Nadhani umeongea hayo ili uendelee kuhalalisha kwamba the guy deserved to be killed by police na kwamba, kama ni kuuawa, black wanauana wenyewe kwa wenyewe zaidi kuliko wanavyouazwa na polisi! In short, unaongea lugha ile ile ya White Supremacy! Lakini wakati unajaribu kuhalalisha kwa staili hiyo, ama kwa makusudi au kwa kutojua unashindwa kueleza ukweli wa historia yake tangu atoke jela zaidi ya miaka 5 iliyopita! Ama kwa makusudi au kwa kutojua unaacha kusema baada ya kutoka jela akaamua kujihusisha sana na masuala ya kidini huku akiwa mentor kwa vijana! Ama kwa kutofahamu au kwa makusudi umeacha kusema miaka michache iliyopita alifikia hadi kutengeneza video kuwaasa vijana kuachana na gun violence!!
Ama kwa makusudi au kwa kutojua unaacha kusema jamaa alilazimika kutoka kwako Texas na kuhamia Minessota kwavile pande za home aliona ni kama bad influence kwake kwa sababu kote alifahamika kama OG! Ama kwa kutofahamu au kwa kufahamu unaacha kusema baada ya kufika Mineapolis akaamua kutafuta kazi ili aishi kama raia wengine, na ndio maana hakuona taabu kufanya kazi kama mlinzi! Alifanya kazi ya ulinzi sehemu gani? Kwenye Makazi ya Watu Wasio na Makazi ambayo yapo chini ya usimamizi wa kanisa!!
Ama kwa kutofahamu au kutojua unaacha kusema katika harakati zake za kutaka aishi kama raia kama raia mwema ndipo akaamua kujifunza kuendesha malori na baadae kuwa truck driver! Ama kwa kutofahamu au kwa kutojua unaacha kusema ni tuhuma kwamba alifanya manunuzi kwa fake $20 ndiyo sabababu iliyoondoa uhai wake!!
Yaani seriously bado unaendelea ku-justify kuuawa kwa mtu wa aina hiyo eti kisa tu aliwahi kufungwa kutokana na ujambazi?! Na kwa maisha aliyokulia, na kitongoji alichokuwa anaishi, hata kama haiwezi kuwa justification lakini pia hakuna anayeweza kushangaa kusikia at his early 20's to 30's alikuwa ni mtu wa visanga! Na ni kutokana na ukweli huo ndio maana ilisemwa washikaji zake wengi hata hiyo 30 years hawakuigusa!
But all in all, hata kama bado angekuwa ni mhalifu, kwako unaona alistahili kuuawa huku anajiona namna ile?! Hivi ni kipi hasa kinachokusukuma kutetea mauaji ya kishenzi namna ile?!