Waafria tuamkeni kifikra

and 100 others

JF-Expert Member
Feb 3, 2023
732
2,194
Muafrika anaabudu Mungu kutoka arabuni na Middle East, hivi Mungu ana upendeleo kiasi hiko ashukie arabuni na Middle East pekee?

Wazee wetu walipokuwa wakitoa kafara ya wanyama wageni wakawaambia huo ni uchawi na ni dhambi, lakini kwenye biblia agano la kale kafara zilikuwa zinatolewa na wanasema wana muabudu Mungu.

Mungu wa Africa naamini yupo, ni vile mmesahaulishwa na wageni.

Hivi Maasai na Sandawe katika mila zao na desturi na hawafahamu kama kuna Bible na Quran wanapata dhambi kutoka kwa Mungu wa arabuni na Middle East kufuata mila zao na desturi ambazo zinakinzana na kukatazwa na dini za kuletwa? Mungu anae walaani anatumia vigezo vipi? Ana huruma huyo Mungu?

Umezaliwa porini, ukakulia porini, wazazi wako wamekuambia mila zetu ni kuoa wake 12, anakuja mzungu anakuambia ni dhambi oa mmoja na muarabu anakuambia wanne mwisho, wewe kosa lako hapo lipo wapi? hufahamu kama kuna bible wala quran, hio dhambi unaipata kwa vigezo vipi?

Africa tunaonekana gorilla tu mbele ya watu weupe, licha ya kujifanya mnakufa kwa ajili ya kutetea dini zisizokuwa na nyuma wala mbele, wengine wakijitoa mhanga kabisa, wengine wanakuambia nchi fulani ni wateule wa Mungu. Pumbavu kabisa.

Congo mauaji ya kila siku ni zaidi ya yanayoendelea Middle East, lakini kwa sababu Africa ni kama wanyama pori unaonekana huna thamani, hakuna double standards kwenye media,.


King Leopold II of Belgium aliua Congolese zaidi ya milioni 15, lakini story ya Hitler kuua jews 6 million ni habari kuliko Africans waliouawa kinyama na mzungu.

Tumedanganywa.
 
Tafakari Kuhusu mungu unaemwabudu kama keshawahi kukufunulia walau matumizi kadhaa ya raslimali zilizo chini ya ardhi yako, dhahabu, almasi, tanzanite, nk. Kama bado basi MUNGU wako halisi kaamua kususa sababu umeamua kumtenga
Mungu yupi huyo katokea Uarabuni?
 
Mungu wa kweli kwangu hana viashiria vya uarabu, bahati mbaya nmekua ktk jamii iliyomtenga kabisa

Nkisema me si muislamu wala mkiristo jamii inayonizunguka huhitimisha kwa kuniita mpagani, kuna ushenzi sana ndani ya damu ya mtu mweusi.
Mungu yupi huyo katokea Uarabuni?
 
Kweli upokee imani ya mzungu na kupuuza imani yako!!! Tumekwisha. Ujue kwamba ukristu ni "uzungu" na uislamu ni "uarabu ". Uafrika tumeuchimbia wapi?? Please! Come out from the cave, we are completely enslaved.

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
That's a genius level of thinking lakini wajinga na wapumbavu watakuona huna akili kwa taka walizowekewa vichwani mwao.
 
Mungu ni Mmoja tu kwa wote,

Hata hizi bibilia huenda ziliandikwa kuua tamaduni zetu tufate zao iwe rahisi kututawala
 
Back
Top Bottom