Skype hakuna lisilo na mwisho,linafadhaisha ila tambua kwamba tangu misingi ya Dunia kuwapo,uwongo haujawahi kuushinda ukweli,pamoja na mambo yote ya kisiasa lkn mwanadamu mwenye kujitambua ni lazma amtambue Mungu.Mtu au Kiongozi yeyote asiyekuwa na hofu ya Mungu hatma yake haielezeki,Serikali ya ccm misingi na nguzo zake zimesimamia kuzimu,na siku zote baba yake mtu muongo na muovu ni SHetani,Tbc wanajua wafanyacho wakijiaminisha wametuaminisha.ebu tuendelee kuishi kwa imani tukiamini hakuna kamba isiyo na mwisho,hao vibaraka wa maccm hawana muda.UKWELI HUU NTAUUFIA...
The nation that destroys its destroys itself.
Habari nzima ya "hakuna lisilo na mwisho" ni methali ya faraja zinazoweza kutumiwa na waangamizi.
Kwanza hatujui kama ni kweli hakuna lisilo na mwisho. Kwa kadiri tujuavyo namba hazina mwisho kwa maana ya kwamba unaweza kuongeza moja juu ya mwisho wowote ulio nao katika mstari wa namba.
Hapo habari nzima ya "hakuna lisilo na mwisho" inakauka. Mwisho wa namba ni namba ngapi?
Pili, hata kama kuna mambo yataendelea kwa muda mrefu sana na kuisha, kama vile jua letu hili "sole Sol" litavyozimika katika miaka bilioni tano ijayo - mingi ajabu- kwa sababu hydrogen na helium zinazolipa mafuta ya kuangaza zitakwisha, hilo halimaanishi kwamba halina mwisho.
Habari ya "hakuna lisilo na mwisho" ni habari ya kutolewa na viongozi walioshindwa kuongoza, wanaowapa wananchi wao matumaini mafu kwamba matatizo yataisha "in due time" na "of course".
Kama Kikwete anapokwenda kwenye "ajali" ya kifusi kufukia wachimba madini na kuwaua, na badala ya kuongelea tahadhari na kujiandaa maafa yasitokee, anawaambia watu habari ya "kazi ya mungu haina makosa".
Wanamapinduzi hawatakiwi kusema "hakuna lisilo na mwisho".
Vipi ukiambiwa "ni kweli hakuna lisilo na mwisho, utawala dhalimu nao una mwisho, ila mwisho wake utakuja miaka bilioni tano ijayo pale jua litakapoishiwa na hydrogen na helium atoms". Utasemaje hapo?
Uongo haujawahi kuushinda ukweli?
Ukisoma Aristotle alivyodanganya dunia mpaka dunia kuja kuoneshwa na Galileo hapo kwenye "leaning tower of Pisa" kwamba Aristotle alidanganya au kukosea ilikuwa miaka karibu 2000. Kama unasema uongo mara zote huwa na historia ya hatima ya kuvumbuliwa labda unaweza kuwa na jambo la kusema, lakini kuna mangapi ambayo mpaka leo ambayo watu wanaamini ambayo bado ni ya uongo?
Tuchukue mfano hiyo habari ya mungu. Uongo mkubwa kabisa kuliko mambo yote yaliyoweza kusemwa na binadamu. Mpaka leo unaaminiwa na hakuna shaka kwamba miaka 100 ijayo, hata 500, unaweza kuendelea kuaminiwa kama leo baadhi ya watu wanavyoendelea kuamini kwamba dunia ni ya ubapa.
Kuzimu? Ndo wapi huko? Uongo mwingine huo. Ukiamini kuna kuzimu ni bora hata uamini utawala wa CCM ni mzuri. Mana utawala wa CCM unaonekana na mtu anaweza kukuonyesha barabara uliojenga.
Kuzimu umekuona lini?
Shetani?
Uongo mwingine huo.
Shetani mnamsingizia tu mambo ambayo yamewashinda. Kama mungu.
Leo naamua kuwa wakili wake. Pro bono.
Shetani ni wewe binadamu. Mungu ni wewe binadamu. Wewe una uwezo wa kufanya vibaya (ukawa shetani) na vizuri (ukawa mungu). Vibaya ni nini na vizuri ni nini ni swala jingine. Kwa nini unamtafuta shetani na mungu mwingine?
Imani?
Kwa nini tuishi kwa imani wakati tunaweza kutafuta ujuzi? Kama unataka kuishi kwa imani kwa nini usiuamini utawala wa CCM unapokuhubiria habari za "Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania"?
Angalia mambo kwa kina kabla kumtaja adui kwa jina.