani kwa tabia hii ya polisi kuanzisha fujo wanyambala watarudisha mapigo na amani itatoweka!!
 
Nimemsikia Waziri asiye na Wizara Maalum Mark Mwandosya katika Ebony FM akisema vyama vya siasa vinahusika na mauaji, ameelekeza wazi lawama kwa CDM kwamba ni wauaji.
Sijui kwa nini wanaogopa kuwataja Polisi?
 
Walichofanya polisi ni sawa na kulala na mama wa kambo tena kwenye kitanda cha baba yako, halafu ukafumwa. You never kill a journalist.

By the way anataka aseme nini wakati tume iko kazini?
 
Ktk muendelezo wa msimamo wa waandishi wa habari nchini kugomea kuandika habar zihusuzo polisi na maagents wao umechukua ukurasa mpya baada ya leo waandishi wa habari mkoani iringa walipogemea mwaliko wa kamishina wa makosa ya jinai nchini Robert Manumba (Gamba asilia) ambapo alihitaji kuzungumza nao.

The Struggles aluta continua.
Fear not.

Maumivu huanza polepole. Kazi ndiyo imeanza. Ila ningetaka wagomee Jeshi la Polisi lote kwa kuandika habari mbaya tu zinazohusu uozo wao. Yaani walichambu mno maana hata makao makuu wana makosa, na waziri mwenye dhamana naye ana makosa yake na wizara yake iadhibiwe kwa kutoiandika vema kwa watanzania.
 
Nimemsikia Waziri asiye na Wizara Maalum Mark Mwandosya katika Ebony FM akisema vyama vya siasa vinahusika na mauaji, ameelekeza wazi lawama kwa CDM kwamba ni wauaji.
Sijui kwa nini wanaogopa kuwataja Polisi?

huyu mzee naye toka kaumwa na kupewa offer ya uwaziri basi kashachanganyikiwa kabisa.
 
Walichofanya polisi ni sawa na kulala na mama wa kambo tena kwenye kitanda cha baba yako, halafu ukafumwa. You never kill a journalist.

By the way anataka aseme nini wakati tume iko kazini?

Yaani Mkuu MtamaMchungu popote pale duniani Journalist ana kinga na ndiyo maana hata vita viwe vikali kama vya Libya, Siria, Dufur huwezi sikia ameuawa kwa kulengeshwa. Akifa inakuwa kwa bahati mbaya. Na ndiyo maana wanakuwa front kabisa wana ripoti matukio magumu kabisa. Leo hii eti Tanzania inajidai kisiwa cha amani na kutumika kusuluhisha migogoro ya nchi nyingine leo inakuwa ndo nchi yenye migogoro tena na raia wake? Sielewi hili kabisa.
 
waendelee na msimamo huo ikiwezekana hata JK akiwaihitaji wasiende maana ndie chanzo cha huu hujinga kuteua mawaziri uchwara wasiojua nini maana ya uongozi
 
TBCCM si watakuwa wameenda ? Poleni ndugu zangu wa mbeya najiulizaga sana kwa nini mnaandamwa nyie tu.

Alianza Prof.mwandosya-Sumu iuayo polepole! akaja Dr.Mwakyembe-Immediate killing poison (Mungu tu alimwokoa), kisha Dr.Ulimboka-Mabwepande (Ananikera sana kwa nini mpaka sasa ameuchuna kuwataja waliotaka kumuua) na sasa mwandishi Mwangosi daud (Bomu la kujitoa mhanga la Polisi).Sijui anafuatia nani na kwa nini Mbeya kama mko kimya vile au tusubiri kama Uli!!!!!!
 
RED: Linasomwa kwenye ofisi za chama na serikali tu (tena na mawaziri na manaibu wao tu)

Blue: Haliuzwi Tandale kwa Mtogole

Hao wenye blue wamenichekesha sana,yupo jamaa anadili na mtandao wao akaulizwa na makwaia wa kuhenga(je tutafika?) wanapata watu wangapi kwa siku akasema km laki kadhaa wanatembelea mtandao wao kwa siku,mara akabadili akasema kila siku watu wanasoma headings mara laki kadhaa mara akasema watu wanaotembelea mtandao huo kwa siku ni elfu sita duniani kote,mwisho ndio nikachoka zaidi eti kwa mwezi wanatembelea watu million moja,yaani wakati kwa siku ni elfu sita, hawana kitu
 
Nimemsikia Waziri asiye na Wizara Maalum Mark Mwandosya katika Ebony FM akisema vyama vya siasa vinahusika na mauaji, ameelekeza wazi lawama kwa CDM kwamba ni wauaji.
Sijui kwa nini wanaogopa kuwataja Polisi?

1.Analipa fadhila za uwaziri usio na kazi maalum,may be mojawapo ya kazi zisizomaalum ni kuropoka kama hivi.Penyewe Prof,labda kadata na ugonjwa hivyo amepoteza ule umakini wake(Sijui bado anaota Urais?)

2.Hii redio ni wambea balaa,wengi waoga na wanafiki EXCEPT, to me at present best wa hii redio ni Raymond Fransis na Edo na baadhi nimewasahau majina, (Malegesi na Neema jirekebisheni mmenikera sana juzi na jana-Sio Vurugu za Wafuasi wa CDM na Polisi semeni Vurugu za Polisi kuzuia mikutano ya ndani ya wafuasi wa CDM ambayo CCM wanafanya siku nzima usiku na mchana)

3. Ni kweli kabisa, Vyama hivyo ni CCM na POLISI (Namshauri Tendwa badala ya kusajili ADC aipe usajili wa kudumu POLISI)
 
Tutatue kwanza msingi wa tatizo, ndiyo tuje kwenye tatizo lenyewe, la sivyo, kuongea upuuzi, eti mara Dailynews halisomwi, haitusaidii. Daily news lenyewe, huenda hata wewe mwenyewe na kadigirii au kadiploma kako ka Gentleman class huwezi kulisoma na kulielewa. Chanzo cha watu kufa ni ubishani wa Chadema kulazimisha kikao eti kwa sababu CCM nao wanafanya kikao somewhere. Hiki ndo chanzo, Polisi wamefanya kazi yao tu, kwa mujibu wa Police duties and CPA 1985.Utazunguka sana, tutapiga kelele siku kadhaa, lakini damu ile hairudi. Suala la kusema Mungu amsamehe ni falsafa tu, amekwenda huyo, watoto wake wanateseka, hata wewe mwenyewe hutawasaidia kitu. Tunasema aluta continue, ebu nenda nawe angalau uvunjwe mguu ili uone. Mbona ulimboka hasemi aluta continue tena?Tujichunge, fujo zetu zitaathiri familia zetu, ni kazi ya chama chochote kile tawala duniani kutumia majeshi yake kwa wapinzani. ndiyo hali halisi, usimuhimize mwenzio kuwa chambo, anza wewe.
 
Ktk muendelezo wa msimamo wa waandishi wa habari nchini kugomea kuandika habar zihusuzo polisi na maagents wao umechukua ukurasa mpya baada ya leo waandishi wa habari mkoani iringa walipogemea mwaliko wa kamishina wa makosa ya jinai nchini Robert Manumba (Gamba asilia) ambapo alihitaji kuzungumza nao.

The Struggles aluta continua.
Fear not.

jipange upya kaka.
 
Back
Top Bottom