SihamiTZ
Member
- Dec 17, 2016
- 17
- 8
Mkuu wa Mkoa amepiga marufuku kujiingiza kwa walimu katika biashara ya uendeshaji bodaboda na upigaji picha mitaani kwa sababu kunashusha kiwango cha taaluma kwa wanafunzi.
Telack alitoa katazo hilo juzi baada ya kupokea taarifa kuwa baadhi ya walimu wanatoroka shuleni na kwenda kufanya shughuli zao binafsi, ikiwemo ubebaji abiria kwa pikipiki.
Akizungumza na wakuu wa shule zote za manispaa ya Shinyanga, waratibu elimu na maofisa elimu, Telack alisema atawafukuza kazi walimu wanaokacha vipindi.
Kwa habari zaidi nunua nakala yako ya NIPASHE LEO
My take;
Roho inaniuma mpaka natamani kuhama nchi hii. Maisha ni watu na watu ndio sisi tuwajali basi waalimu wetu. Roho imeninyonga nyonga asubuhi hii kwa hii taarifa. Inauma walahi