TANZIA DCI wa zamani, Robert Manumba afariki dunia

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
20,714
45,103
Mkurugenzi mstaafu wa makosa ya Jinai DCI Robert Manumba amefariki dunia usiku huu.

Taarifa zaidi zitakuja hivi punde

1F9A85F3-5220-4F00-AE4F-04330ADEBE32.jpeg


===
Katika utumishi wake ndani ya Jeshi la Polisi amefanya kazi katika nyadhifa mbalimbali zikiwemo Chumba cha kupokea mashtaka kuanzia mwaka (1976 – 1977), mwendesha mashtaka wilaya ya Kibondo na Kasulu mkoani Kigoma, 1977 – 1984), Mkufunzi katika chuo cha polisi Dar es salaam, (1984 – 1987), Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Magomeni na Kinondoni na Naibu Mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Dar es salaam (1987 – 1993).

Pia, amewahi kuwa Mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Arusha, ( 1993 – 1995), Mkufunzi mkuu wa Chuo Cha Polisi Moshi ( 1995 – 1996), Mkuu wa kitengo cha Fraud makao makuu ya upelelezi, (1996 – 1997), Mkuu wa kitengo cha usalama wa nchi, intelijensia na madawa ya kulevya makao makuu ya upelelezi (1997 – 2001) na kuwa msaidizi wa mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai nchini (2001 – 2006). Kuanzia mwaka 2006 hadi anastaafu, alikua Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai nchini.
 
kuna wakati aliwahi kuugua malaria kali iliyofika hadi eti vidudu elfu 50 , inasemekana aliponea Johannesburg .
Yani vitatu tu kwa wengine iwe shida ila kwake elfu 50 basi inaonekana alikuwa na kinga za kutosha.
 
Back
Top Bottom