Waafrika wengi wanatamani mapinduzi kama ya Niger na Burkina Faso. Ufisadi unawakera na kuwachosha

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
1,126
4,169
Waliofanya mapinduzi huko Afrika ya Magharibi kwa sasa wanaonekana ni mashujaa.

Kila kona kwenye mitandao ya kijamii wamapostiwa kuwa ni mashujaa

Ni dhahiri sasa waafrika wengi wamechoshwa na ufisadi na matumizi ya madaraka mabaya

20230813_164038.jpg
 
Subiri ukifika Muda wa utawala wa mabavu kwenye hizo tawala za kijeshi ndio uongee. Wewe unadhani ni Kwa Nini Raia wanavumilia utawala wa kiraia ? Kwa sababu utawala wa kiraia hauna ubabe na mambo mengine.

Utawala wa kiraia unaondoka Kwa kura ila utawala wa kijeshi unaondoka kama ulivyoingia, Kwa mapinduzi
 
Mapinduzi au machafuko huwa yanasababishwa na viongozi wenyewe wa serikali, hasa wanaposhindwa kuwatumikia waliowapigia kura na badala yake wakaanza kujinufaisha wao na familia zao huku hali ya raia ikizidi kutopea katika lindi la umaskini na uhitaji.
 
Waliofanya mapinduzi huko Afrika ya Magharibi kwa sasa wanaonekana ni mashujaa.

Kila kona kwenye mitandao ya kijamii wamapostiwa kuwa ni mashujaa

Ni dhahiri sasa waafrika wengi wamechoshwa na ufisadi na matumizi ya madaraka

Waliofanya mapinduzi Niger ni zaidi ya mafisadi. Serikali iliyopinduliwa Niger ni serikali iliyopo madarakani kwa kura za halali tena kwa asilimia zisizozidi 6.

Waliopinduwa hawatafanikiwa kwa kwa wao ndio mafisadi wa kwanza. Hayo yalikuwa ni mambo ya miaka ya mwanzo Afrika kuanza kujitawala. Sasa hapana, Waafrika tusikubali kabisa mambo hayo.

Tukikubali hayo, tutatumiwa milele.
 
Mapinduzi au machafuko huwa yanasababishwa na viongozi wenyewe wa serikali, hasa wanaposhindwa kuwatumikia waliowapigia kura na badala yake wakaanza kujinufaisha wao na familia zao huku hali ya raia ikizidi kutopea karika lindi la umaskini na uhitaji.
Hilo neno wapiga kura liondoe,hamna kiongozi wa afrika anayeingia kwa kura halali madarakani ndio maana hawawajali raia wao
 
Watu wengi huchoshwa na hata kukosa uvumilimu kabisa na serikali zao kutowajibika ipasavyo kutatua changamoto mbalimbali za wananchi, na kugeukia kunufaisha kikundi kidogo tu cha watu wachache kwa kisingizio tu cha kuwa eti, "serikali iliyopo madarakani ipo kupitia kwa kura za halali za wananchi"
Waliofanya mapinduzi huko Afrika ya Magharibi kwa sasa wanaonekana ni mashujaa.

Kila kona kwenye mitandao ya kijamii wamapostiwa kuwa ni mashujaa

Ni dhahiri sasa waafrika wengi wamechoshwa na ufisadi na matumizi ya madaraka
View attachment 2709847
Jambo la kupiga kura ni suala la mpito la kuichagua serikali, kuendana na ahadi na haiba ya viongozi wanaojitokeza kunadi sera za chama chao, na hatimaye kukabalika kuwa kinaweza kukabiliana na changamoto zinazowakabili wanachi katika muda husika.

Lakini uwajibikaji wa serikali ni suala la kudumu pale inapopewa dhamana kufanya hivyo kupitia chama fulani. Haipaswi kubweteka na kutafuta kutokuwajivika kwa visingizio vyovyote vile. Endapo ikithibitika haina dhamira ya kutekeleza majukumu yake kwa makusudi, njia mbadala hutafutwa kwa kulingana na "torelance level" ya jamii, lakini kwa ile iliyochoka na kukata tamaa sana, "the last resort" ni "coup d'etat'
 
Waliofanya mapinduzi huko Afrika ya Magharibi kwa sasa wanaonekana ni mashujaa.

Kila kona kwenye mitandao ya kijamii wamapostiwa kuwa ni mashujaa

Ni dhahiri sasa waafrika wengi wamechoshwa na ufisadi na matumizi ya madaraka
View attachment 2709847

Wameonakana mashujaa kutokana na sababu zilizowachosha mpk wananchi.ndio maana hadi hao wananchi wamesapoti hayo mapinduzi
 
Endelea kuungwa mkono na wajinga wenzako wasiojua mambo. Huko Niger na Bukrina Faso hayo sio mapinduzi ya kwanza. Miaka nenda rudi hizo nchi zina mapinduzi ila ndo nchi masikini hadi zinatia kinyaa. Kama Mapinduzi yangekuwa ndo maendeleo basi hizo nchi zingeongoza kwa maendeleo Afrika
 
Back
Top Bottom