Waalimu wahamia kuendesha bodaboda na kupiga picha mitaani

Mkuu sasa Huyo mwalimu atapata wapi muda wa kuandaa somo ili madent wapate kilicho bora?ataishia tuu kuzuga class ,mind u kwamba mwalimu in MTU was kusoma muda wote
Sasa kama mshahara hautoshi afanyeje? Afe njaa ?
 
Kwani walimu wanamishahara midogo kiasi cha kuonewa huruma kiasi hicho? Si mishahara ambayo hata sisi watumishi wengine wa umma tunapokea. Hilo la kwenda kufanya bodaboda ni maamuzi yao lakini sio kwamba wanashida sana au wanalipwa kiasi kidogo tofauti na sie wengine ambao sio walimu
Wacha upuuzi wako wewe kama umeridhika na mshahara wa Tsh.700000 kwa mwezi ni wewe. Hiyo pesa haitoshi na haitakaa itoshee. Huyo aliyezuia walimu wasiendeshe Boda Boda analipwa milioni 4 na upuuzi kwa mwezi sasa mwambie umlipe hata milioni kwa mwezi kama atakuelewa.
Nawashangaa sana nyie wafanyakazi wa serikali badala ya kuungana mpewe maslahi mazuri iwasaidie ndio kwanza mnasemana . utaendelea kuwa masikini mpaka mwisho wa Dunia. Pumbavu sana
 
Sasa kama walimu wakiume wanaendesha boda boda walimu wakike watafanyakazi gani? Nipe jibu.katika Kazi mbaya na yakimaskini wakutupwa ni Kazi ya uwalimu bora kipindi cha jk alikuwa akiongeza mshahara na madaraja yalipanda kwa huyu muheshmiwa mwenye Sera ya uwakiki badala Sera ya kufanya maisha ya watumishi yawemazuri katika utawala utakao chemka ni huu mwenye kubisha abishe ila muda ndio msemakweli sasaivi watumishi wanavumilia ila muda utafika uwoga utaekwa pembeni
 
mimi naona ni kawaida tu.lazma wawe creative.ili wapate hela ya ziada kwa matumiz mengin ya kifamilia.salary hazikidh ukilinganisha na ugumu wa maisha
 
Ualimu ni kazi sio wito,waalimu wapewe mshahara unaokidhi haja zao!
 
Mkuu sasa Huyo mwalimu atapata wapi muda wa kuandaa somo ili madent wapate kilicho bora?ataishia tuu kuzuga class ,mind u kwamba mwalimu in MTU was kusoma muda wote
Sio Tanzania hii mwalimu ni wa kusoma muda wote.Labda kwengineko wanako heshimu kila taaluma na Ujuzi wa watu.Sio sisi,wanapenda kufanya hivyo ila mazingira na mifumo yetu ipo hovyooooooo....upo sahihi kabisa.Ila mifumo ipo hovyooooo kabisa.
Ikiwa masaa nane napoteza shule na kipato mpaka kinifikie ni 480000/= mpaka 500000/= ambazo bado haziendani na mazingira yangu husika.Sekta ya elimu sio kuongea ongea .....hatufiki popote kwa kuwa tumewekeza kwenye majungu na siasa mbovuuu.Nchi inaongozwa kimajungu majungu,taratibu hazieleweki.Kuna mengi sana yanaharibu mfumo wetu wa elimu.Inatosha....maana hata mimi ni muathirika wa mwalimu aliyekuwa akiuza kachori na bagia na nilikuwa nikisaidia hiyo biashara.Hapo ilikuwa darasa la tatu......
 
bodaboda_0.jpg

Mkuu wa Mkoa amepiga marufuku kujiingiza kwa walimu katika biashara ya uendeshaji bodaboda na upigaji picha mitaani kwa sababu kunashusha kiwango cha taaluma kwa wanafunzi.

Telack alitoa katazo hilo juzi baada ya kupokea taarifa kuwa baadhi ya walimu wanatoroka shuleni na kwenda kufanya shughuli zao binafsi, ikiwemo ubebaji abiria kwa pikipiki.

Akizungumza na wakuu wa shule zote za manispaa ya Shinyanga, waratibu elimu na maofisa elimu, Telack alisema atawafukuza kazi walimu wanaokacha vipindi.

Kwa habari zaidi nunua nakala yako ya NIPASHE LEO

My take;
Roho inaniuma mpaka natamani kuhama nchi hii. Maisha ni watu na watu ndio sisi tuwajali basi waalimu wetu. Roho imeninyonga nyonga asubuhi hii kwa hii taarifa. Inauma walahi
 
Na huyo alitoa hilo tamko analipwa mamilioni na posho kapewa ya kuhutubia hapo.mwalimu wana posho gani na kwa ugumu huu wa maisha na elimu yao bure mbona kutakuwa zaidi ya bodaboda wasitegemee mwalimu afundishe vizuri darasani akiwa na mawazo ya mshahara mdogo majukumu kibao lazima atoroke akajikimu.
 
bodaboda_0.jpg

Mkuu wa Mkoa amepiga marufuku kujiingiza kwa walimu katika biashara ya uendeshaji bodaboda na upigaji picha mitaani kwa sababu kunashusha kiwango cha taaluma kwa wanafunzi.

Telack alitoa katazo hilo juzi baada ya kupokea taarifa kuwa baadhi ya walimu wanatoroka shuleni na kwenda kufanya shughuli zao binafsi, ikiwemo ubebaji abiria kwa pikipiki.

Akizungumza na wakuu wa shule zote za manispaa ya Shinyanga, waratibu elimu na maofisa elimu, Telack alisema atawafukuza kazi walimu wanaokacha vipindi.

Kwa habari zaidi nunua nakala yako ya NIPASHE LEO

My take;
Roho inaniuma mpaka natamani kuhama nchi hii. Maisha ni watu na watu ndio sisi tuwajali basi waalimu wetu. Roho imeninyonga nyonga asubuhi hii kwa hii taarifa. Inauma walahi
Nimewahi kubebwa kwa pikipiki na mwl mmoja hapo shy (baada ya masaa ya kazi). Mie nilimpongeza. Wafanyeje hawa walimu kama mishahara ni midogo sana, promotion hakuna na tuition ni marufuku. Naamini siyo Shinyanga peke yake maana naamini ndiyo njia baadhi yao wameamua kama namna ya ku-cope na hali halisi ya sasa.
 
Kama baba kashindwa kuwajali watoto wake mwenyewe ndani ya familia unategemea nini kutoka kwa watoto kama si kuamua kupambana kivyao ili wayamudu maisha? Walimu hawapaswi kulaumiwa kwa hili, mbona madaktari na manesi wana part time baada ya kazi mmekaa kimya?
 
Acheni walimu wajiongeze.Hivi yeye anataka kuwakamua wakati hawapi malisho stahiki? 480000 kwa mwezi,pango 60000-80000,nauli za uhakiki 30000,photocopy 6000,maji 28000,umeme 20000,chakula 120000,tahadhari 200000.Hapo hajatoa 10%.michango mbalimbali.Hivi katika hii hali unawezaje kuhoji walimu kupiga picha ama kuendesha boda?
 
Acheni walimu wajiongeze.Hivi yeye anataka kuwakamua wakati hawapi malisho stahiki? 480000 kwa mwezi,pango 60000-80000,nauli za uhakiki 30000,photocopy 6000,maji 28000,umeme 20000,chakula 120000,tahadhari 200000.Hapo hajatoa 10%.michango mbalimbali.Hivi katika hii hali unawezaje kuhoji walimu kupiga picha ama kuendesha boda?
 
Mkuu sasa Huyo mwalimu atapata wapi muda wa kuandaa somo ili madent wapate kilicho bora?ataishia tuu kuzuga class ,mind u kwamba mwalimu in MTU was kusoma muda wote
Tgts d wakikata makato yao toka 716000 inabaki 400000+ hapo hajaenda kukopa bank, ana familia zinamtegemea alipe nyumba, chakula na mavazi. Waache waingie huko tu
 
Acheni walimu wajiongeze.Hivi yeye anataka kuwakamua wakati hawapi malisho stahiki? 480000 kwa mwezi,pango 60000-80000,nauli za uhakiki 30000,photocopy 6000,maji 28000,umeme 20000,chakula 120000,tahadhari 200000.Hapo hajatoa 10%.michango mbalimbali.Hivi katika hii hali unawezaje kuhoji walimu kupiga picha ama kuendesha boda?
Hakika maana walimu hawana posho wala vijisemina vya chai
 
bodaboda_0.jpg

Mkuu wa Mkoa amepiga marufuku kujiingiza kwa walimu katika biashara ya uendeshaji bodaboda na upigaji picha mitaani kwa sababu kunashusha kiwango cha taaluma kwa wanafunzi.

Telack alitoa katazo hilo juzi baada ya kupokea taarifa kuwa baadhi ya walimu wanatoroka shuleni na kwenda kufanya shughuli zao binafsi, ikiwemo ubebaji abiria kwa pikipiki.

Akizungumza na wakuu wa shule zote za manispaa ya Shinyanga, waratibu elimu na maofisa elimu, Telack alisema atawafukuza kazi walimu wanaokacha vipindi.

Kwa habari zaidi nunua nakala yako ya NIPASHE LEO

My take;
Roho inaniuma mpaka natamani kuhama nchi hii. Maisha ni watu na watu ndio sisi tuwajali basi waalimu wetu. Roho imeninyonga nyonga asubuhi hii kwa hii taarifa. Inauma walahi
Huyo mkuu wa mkoa kama amefanya utafiti kwamba walimu hao hawaingii madarani badala yake wanaendesha bodaboda basi ni sawa kabisa kuzuia illa kama hajafanya uchunguzi wowote basi ni mwendelezo wa mizuka. Nijuacho mimi ni kosa mtumish wa umma kushuhulika na shughuli zake binafsi saa za kazi na kama hao walimu wanaendesha hizo boda na hawaendi kazin kufundisha basi ni haki kuwakataza tena na kuwachukulia hatua kali za kinidhamu lakin kama wanatimiza majukumu yao ya kiualimu na hizo boda wanaziendesha nje ya saa za kazi ,kuna haja ya kupima kiwango cha uelewa kwa baadhi ya viongozi.huenda wamewehuka na madaraka.
 
Back
Top Bottom