Burkina Faso na Mali kwa pamoja zimewaonya Wakuu wa ECOWAS juu ya mpango wa uvamizi nchini Niger

masaga ndoshi

Member
Apr 3, 2015
46
81
Burkina Faso na Mali kwa pamoja zimewaonya Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) kwamba wakithubutu kuvamia Nchi ya Niger ili kuwakabili Wanajeshi waliompindua Rais wa Nchi hiyo basi itakuwa ni sawa na kutangaza vita na Nchi hizo pia na hawatosita kupigana ili kuwasaidia Wanajeshi wa Niger.

Kauli ya Burkina Faso na Mali inakuja siku moja tangu ECOWAS itishie kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya utawala wa Niger baada ya kumpindua Rais wa Nchi hiyo Wiki iliyopita ambapo ECOWAs iliwapa siku saba Wanajeshi wamrejeshe madarakani Rais aliyepinduliwa Mohamed Bazoum ambaye anashikiliwa mateka.

Burkina Faso na Mali ambazo pia zinatawaliwa Kijeshi baada ya mapinduzi, kwenye taarifa yao ya pamoja wamesema “Serikali zetu za mpito zinaunga mkono Waniger ambao wameamua kujikomboa wenyewe na kuchukua Mamlaka yao”

“Uvamizi wowote wa kijeshi kwa Niger itakuwa ni sawa na kutangaza vita kwa Burkina Faso na Mali pia na itapelekea machafuko ambayo yatauletea shida ukanda mzima, na hatutaki kushiriki kuiwekea vikwazo visivyo halali Niger”
 
Hao ECOWAS waache upumbavu wakitulize Mbona hawakumsaidia Gadafi alipovamiwa na mataifa ya nje waache unafiki
Aljazeera walikuwa wanatangaza kuwa kikao kilichotoa hilo tamko kilishinikizwa na wafaransa na wamarekani wanaotaka kulinda madini na rasilimali nyingine wanazopora huko.

Wagner PMC njooni haraka tukipige tumalizane na hawa wahuni.
 
Kabisa. Mi naamini majeshi ya Africa yapo vizuri sana. Hawataki mambo ya siasa. Ttzo ni kuleta mambo ya jeshi na kuyachanganya na siasa na mambo ya utawala. Hapo pagumu. Ndomana nchi nyingi zilizopinduliwa kijeshi hazina maendeleo. Otherwise kwenye jeshi kuna watu wanajua siasa, utawala na Maendeleo ya jamii ndo washike dola. Tofauti na hapo hamna kinachoweza kutokea
 
Sio uoga ila chukua nchi TANO tu za afrika zilizopitia njia hiyo halafu angalia mwananchi wa kawaida kafaidika nini? Tuanzie na Libya, Tunisia, Sudani, Sudani kusini n.k Nje ya Afrika Irak na Siria. Kama wananchi wamefaidika zaidi ya walivyokuwa kabla basi endelea kutangaza idolojia yako.
kwa hio mkuu tuendelee kukanyagiwa shingoni tuvumilie tuu?. Tusipamanie vizazi vyetu vijavyo? cost zipo haziepukiki ila manufaa kama yatakuwepo hamna namna.
 
Hapo kichapo lazima kiende sio kwa sababu wanajali sana hayo mapinduzi yao; ila zuio la uranium kwenda ulaya ni kucheza na national security ya EU katika kipindi hiki bado kuna mgogoro na Russia kwenye nishati.

Ni swala la muda asiporuhusu uranium kwenda France au kupata suluhu ya haraka kwenye hiyo Issue; kichapo lazima kiende Niger kwa namna moja au nyingine.
 
Burkina Faso na Mali kwa pamoja zimewaonya Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) kwamba wakithubutu kuvamia Nchi ya Niger ili kuwakabili Wanajeshi waliompindua Rais wa Nchi hiyo basi itakuwa ni sawa na kutangaza vita na Nchi hizo pia na hawatosita kupigana ili kuwasaidia Wanajeshi wa Niger.

Kauli ya Burkina Faso na Mali inakuja siku moja tangu ECOWAS itishie kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya utawala wa Niger baada ya kumpindua Rais wa Nchi hiyo Wiki iliyopita ambapo ECOWAs iliwapa siku saba Wanajeshi wamrejeshe madarakani Rais aliyepinduliwa Mohamed Bazoum ambaye anashikiliwa mateka.

Burkina Faso na Mali ambazo pia zinatawaliwa Kijeshi baada ya mapinduzi, kwenye taarifa yao ya pamoja wamesema “Serikali zetu za mpito zinaunga mkono Waniger ambao wameamua kujikomboa wenyewe na kuchukua Mamlaka yao”

“Uvamizi wowote wa kijeshi kwa Niger itakuwa ni sawa na kutangaza vita kwa Burkina Faso na Mali pia na itapelekea machafuko ambayo yatauletea shida ukanda mzima, na hatutaki kushiriki kuiwekea vikwazo visivyo halali Niger”
Waafrika ni manyumbu kbs , siungi mkono kushikwa mkono na jeshi , kwavile hatuoni mbali ila ukifika wkt watalia na kusaga magego , kile cheo hupewa mwanasiasa kwa minajir mingi tu
 
Back
Top Bottom