GE2025 Waandishi ambao hawajasajiliwa JAB marufuku kuripoti Uchaguzi Mkuu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,234
Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, ametoa onyo kali na kupiga marufuku waandishi wa habari ambao hawana ithibati kutoripoti kabisa uchaguzi mkuu kwani kufanya hivyo ni kosa la kisheria.

Amesema kuwa ni kosa la kisheria kwa mwandishi wa habari kufanya kazi bila kuwa na kitambulisho maalum kilichotolewa na Bodi ya Ithibati, hasa wakati wa uchaguzi, adhabu yake ni faini ya kati ya shilingi milioni tano hadi milioni kumi au kifungo cha miaka mitatu hadi mitano jela.

Akizungumza katika mkutano wa wadau wa sekta ya habari na utangazaji kutoka Kanda ya Mashariki uliofanyika jijini Dar es Salaam, Kipangula amewaonya wanahabari wanaofikiria kutumia vitambulisho kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) wakati wa uchaguzi, akisitiza kuwa INEC watatoa vitambulisho hivyo kwa wanahabari wenye Bodi ya Ithibati tu.

Amesisitiza kuwa Bodi ya Ithibati itaendelea kushirikiana na taasisi nyingine kuhakikisha kuwa sheria hiyo inatekelezwa kikamilifu ili kulinda weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari nchini.
 
Mwandishi ambae atapeleka maombi akumbuke kuambatanisha na kadi ya CCM wakati wa maombi hayo Asante.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, ametoa onyo kali na kupiga marufuku waandishi wa habari ambao hawana ithibati kutoripoti kabisa uchaguzi mkuu kwani kufanya hivyo ni kosa la kisheria.
Amesema kuwa ni kosa la kisheria kwa mwandishi wa habari kufanya kazi bila kuwa na kitambulisho maalum kilichotolewa na Bodi ya Ithibati, hasa wakati wa uchaguzi, adhabu yake ni faini ya kati ya shilingi milioni tano hadi milioni kumi au kifungo cha miaka mitatu hadi mitano jela.

Akizungumza katika mkutano wa wadau wa sekta ya habari na utangazaji kutoka Kanda ya Mashariki uliofanyika jijini Dar es Salaam, Kipangula amewaonya wanahabari wanaofikiria kutumia vitambulisho kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) wakati wa uchaguzi, akisitiza kuwa INEC watatoa vitambulisho hivyo kwa wanahabari wenye Bodi ya Ithibati tu.

Amesisitiza kuwa Bodi ya Ithibati itaendelea kushirikiana na taasisi nyingine kuhakikisha kuwa sheria hiyo inatekelezwa kikamilifu ili kulinda weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari nchini.
 
Masharti kibao uchaguzi usiotiliwa maanani na wapiga kura wa nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…